Update : Ni John Pombe Magufuli
Mkuu ahsante kwa mchango, hapa turejee nyuma.hilo ndilo lililotarajiwa kwa sababu ulizozieleza hapo juu, he was the best candidate among ya wale walioingia top 3, pia ni mnufaika wa mnyukano kati ya team Membe na team Lowassa.
waiting for the last part, udhaifu wa upinzani kutoa ruum kubwa ya coverage kwa mchakato wa Dodoma kwa wao kukaa kutokua na shocking activities na kutegemea mvurugano wa CCM, na wht is the way forward UKAWA wafanyaje kukabiliana na CCM iliyoimarika sio kwa umoja wao bali kulinda interest zao
Mkuu Rev. KishokaNguruvi3,
Ukawa kama wakiwa smart, wangeweza ku-target vijana na wanawake wa CCM ambao wako marginalized.
January Makamba alitumia muda mrefu kujenga base kupitia vyuo, John Mnyika anatumia muda kupigania maslahi ya jimbo.
Kuna haja ya Chadema, CuF, NCCR kuanza kubadilisha Guards. Mtu kama Himid angekuwa chambo kizuri sana kwa Ukawa kugombea Muungano kama CUF wanaweza kuwa open minded na kuachana kung'ang'ania Zanzibar.
Njaa ya kukimbilia IKulu pekee, ndiyo itakayowaangusha Ukawa. Aidha kutarajia fall out na makombo ya CCM au viporo vya CCM si tija.
I trully hope kutatokea change of guard ndani ya hivi vyama pamoja na kujibadilisha kimfumo na utendaji kuhakikisha kuna balance katika bunge.
Kinana keshatangaza kuwa wanafanya reforms ndani ya chama na kuwavua mawaziri na watendaji wakuu wa Serikali sehemu kuu za maamuzi ya kichama ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji.
Ukawa tuliwashauri hili, kuunda timu ya kukaa bungeni pekee kama serikali na timu ingine kichama kutangaza sera na itikadi. Lakini sidhani kama hili lilizingatiwa au kupewa kipaumbele.
Mengi ya kujifunza mwaka huu!
Tanzania hatuna upinzani wa kuweza kuwasaidia watanzania kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine. Wapinzani wangekuwa na nia ya dhati wangejiunga na umoja wao kama vyama vilivyounda UKAWA na kuhakikisha wanaisimamia serikali kuandikisha watu wote wenye vigezo vya kupiga kura. Hii ingewasaidia sana kuitoa CCM madarakani. Wasimamie zoezi zima la kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.
Nguvu ya umma.
Watanzania ni waoga na wasahaulifu sana. Ukiangalia toka JKikwete aingie madarakani hadi leo madudu mengi yamefanyika, kuna ufisadi wa wazi sana na hadi waziri mkuu kujiuzulu. Lakini sisi tumesahau kiasi kwamba huyo waziri mkuu tunamuona amegeuka lulu.
Maswala nyeti yanayohusu maslahi ya taifa tunayasahau sana. Watu wanaendelea na shughuli zao kana kwamba hayawahusu kumbe wao ndo wahanga wakuu wakubwa.
Binafsi naona dhahiri kuwa ukombozi tunaoudhania utatokea 2015 hautatokea kwasababu wananchi hatujatambua nguvu tulionayo.
Mkuu Msukumo wa hali ya hewa ya kisiasa, kijamii na kiuchumiupo. Kuna matatizo yanayojitokezaMkuu inawezekana kuwa Tanzania imefika mahali tulipokuwa tunapasubiri.
Inawezekana uchaguzi wa safari hii ukaleta mabadiliko makubwa ya kuifanya Tanzania ivuke kutoka kwenye lindi za siasa za chama kimoja kivitendo na kuwa za chama zaidi ya kimoja.
Tukiweza kuwa na makubndi mawili yenye nguvu ndani ya bunge, kuna uwezekano kuwa Tanzania ikawa ya maana zaidi kuliko vyama. naweza kukubaliana na wewe kuwa vyama vyetu vya kisiasa bado haviko tayari, na hata wananchi hawako tayari kuleta mabadiliko kivitendo...lakini hali ya hewa kisiasa, kiuchumi na kijamii inaweza kuwa msukomo.
Membe aliaga kamawengine. Hakuna utaratibu wa kuadhibu wanaoongopa. Mfumo umejengwa kuleana nakuvumiliana.By the way, tukiangalia wanasiasa wetu. Kama sijakosea nakumbuka mh Membe alisema hatagombea tena ubunge, sina uhakika sana. Ningependa kujua kama ni kweli atafanya hivyo, au alikuwa anadanganya tu, na kama kuna utaratbu wowote wa kuwachukulia hatua wanasiasa wanaodanganya.
Naufatilia kwa karibu mjadala huu, na ahsanteni nyote kwa michango yenu.....
3. Amina Ali-akiwakilisha kundi la muungano
....…
Alinda , CCM haiwezi kutoa elimu ya Uraia. Wanafahamu huo unaweza kuwa ndio mwisho wao. Wanachokifanya ni kwenda kula na wananchi au kubeba matofali mawili ili wananchi waone hiyo ndiyo haki zao.Mkuu Nguruvi3 uliongea ni kweli kuhusu wananchi wa vijijini kuamini kuwa bila CCM maisha yao hayaendi.. Matatizo kwao imekuwa ni sehemu ya maisha yao hivyo hawaoni kero, kwao muhimu ni mvua zinyeshe walime, wavune, washerekea mavuno basi kwao wanakuwa wameridhika.
Hawa watu hawaelewi kuwa ni haki yao kupata maji, umeme, mashule, kujenga barabara, serikali kutengeneza vyanzo vya ajira kwa ajiri ya watoto wao, ni wajibu wa serikali kuhakikisha hakuna mtu anayekosa matibabu na nk. Hawa watu wanaamini kabisa kuwa kukosa dawa hospitali ni kawaida, watoto kurundikwa madarasani ni kawaida, shule kukosa waalimu ni kosa la waalimu, kukosa maji ni adhabu kutoka kwa mwenyezi Mungu na nk.
Hawa watu wanahitaji elimu ya uraia hii elimu kwa bahati mbaya au nzuri hawezi kutolewa na serikali maana serikali kuwapa elimu ya haki zao ni kama kujichongea.. Elimu hii inabidi itolewa na vyama vya siasa, wapenda mabadiliko, wanaharakati na nk.Lakini kwa bahati mbaya kutokana na ukosefu wa pesa, vikwazo mbali mbali kutoka serikalini inakuwa ni vigumu kutoa elimu hii. Hivyo basi kujikuta watu wengi waishio vijijini kuendelea kuichagua ccm pamoja na umasikini mkubwa walionao.
Tatizo lingine linalokumba siasa yetu za Tanzania au za Afrika kwa ujumla ni ubinafsi wa viongozi, viongozi wetu wa vyama vya siasa ni wabinafsi anapokuwa kiongozi malengo yake si kukuza hicho chama bali malengo yake ni yeye kama yeye kufaidka kwa namna moja au nyingine na uongozi wa hicho chama.
Tukiangalia baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikifanya vibaya mwaka hadi mwaka lakini huoni uwajibikaji wa uongozi pale wanapopoteza kura/wanapopata kura chache kulingana na chaguzi zilizopita. Utakuta kiongozi tena msomi kabisa chama chake kinadidimia kila mwaka lakini hashutuki na kuachia ngazi bali atang´angánia mpaka chama kife au kisahaulke kabisa, sasa mtu unajiuliza hivi hawa viongozi akili zao huwa ziko sawa kweli? huyu mtu anaweza ana mapenzi mema na chama chake kweli?