Yu wapi Bi. Hadija Mwinyi, mke wa pili wa Mzee "Rukhsa"

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu ndugu, jamaa na marafiki mliopo hapa. Kwanza kbs napenda kutoa pole kwa Raisi wetu mama Samia Suluhu Hassani, kwa familia ya mama yetu mama Janet Magufuli na kwa watanzania wenzang kwa kuondokewa na aliekuwa raisi wetu marehem John Pombe Magufuli.

Niingie sasa kwenye mada husika. Nakumbuka zamani wakati nipo mdogo niliwahi kusikia kuwa aliekuwa Rais wetu enzi zile mheshimiwa mzee Ally Hassan Mwinyi alikuwa na wake wawili yani bi siti Mwinyi na bi Hadija Mwinyi (ingawa kuna wengine walisema eti ana wake watatu) ila huyo wa 3 mimi sijawahi hata kulisikia jina lake.

Sasa basi miaka yote hiyo nimekuwa nikimuona Mzee Mwinyi akiwa na bi Siti Mwinyi pekee, huyo bi Hadija Mwinyi sijawahi kumuona.

Sasa swali langu je ni kweli mzee Mwinyi ana mke anaitwa Hadija? Na kama anae yuko wapi? Na ni kwanini huwa haongozani nae kama ilivyo kwa bi Siti Mwinyi?

Tafadhali mwenye kujua naomba anieleweshe huenda tulikuwa tunapotoshwa
 
Yule bi mkubwa atakuwa amezeeka kuliko mwinyi kwa hiyo nadhani atakuwa amepumzishwa mikiki ya kutembea muda wote na mhe. Mwinyi. Kwenye awamu ya kwanza ya Rais Mwinyi kuna siku niliona sijui alikuwa anaapishwa alikuwa na wote wawili pale uwanjani wa taifa alionekana ni mkubwa.

Halafu usipende kujua detail za mambo ya watu ,hasa wastaafu wetu waliofanya kazi nzuri. Kwani ukijua mstaafu wa 20 yes ago inakusaidia ni una usipojua inakupunguzia nini, hata weed ukiulizws undani wa maisha yakp uttang'aka na kuuliza.

Unayatakia nini maisha yngu.
 
Huyo bi Sitti nasikia alikuwa mjanjanja tangu kitambo! Ilifikia hatua hata Mwalimu alimponda mzee Ruksa eti anashauriwa na mkewe kufanya baadhi ya maamuzi!
 
Yule mwingine ana wa4 sema ni siri kubwa sana.

Gharib yeye kila mahala penye shughuli rasmi walikuwa wake zake wawili lazima wawepo tena wanapanda gari moja.
 
Mimi namuona sana sijui wewe au kwa kuwa wote wana rangi za kichotara unawafananisha. Wenzetu waislamu hawana unafiki kama sisi wakristo wa kuficha wake zao wote.
 

Attachments

  • Screenshot_20231216-074632_Facebook.jpg
    Screenshot_20231216-074632_Facebook.jpg
    254.7 KB · Views: 15
  • Screenshot_20231216-074457_Google.jpg
    Screenshot_20231216-074457_Google.jpg
    110.7 KB · Views: 22
  • Screenshot_20231216-075136_Chrome.jpg
    Screenshot_20231216-075136_Chrome.jpg
    219.4 KB · Views: 22
  • Screenshot_20231216-075408_Facebook.jpg
    Screenshot_20231216-075408_Facebook.jpg
    267.7 KB · Views: 19
Hii picha ndiyo itakuonyesha vizuri Bibi Sitti ni yupi na Bibi Hadija ni yupi, namba moja wa kwanza kushoto Bibi Sitti na wa pili kulia Bibi Hadija. Bibi Khadija anavaa miwani wakati mke mwenzake havai miwani.
 

Attachments

  • Screenshot_20231216-074632_Facebook.jpg
    Screenshot_20231216-074632_Facebook.jpg
    254.7 KB · Views: 14
Back
Top Bottom