Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Juma Homera amesema tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mdude Nyagali, huku akiahidi Sh5 milioni kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa hai au amekufa...
Salaam,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dsm Muliro J. Muliro Leo tarehe 05 May 2025, ataongea na waandishi wa habari.
Kama hatongelea utekaji nashauri akae kimya tu.
Ndugu zetu wanapotea. Polisi wamevunja Miguu wananchi wa Tanzania.
Je, Utawala wa Sheria Tanzania umeishia wapi...
https://www.youtube.com/live/IKo0vWFgOXo?si=VROW5KWJw-PEMKcw
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), leo Mei 5, 2025 kimezindua ripoti ya hali ya haki za binadamu nchini kwa mwaka 2024.
Ripoti hiyo imezinduliwa Jijini Dar es Salaam ikiwa ni ripoti ya 23 tokea walipoanza utaratibu...
Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na mwananchi mmoja ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa akiwatuhumu askari wawili kupitia mitandao ya kijamii kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi pamoja na kumuahidi kumpatia fedha.
Kufuatia taarifa hiyo, Jeshi la...
KUKEMEA NA KULAANI VIKALI SHAMBULIO DHIDI YA NDUGU MDUDE NYAGALI
Dar es Salaam, 02 Mei 2025
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinalaani na kukemea vikali shambulio dhidi ya ndugu Mdude Nyagali lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2025 akiwa nyumbani kwake mkoa wa Songwe. Hivi...
MKuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Twange amemuagiza Mkuu wa Polisi, Wilaya ya Kipolisi Kimara/Ubungo kuwatafuta na kuwakamata Watu wote waliovamia na kuchoma moto Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Msewe, na kuteketeza nyaraka na samano zote za ofisi hiyo.
Tukio hilo la kuvamia na kuchoma moto...
Ibada hii imefanyika katika Usharika wa Agape Kahama, Jimbo la Magharibi Kahama Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria. Imeongozwa na Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Baba Askofu Dkt. Yohana Nzelu amegusia umuhimu wa maridhiano kwa Serikali.
Video: Kitenge TV
Bibi wa miaka 72 mkazi wa mtaa wa Mwanyanje, kata ya Igawilo jijini Mbeya ambaye aliingiliwa na watu wasiofahamika nyumbani kwake anategemewa kujengewa nyumba na Dkt. Tulia Ackson
Ikumbukwe bibi huyo ni moja ya watu wanaoishi katika mazingira magumu ambao walifikiwa na bendera ya Upendo...
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiziguzigu Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Mwl. Martin Runaku Mpemba, amefariki usiku wa Aprili 3 katika Kijiji cha Kibingo Kata ya Kiziguzigu, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma, Christopher Palangyo...
Watu 'wasiojulikana' wamefika katika Kitongoji cha Mchango wa Hela, Pwani, na kubomoa nyumba kadhaa huku wakichoma moto baadhi ya vitu, wakidai kutumwa na mmiliki wa eneo hilo.
Tukio hili limezua taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambao wamemlilia Rais Samia Suluhu Hassan awasaidie...
Lucy Mrimi, dada wa Daniel Chonchorio Nyamhanga, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye hajulikani alipo mpaka muda huu ameiomba serikali kuingilia kati juhudi za kumtafuta ndugu yao, akieleza kuwa kuna ushahidi wa mashuhuda waliomuona akichukuliwa na watu...
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara kimewasilisha ripoti maalum kwa Kanisa Katoliki, ikielezea matukio ya watu waliouawa au kupotea katika mkoa huo. Sambamba na hilo, chama hicho kimetumia nafasi hiyo kueleza msimamo wake wa No Reform No Election, ukimaanisha kwamba kitazuia...
Wakuu,
Mfanyabiashara wa huduma za kifedha (wakala), Davis Mandari (48), mzaliwa wa Kilimanjaro na mkazi wa Kwa Mrefu, jijini Arusha, ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Inadaiwa kuwa kabla ya kutoweka, alituma ujumbe mfupi kwa mke wake akidai kuwa amechukuliwa na jeshi la...
Familia ya Mariamu Ibrahim Juma, mkazi wa Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu, Mjini Geita, imeiomba serikali kupitia Jeshi la Polisi kusaidia kumtafuta mtoto wao, Abdurahman Yunusu (24), ambaye ametoweka kwa siku 13 katika mazingira ya kutatanisha.
Pia Soma: Mfanyabiashara wa huduma za kifedha...
Wakuu hii ni kweli kuwa Mahinyila amesema vijana wa CHADEMA wanafanya mambo ya kihalifu, wakikamatwa wanataka chama kiseme wametekwa na watu wasiojulikana?
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Deogratius Mahinyila anazungumza na Vyombo vya Habari muda huu akizungumzia sakata la utekaji nchini huku akianza kueleza namna ambavyo Amani Manengelo, Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, alivyotekwa na kupotea tangu...
Method Damian Kumdyanko mkazi wa Sinza Dar Es Salaam anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wenye silaha siku ya Februari 28, 2025 nje ya geti la nyumba yake Sinza Dar Es Salaam.
Akizungumza na Jambo TV Tura Chaula ambaye ni rafiki wa kike wa Method na aliyeshuhudia tukio hilo amesema siku hiyo...
Mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake amechukuliwa kwa nguvu na Watu wasiojulikana ambao walikuwa wamebeba silaha na ripoti zinadai tukio hilo limetokea February 20,2025 saa saba mchana katika Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa ripoti za Mashuhuda Kijana...
Inasemekana kwamba tukio limetokea jana (20.2.2025) majira ya saa saba mchana.Mkoa wa Pwani, Kibaha, Njuweni, sheli ya Puma.
Huyu kijana (boda boda) alikuwa anapambania maisha yake, akaomba msaada. Wananchi waliposogelea eneo la tukio, alishuka dereva wa hiyo Noah nyeusi ya watekaji akiwa na...
Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA (BAVICHA) Kanda ya Victoria limelaani na kukemea matukio ya watu kutekwa yanayoendelea kujitokeza nchini.
Akitoa kauli hiyo, tarehe 19 Februari 2025 Mwenyekiti wa BAVICHA Kanda, Fred Michael akiwa kwenye kikao cha baraza hilo Jimbo...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.