Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757


Sina la kusema, nimepigwa butwaa. Najiuliza kama ule nilioushuhudia nchini Tanzania mwaka 2020 ulikuwa ni uchaguzi kweli.

Tukubali tusikubali, huu uchaguzi nchini Kenya umetuvua nguo na kutuacha uchi wa mnyama na kama bado tunazo tuchutame.

Nafuatilia matokeo yanavyotiririka kwenye TV na kushuhudiwa na Dunia nzima, bila kusubiri ruhusa.

Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?

Salaam zetu kutoka Twitter

1660138926347.png

Kwa kweli tumevuliwa nguo...
 
Kenya mpaka wamefikia hapo walichapana na damu ikamwagika, naomba sisi tusipitie njia kama hiyo ila kuna mijitu inatulazimisha kufika uko kwa wizi wao wa kura
Masikini Prince Kunta, Tanzania mambo ni gizani gizani tu. Umewasahau wasiojulikana, umesahu utekaji, umesahau maiti kuokotwa kwenye viroba...pole sana ndugu yangu!
 
Sina la kusema, nimepigwa butwaa. Najiuliza kama ule nilioushuhudia nchini Tanzania mwaka 2020 ulikuwa ni uchaguzi kweli.

Tukubali tusikubali, huu uchaguzi nchini Kenya umetuvua nguo na kutuacha uchi wa mnyama na kama bado tunazo tuchutame.

Nafuatilia matokeo yanavyotiririka kwenye TV na kushuhudiwa na dunia nzima , bila kusubiri ruhusa ya wenye mtindio wa ubongo!
Mkuu, chaguzi za 2019 & 2020 chini ya wachafuzi wa CCM, upepo ulivuma na kuziacha nyeti za kuku hadharani bila kificho.
 
Namuona Kenyata anaenda kupiga kura akiwa hana rundo la maaskari na wanajeshi waliojihami kwa bunduki wakimzonga zonga

Huku kwetu wkt wa upigaji kura kule Dodoma tuliona Magu akiwa na lundo la wanajeshi wenye silaha za kivita utafikiri tupo Afghanistan
 
Back
Top Bottom