BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,365
- 8,098
Uchaguzi Mkuu wa Kenya umefanya nijue umuhimu wa utawala wa sheria na Katiba hasa kwenye masuala muhimu ya kusimamia haki za msingi za wananchi.
1. Hakuna Kupita bila Kupingwa
2. Mtandao Haukuzimwa (No VPN Needed)
3. Majukumu ya Vyombo vya Dola (Kulinda usalama wa Wapiga Kura na zoezi hilo)
4. Wagombe Binafsi Kushiriki Uchaguzi
5. Umuhimu wa Tume Huru ya Uchaguzi
Uwepo wa Tume Huru unaondoa mambo mengi kutokea ikiwemo wizi wa kura au upendeleo kwa wagombea wa upande wowote.
1. Hakuna Kupita bila Kupingwa
Kenya imeonesha kuwa wananchi ndio waamuzi wa mwisho wa nani wanataka awe kiongozi wao na si vinginevyo
2. Mtandao Haukuzimwa (No VPN Needed)
Licha ya msuguano mkali wa wagombea pia kutofautiana kwa Naibu Rais Ruto na Rais Kenyatta hakujafanya serikali ya nchi kuzima mitandao, kila traarifa zinapatikana bila matumizi ya VPN.
3. Majukumu ya Vyombo vya Dola (Kulinda usalama wa Wapiga Kura na zoezi hilo)
Tumeshuhudia kwenye baadhi ya nchi majeshi yakitumika kuingilia mchakato wa Chaguzi ikiwa ni pamoja na kukamata wapiga kura wa vyama vya upinzani, lakini kwa Kenya hali imekua tofauti, Wakenya wanapiga kura kwa uhuru na kulindwa katika kutimiza haki yao ya kikatiba.
4. Wagombe Binafsi Kushiriki Uchaguzi
Hili ni kati ya mambo ya kipekee kabisa kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo wagombea binafsi wasio na vyama vya siasa wameshiriki uchaguzi na kupigiwa kura bila shida yoyote.
5. Umuhimu wa Tume Huru ya Uchaguzi
Moja ya masuala muhimu kwenye demokrasia ni pamoja na kuwa na chombo kinachoamua na kuendesha michakato ya uchaguzi. Kenya ni kati ya nchi chache za Afrika zilizofanikiwa kuacha suala la uchaguzi liendeshwe na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo haiingiliwi na mamlaka yoyote kwasababu viongozi na wafanyazi wake hawawajibiki kwa mamlaka nyingine isipokua Tume ya Uchaguzi.
Uwepo wa Tume Huru unaondoa mambo mengi kutokea ikiwemo wizi wa kura au upendeleo kwa wagombea wa upande wowote.