Rais Dkt. Hussein Mwinyi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye mkutano wa Wakuu wa nchi SADC

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mwinyi.jpg

Dkt. Hussein Mwinyi akiagana na viongozi wa Serikali wakati akielekea nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC, kumuwakilisha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hii ni itakuwa ni safari yake ya kwanza Dkt. Mwinyi tokea kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar.

Huu ni mwanzo mzuri kwa manufaa ya JMT.

=====

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi tayari yupo nchini Msumbiji, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Malavane, Maputo, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo pamoja na gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake.

Mkutano huo wa siku moja unawahusisha wakuu wa nchi wanachama wa SADC na miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni masuala ya usalama na hatua za kukabiliana na vitendo vya ugaidi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Chanzo: TBC
 
Kwani Zanzibar sio member Kama ilivyo kwenye EAC? Kama sio ni heri wapewe membership, Zanzibar kufanya maamuzi kwa Niaba ya JMT duh!
Akienda kwenye mkutano,anaenda kama mwakilishi wa Rais wa Tanzania,haendi kama Rais wa Znz....

Mhe Samia angeweza kumtuma yeyote aende kumwakilisha either awe madarakani au asiwe madarakani

Mfano the late JPM alishawahi kumtuma mzee Mkapa na Mzee kikwete mara nyingi waende kumwakilisha.

Uwakilishi is not a big deal.
 
Akienda kwenye mkutano,anaenda kama mwakilishi wa Rais wa Tanzania,haendi kama Rais wa Znz....

Mhe Samia angeweza kumtuma yeyote aende kumwakilisha either awe madarakani au asiwe madarakani

Mfano the late JPM alishawahi kumtuma mzee Mkapa na Mzee kikwete mara nyingi waende kumwakilisha.

Uwakilishi is not a big deal.
Hayo yote nimekubali
Swali ni kwanini hajaenda mwenyewe?
Au anaanza kuwa paranoid of coup d'etat kama mwendazake?
 
Back
Top Bottom