uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. MK254

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Ulaya wasifia uchaguzi wa Kenya na kusema umeweka kiwango kipya Afrika

    Vyombo vyote vya habari vina takwimu za matokeo kituo kwa kituo, data zipo kote, kila mmoja yupo huru kukotoa na kuibua popote penye tashwishi au kasoro, binafsi sikumchagua Ruto, sikumpa kura yangu ila nimependa namna uchaguzi uliendeshwa kwa njia za wazi kabisa, Afrika haijatokea uchaguzi...
  2. BARD AI

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Chebukati: Makamishna wanne walishinikiza Uchaguzi urudiwe kinyume cha Sheria, Nilikataa

    Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi (IEBC) Wafula Chebukati, amesema aliwazuia kuingia eneo la Bomas Makamishna wanne waliokana kutambua matokeo ya Urais kwa kulazimisha uchaguzi urudiwe. Chebukati ameshikilia msimamo wake kuwa Makamishna hao walipata matokeo yote na walihusika katika shughuli zote...
  3. M

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi 2025 Watanzania tupige kura 5

    Heshima kwenu wakuu! Kama wengi tunavyojua watanzania tunatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025. Kwa kujifunza kutokana na uchaguzi mkuu uliomalizika nchini Kenya hivi karibuni ni wakati sasa kwa Tanzania kuendesha uchaguzi wa serikali za mitaa...
  4. BARD AI

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Madaktari kuchunguza mwili wa Afisa wa Tume ya Uchaguzi Kenya

    Madaktari wa Uchunguzi wataufanyia uchunguzi mwili wa afisa wa IEBC, Daniel Musyoka aliyekutwa amefariki baada ya kutoweka kwenye kituo cha Kura. Mchunguzi wa serikali pamoja na Daktari aliyeteuliwa na familia watafanya shughuli hiyo ili kubaini sababu za kifo cha Afisa huyo aliyetoweka kwa...
  5. chiembe

    JamiiForums Tanzania Funzo uchaguzi wa Kenya: Wananchi wamechagua uchumi badala ya mabadiliko ya vifungu vya katiba, CCM wako njia sahihi ya kujenga uchumi

    HANDSHAKE kati ya Raila Amolo Odinga na Uhuru Kenyata ililenga kufanya mabadiliko makubwa ya kikatiba ili kuweka vyeo, pamoja na mambo mengine mengi. William Rutto aliwaambia wakenya kwamba shida yao sio katiba nyingine, shida yake ni kukomboa mama mboga na mtu wa bodaboda, kwamba shida ya...
  6. C

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Hili lisipofanyika naiona Damu Kubwa sana inaenda kumwagika Kenya baada ya huu Uchaguzi Mkuu

    Ili Kukonga nyoyo za kila upande Hasimu Team Ruto na Team Odinga yeyote atakayetangazwa rasmi na Supreme Court ya nchini Kenya kuwa ndiye Mshindi' amteue Mpinzani wake kuwa Waziri Mkuu Cheo ambacho kwa Katiba ya Kenya hakipo ila katika Mazingira tatanishi na kuleta Usawa na Utulivu huwa...
  7. Zanzibar-ASP

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 MAHESABU YA KURA: Kumbe elimu ya Kenya ipo chini sana na upeo wa wakenya upo chini mnoo!

    Kituko kikubwa cha karne kuhusu hesabu leo kimeonekana huko Kenya baada ya makamishina wanne wa tume ya uchaguzi waliotangaza kujitoa kwenye mchakato wa kutangaza matokeo ya urais kuja na hoja finyu za ukilaza wa mahesabu. Mbali na sababu zingine walizozitoa, kubwa lilikuwa ni wao kujenga hoja...
  8. L

    JamiiForums Tanzania Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

    Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja...
  9. R

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Sikiliza Busara za Ansbert Ngurumo kutoka juu ya funzo kutoka uchaguzi wa Kenya

    Uchambuzi kutoka akili kubwa. Changia hoja na si matusi. Challenge hoja zake, then JF itakuwa na Great Thinkers. Msikilize CC Tundu Lisu; Mbowe Freeman, Godbless Lema
  10. The Sheriff

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Raila Odinga akataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa Rais

    Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais nchini Kenya na kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anatarajiwa kuzungumza na Wakenya kupitia vyombo vya habari leo Jumanne, Agosti 16, 2022. Taarifa hiyo iliyotolewa na Dennis Onsarigo ambaye amekuwa msimamizi wa mawasiliano katika kampeni...
  11. Lady Whistledown

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Afisa wa Uchaguzi aliyetoweka akutwa amefariki

    Mwili wa aliyekuwa Msimamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika Jimbo la Embakasi Mashariki, Daniel Mbolu Musyoka, ambaye alitoweka akiwa katika eneo lake la kazi Agosti 9, umeokotwa Kajiado Maafisa wa Polisi wa eneo hilo, wamesema walitahadharishwa kuhusu kuwepo kwa mwili wa...
  12. comte

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi unatugawa sana -bora turudi kwenye uchifu

  13. comte

    JamiiForums Tanzania Tume Huru ya Uchaguzi imemebaki Tume ya Uchaguzi ya Tanzania

    Huwa siamini hata kidogo kama upo uwezekano wa kupata tume huru ya uchaguzi kwa namna kama Kenya walivyofanya; au hata Zanzibar walivyowahi kufanya. Kwa kilichotokea Kenya kupitia baadhi ya wajumbe kuyakana matokeo ya kazi yao natangaza kuwa Tanzania tuna tume bora na huru ya uchaguzi
  14. M

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Kuchafua uchaguzi wa Kenya kwa kisingizio cha ukabila ni kujilisha upepo

    Nianze kwa kuwapongeza ndugu zetu wakenya kwa kumpata Rais aliyetokana na uchaguzi ulio huru, haki na uwazi ambao pengine siyo somo kwa waafrika tu bali pia hata katika baadhi ya mataifa ya mabara mengine. Humu wamejitokeza wanaJF ambao wamejipa kazi ya kuchafua jitihada nzuri Sana zilizo...
  15. Roving Journalist

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 IEBC: William Ruto ameshinda Urais kwa 50.4% dhidi ya 48.8% za Raila Odinga

    Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC) imemtangaza aliyekuwa Naibu Rais, William Ruto (55) kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano kwa tiketi ya Chama cha UDA kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022 Tume imesema Ruto amepata Kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49 huku akifuatiwa na Raila...
  16. Mbaga Jr

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Uchaguzi wa Kenya: Mkutano wavurugika kwa fujo, watu wapigana

    Inasikitisha sana wakuu
  17. S

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Uchaguzi Mkuu wa 2025, nasi watanzania tutumie vifaa vya teknolojia (TIEMS). Vinginevyo...

    2025 nitagombea ubunge kwenye Jimbo fulani. Lkn ninasubiri kuona Kama nchi yetu itatekeleza mambo 3. 1. Katiba itabadilishwa. 2. Tume huru ya uchaguzi itaundwa. 3. Vitanunuliwa vifaa vya kielektroniki vya kunakiri na kuposti matokeo toka vituo vya kupigia kura kwenda tovuti ya Tume:- Tanzania...
  18. T

    JamiiForums Tanzania Hata kama Mbowe akiwa Mwenyekiti na Lissu Mkurugenzi wa NEC Mnyika awe IGP bado CHADEMA ya sasa haishindi uchaguzi

    Ukweli ni kwamba hali ya kisiasa ya sasa hapa nchini inakatisha tamaa sana. Ukisoma maandiko mengi humu ndani ya wenye mrengo wa upinzani, wanailaumu ccm kuwadhoofisha huku wakisahau kwamba hakuna chama siasa chenye jukumu la kuruhusu chama pinzani kisitawi. Ukiwa kama mpinzani unalazimika...
  19. Iam__junior

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi Wa Kozi

    Habari Wana JF. Naomba Kuuliza Kipi Hupewa Kipaumbele Katika Uchaguzi Wa Kozi.?? Ama Nini Mtu Aweze Kuangalia Katika Uchaguzi Wa Kozi.?? NB:Achana Na Ajira
  20. MIMI BABA YENU

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya2022 Hakika hakuna cha kujifunza kutoka katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya

    Nikiwa napitia katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini niliona baadhi ya wanaharakati, wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani wakidai kuwa Tanzania inapaswa kujifunza kutoka uchaguzi Mkuu wa Kenya. Wakidai kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki. Kwa ufuatiliaji nilioufanya katika...
Back
Top Bottom