Miaka ya 1990 kurejea nyuma, wanaume tulikuzwa na familia zetu kuwaona wanawake kama viumbe wa kuwalinda na kuwajali sana.
Hii haikuwa Tanzania tu bali ulimwenguni. Ukitazama filamu,wanaume walikuwa wakisalimia wanawake wanawavulia kofia na kuinamisha kichwa kidogo na kuwaita majina ya heshima...