King Kisali

JF-Expert Member
Nov 20, 2019
1,042
1,349
Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anategewa kuwa mgeni rasmi siku ya uzinduzi wa kitabu Cha maisha ya rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi al maaruf Mzee Rukhsa.

========

photo_2021-05-06_14-55-45.jpg

Rais wa Tanzania Samia Suluhu anatarajia kuwa Mgeni rasmi kesho May 08, 2021 kwenye Sherehe za uzinduzi wa kitabu cha simulizi ya maisha ya Rais wa Pili wa Tanzania Dkt. Ali Hassan Mwinyi kiitwacho “Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu”, uzinduzi utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Nyerere, Dar es salaam.

Kitabu hiki kimechapishwa kupitia mradi wa kuhifadhi kumbukumbu za Viongozi Wastaafu Tanzania na Afrika unaoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI, wengine watakaohudhuria ni Rais Mstaafu Dr.Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu Dkt. Shein n.k

Habari zaidi....

1620649048246.png

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema aliposoma Kitabu cha maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa mara ya kwanza aliyokutana nayo yalimshitua lakini alipokirudia, kimemtoa woga huku kikiacha mafunzo mengi kwa viongozi ikiwamo la kutambua kwamba uongozi si lelemama.

Akizindua kitabu hicho ‘Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha yangu’ Samia alimtaja Mzee Mwinyi, maarufu Mzee Rukhsa kwamba ni Baba wa Mageuzi, alisema kitabu hicho ni fundisho kubwa kwake kama Rais kwani kinafariji, kinatoa mwongozo wa nini kinatakiwa kufanyika kwa kiongozi hasa wa ngazi kubwa ya urais.

Kitabu hicho kinachoelezea maisha ya Mzee Mwinyi aliyeongoza Tanzania tangu mwaka 1985 hadi 1995, kinaeleza tamu na chungu wakati wa uongozi wake.

“Nimekisoma kitabu chako mara mbili. Nilipokisoma mara ya kwanza, niliyokuta ndani nikashituka kidogo nikasema mtu wa maarifa na heshima zote , Mzee Mwinyi yamempata haya, mimi je?

Lakini kutokana na ufasaha wa lugha, nikakirudia na woga ukanitoka nikasema kazi iendelee,” alisema Samia.

Alisema kitabu hicho ni hazina kubwa kwa nchi na vizazi vijavyo kwani kimeeleza maisha yake yote ya kikazi na tangu akiwa mtoto mdogo hadi kuwa mkubwa na kuwa Rais wa nchi.

Baba wa Mageuzi

“Hivi punde tumesikia muhtasari wa kitabu cha Mwinyi lakini mimi pia nimekisoma, kimeshehemi mambo mengi… Kwa yeyote atakayekisoma atajifunza mambo mengi sana. Binafsi nimepata mengi ya kujifunza kama kiongozi kubwa kuliko yote. Ni kwamba Mwinyi ni Baba wa Mageuzi nchini,” alisema.

Alisema Mzee Mwinyi ndiye alisimamia mageuzi makubwa ya kiuchumi akisema: Na bahati nzuri ameeleza kwamba wakati anaingia madarakani, hali ya uchumi ilikuwa mbaya kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo kupanda kwa mafuta, ukame, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuibuka vita ya Uganda na masharti magumu kutoka kwa wafadhili na taasisi za kifedha mwaka 1980.

Alisema baada ya Mwinyi kuingia madarakani alianzisha mageuzi makubwa ya kiuchumi hususani kwa kuanzisha sekta binafsi kushirikiana na serikali kushirki shughuli za kiuchumi.

Samia aliendelea kumwelezea Mwinyi alivyoanzisha ubinafsishaji wa mashirika ya umma ambayo mengi yalianzishwa kwa hasara na kubebesha serikali hasara miongoni mwake ikiwa ni Kiwanda cha Bia Tanzania. Mageuzi mengine ni katika sekta ya fedha na bima na yale ya kusimamia mageuzi ya kisiasa kwa kurudisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1994. “Ni sahihi kusema Mzee Mwinyi ni Baba wa Mageuzi nchini.”

Mafunzo ya kitabu

Rais Samia alisema mbali na kusimamia mageuzi, kitabu kinatufundisha mambo mengine mengi hususani kwa viongozi.” Kwanza, ametufundisha uongozi wa nchi hautafutwi bali unatoka kwa Mungu,” alisema akirejelea muhtasari wa maisha yake unaoeleza kuwa Mzee Mwinyi alizaliwa Mkuranga na kisha akapelekwa Zanzibar kuwa Shehe mkubwa.

Alieleza zaidi kuwa Mzee Mwinyi hakuwa muasisi wa ASP na wala hakushiriki Mapinduzi ya Zanzibar na nafasi pekee aliyoshika ilikuwa ni ukatibu wa ASP kwenye tawi. Alisema kwa kudra ya Mungu alikuwa Rais wa Zanzibar na Muungano bila kuhonga mtu yeyote jambo alilosisitiza kuwa ni fundisho kubwa kwa wenye dhamira ya kutaka kuongoza kwamba uongozi wowote ni kwa Kudra za Mwenyezi Mungu.

Funzo lingine ambalo Rais Samia amelitaja kutokana na kitabu hicho ni kwamba uongozi ni dhamana akirejelea uamuzi wa Mzee Mwinyi kujiuzulu kutokana na mauaji ya vikongwe. “Kitabu kinafundisha uongozi si lele mama. Utakumbana na changamopto mbalimbali,” alisema na kukumbushia changamoto alizokumbana nazo Mwinyi ikiwamo kuibuka kwa Ukimwi, migogoro ya kidini, kundi la G55, migomo ya wanafunzi na kuongeza kuwa uvumilivu na ustahimilivu ndiyo silaha pekee iliyomsaidia.

Funzo la nne alilokutana nalo ni umuhimu wa kukiri makosa. Samia alisema viongozi si malaika ni binadamu huku akipongeza kitendo cha Mwinyi kukiri baadhi ya makosa yaliyofanyika katika kipindi chake wakati wa kufanya mageuzi ya kiuchumi na hasa baada ya misamaha ya kodi kutumika vibaya na baadhi ya wajanja.

Rais alitaja funzo la tano ni la viongozi kupendana na kushirikiana kwa kutoa mfano wa Mzee Mwinyi kuondolewa kwenye nyumba ya serikali Oyster Bay jijini Dar es Salaam kwa vitimbwi lakini baadaye, alipopata urais wa Muungano, akamteua waziri huyo katika Baraza lake la Mawaziri.

Alisema alikuwa na vifaa vya ujenzi vilivyokuwa kwenye nyumba hiyo na waziri aliyechukua madaraka alimwondoa kwa nguvu na akashindwa kuvichukua lakini alipokuja kuwa Rais alimteua kuwa kati ya mawaziri wake.

“Waziri mpya alikuja akamtaka aondoke haraka .Alikubali kuondoka na kuacha vifaa vyake…Pamoja na kufanyiwa vitimbwi hivyo vyote, alimteua waziri kwenye Baraza la Mawaziri. Kama huyo waziri bado anaishi, sijui anajisikiaje huko aliko. Sina hakika wangapi kati yetu tungefanya aliyofanya Mzee Mwinyi,” alisema Rais Samia.

Akimwelezea zaidi Mwinyi ambaye ndiye Mtanzania pekee aliyeshika urais Zanzibar na Muungano kwa nyakati tofauti, Samia alisema, “Tunapata fundisho jingine kwamba sisi binadamu hatuna budi kupendana, kuheshimiana unayemfanyia vitimbi leo hujui kesho utamkuta akiwa nani. Ametufunza pia kutokuishi na visasi mioyoni mwetu.”

Rais Samia amewataka viongozi kuiga utendaji kazi wa Mzee Mwinyi kwa kuwa alikuwa mwenye hekima kubwa katika kuwahudumia wananchi na mwenye subira na maadili mazuri.

Aliwataka wananchi kukinunua kitabu hicho kwa kuwa kinaelezea mengi mbali na mafundisho ya kisiasa, pia kuna mambo ya kijamii na kiuchumi na historia..

Alisema kati ya mambo aliyojifunza katika suala la kuitikia mwito wa kazi ya Mungu ni pamoja na kusoma historia ya Mzee Mwinyi kuwa wakati akiwa na miaka minne alipelekwa Zanzibar ili kuja kusomea elimu ya dini awe Shehe mkubwa nchini lakini akaja kuishia kuwa mtumishi wa umma na Rais wa Zanzibar na Tanzania.

Pia alimwelezea Rais Mwinyi kama mtu mwenye bahati ya kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania Bara huku akimwombea kwa Mwenyezi Mungu ambariki aendelee kuishi kufikia zaidi ya miaka 100. Sasa ana umri wa miaka 96.

Wakati huo huo Serikali imemkabidhi zawadi ya gari jipya aina ya Mercedes Benzi imsaidie kwenye shughuli zake mbalimbali.Kwa mujibu wa Rais Samia, uzinduzi huo wa kitabu ulipangwa ufanywe Machi mwaka huu na Rais John Magufuli.

Chanzo: Habari leo
 
Tunaomba hivi vitabu vya historia za Viongozi wetu haswa Marais wastaafu viwe vinasambazwa bure Mashuleni ili wanafunzi wajifunze.

Namaanisha vitolewe buree mashuleni ili vizazi vyetu vijifunze kuhusu historia za Marais wastaafu.
 
Taarifa hii ni nzuri ila bado inakosa mambo kadhaa ya msingi sana hasa kwa ''wadau wa vitabu'' wanaotaka kuhudhuria tukio hili muhimu la uzinduzi.

Haisemi muda ambao tukio hili litaanza/litafanyika.

Haisemi kama ni aina gani ya wahusika wanaotarajiwa kuwapo.
Yaani itakua ni ''nyote mnakaribishwa'' au ni ''ndugu wageni waalikwa msikose''

Na kwa bahati mbaya ''wahusika'' niliojaribu kuwauliza hawajatoa majibu yoyote juu ya hilo.

Pengine kama kuna mdau analijua hili basi anaweza kutusaidia ''sisi'' jamii ya wadau wa vitabu.

Vinginevyo, pengine tusubiri subra ivute heri.
 
Magufuli amekufa bila kuweka legacy ya chochote. Na kitabu chake hata kama kingeandikwa kingekuwa hakisomeki kutokana na ukatili uliomo
 
Magufuli amekufa bila kuweka legacy ya chochote. Na kitabu chake hata kama kingeandikwa kingekuwa hakisomeki kutokana na ukatili uliomo
Kobe bryant,michael jackson,tupac n.k wamekufa ktab hawjaacha je legacy wmeacha hwjaacha?acha ujuaji,unaonekana mkubwa akili huna..MUACHENI MAREHEMU APUMZIKE,ukiona huwezi kumuacha marehem apumzke basi waseme vibaya ndgu zako waliofariki..FUC*K YOU LAME AS*S NIGGA
 
Mkundu wa maza yako
 
Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anategewa kuwa mgeni rasmi siku ya uzinduzi wa kitabu Cha maisha ya rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi al maaruf Mzee Rukhsa.

========

Rais wa Tanzania Samia Suluhu anatarajia kuwa Mgeni rasmi kesho May 08, 2021 kwenye Sherehe za uzinduzi wa kitabu cha simulizi ya maisha ya Rais wa Pili wa Tanzania Dkt. Ali Hassan Mwinyi kiitwacho “Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu”, uzinduzi utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Nyerere, Dar es salaam.

Kitabu hiki kimechapishwa kupitia mradi wa kuhifadhi kumbukumbu za Viongozi Wastaafu Tanzania na Afrika unaoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI, wengine watakaohudhuria ni Rais Mstaafu Dr.Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu Dkt. Shein n.k
Mkapa alitoa kitabu akaukata! Mengi nae akatoa kitabu akaaga dunia!!

Mungu pitisha mbali...
 
Mkundu wa maza yako
Kobe bryant,michael jackson,tupac n.k wamekufa ktab hawjaacha je legacy wmeacha hwjaacha?acha ujuaji,unaonekana mkubwa akili huna..MUACHENI MAREHEMU APUMZIKE,ukiona huwezi kumuacha marehem apumzke basi waseme vibaya ndgu zako waliofariki..FUC*K YOU LAME AS*S NIGGA
Unapoona watu wanatukanana usilaumu sana. Sometimes kila mtu anapitia matatizo yake nje ya jf ambayo yanampa frastresheni kali sana...

Wakuu mimi siwalaumu nawapo pole ila nawashauri mjitahiti ku control mihemko yenu.

Maisha mafupi haya hamna haja ya kutukanana..

Peace!
 
Huyu jamaa anataka kuleta usela mavi. Ndo maana anajiita ''Bad Man". Fala tu huyu. Mimi ni Gangsta kuliko yeye
 
Rais wa awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi leo anazindua kitabu kinachohusu maisha yake.

Mgeni rasmi ni Rais wa JMT mh Samia

Tukio litakuwa mubashara kupitia runinga ya Channel ten.

Nitawajuza yanayojiri.

Wahenga karibuni tujikumbushe maisha wakati wa mzee Rukhsa.

Updates;

Mzee Mwimyi ameshaingia ukumbimi na tayari ukumbi umeshasheheni wageni waalikwa mbalimbali.

Sasa anasubiriwa mgeni rasmi Rais Samia.

Rais Samia ameingia ukumbini na sasa wanaimba wiimbo wa taifa.

Ukumbi mzima ni full barakoa.
 
hivi unaweza kupoteza muda wako kabisa unasoma kitabu cha huyu mzee??unapata faida gani humo ndani?kwa background ip?kwa legacy ipi?
kuna mwingine alikuwa anaitwa mkapa naye alitoa kitabu nasikia,mtanzania yupi??
 
Watoto wa miaka ya 2000 mnajulikana tu. Sikiliza nikwambie kijana.. usione maduka kibao k'koo, shule nzuri za serikali na binafsi, mitumba ya kumwaga tandale, manzese, k'koo na sehem mbali mbali za nchi, zahanati na hospital za serikali na binafsi, mchele mzuri wa kunukia, unga safi wa ugali na ngano ukafikiri labda vimeletwa na Kikwete au Magufuli. Hizo ni juhudi za huyo unaemkandia, pengine bila upendo wake kwa wananchi wake leo hii ungekuwa unavaa magunia. Hata hiyo sim unayotumia kuandikia pumba pengine leo usingekuwa nayo. Usione vyaelea vimeundwa kaka
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom