Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi maarufu kwa jina la Mzee Ruksa leo anatimiza miaka 90. Bado ana nguvu, mchangamfu, mcheshi na anapopata fursa, anawafundisha Watanzania matumizi ya Kiswahili Sanifu na kutoa ushauri juu ya umuhimu wa elimu na kuishi kwa amani na ushirikiano bila ubaguzi...