Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,990
2,000
Jana Rais Samia kwenye uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Mwinyi, alitangaza kuwa katika pia kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais wetu huyo wa zamani aliyetimiza miaka 96, serikali imempatia gari [jipya?] aina ya Mercedes Benz iliyo chini [sedan] kwa sababu aliyokuwa akiitumia [nadhani ni SUV] ilikuwa inampa shida kuipanda na kushuka kutokana na umri wake mkubwa kwa sasa pamoja na kimo chake [hapa nahisi Rais Samia alisema kwa utani].

Tangazo hilo la Rais Samia limezua sokomoko kubwa, hususan mitandaoni.

Mimi sina tatizo na ‘zawadi’ hiyo kwa Rais wetu huyo mstaafu. Kwa maelezo machache aliyoyatoa Rais, sina pingamizi lolote lile.

Ila kuna wengine hawakufurahishwa na jambo hilo. Wamehoji kwamba iweje mtu kama Rais Mwinyi, ambaye katumikia taifa kwa muda mrefu na katika nafasi za juu kabisa, mtu mwenye istihaki nyingi hivyo, ashindwe kujinunulia gari linalomfaa kwa matumizi yake.

Rais Mwinyi keshawahi kuwa waziri. Keshawahi kuwa Rais wa Zanzibar. Na alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Sina hakika kama pia huwa anapata marupurupu ya utumishi wake kama Rais wa Zanzibar au la. Naamini ya urais wa Jamhuri ya Muungano anayapata.

Sasa mimi nina maswali kadhaa:

1. Je, hilo gari alilopewa hivi sasa ni la kwake? Limesajiriwa kwa jina lake? Yeye ndo analilipia bima?
Mimi muda wote huu nimekuwa nikidhani kuwa marais wastaafu huwa wanapewa gari ya matumizi na serikali na kwamba magari hayo huwa ni mali ya serikali.
Yaani, Rais mstaafu huwa anapewa gari, ofisi, watumishi wa ofisi, walinzi, na kadhalika.

2. Kama hivyo ni ndivyo, ni kapewa au wamembadilishia tu gari ya matumizi na siku atayoacha kuitumia itarudishwa ilikotoka?

3. Kama wamembadilishia tu gari, Rais angesema ‘tumembadilishia’ gari la matumizi kuliko kusema ‘tumempa’ gari jipya kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa, ingekuwa ni bora zaidi na isingezua sokomoko?

Tatizo nilionalo hapa ni kuhusu timing, optics, na word choice tu.

Zaidi ya hapo kelele zilizopigwa sizioni kama ni hoja zilizo compelling.

Rais Mwinyi siyo raia wa kawaida. Hawezi kulinganishwa na wazee wengine ambao hawajawahi kuwa marais.

Rais Samia kusema ile majuzi kuwa serikali haina hela za kutosha kuwapa posho wazee, hiyo haina maana serikali haina hela za kuwatunza marais wa zamani.

So this is much ado about nothing.

Go ahead and click that ‘Thanks’ button if you agree with me. Even if you don’t agree but you appreciate the content, go ahead and smash that button.

Happy Sunday and most importantly, have a very happy Mother’s Day!
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,967
2,000
Unajua Mzee Mwinyi alikuwa champion besti besti, tena waziwazi wa JPM. Sasa Bi Mkubwa atamchumbiaje basi!? Ndiyo maana ya zawadi hiyo mujarabu. Umenipata!? Hiyo ni namna moja ya Bi Mkubwa kumwambia: Achana na zilee kauli zako on behalf of Bulldozer. Rudi huku maana ndiyo direction kwa sasa!
 

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
171
500
Kwanza serikali inahaizna ya magari kama yale mengi, wamechagua tu moja wamempa wala hajanunuliwa.

Halafu gari walilompa sio hisani sababu ya uzuri wake au urefu au uzee wake, kama hivyo basi kuna wazee wengi na kuna watu wafupi wengi, ila kapewa sababu alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano na gari anayotumia inampa shida.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,990
2,000
Unajua Mzee Mwinyi alikuwa champion besti besti, tena waziwazi wa JPM. Sasa Bi Mkubwa atamchumbiaje basi!? Ndiyo maana ya zawadi hiyo mujarabu. Umenipata!? Hiyo ni namna moja ya Bi Mkubwa kumwambia: ^Achana na zilee kauli zako on behalf of Bulldozer. Rudi huku maana ndiyo direction kwa sasa!^
Kwani hilo Benzi ni zawadi ya Samia kwa Mwinyi?
 

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
15,808
2,000
It's a PR Disaster.
Pure and simple.
Wiki ile, hakuna hela ya kuongeza kwa wafanyakazi kwani serikali haina hela.
Wiki hii , Mzee Ruksa anapewa zawadi ya birthday ambayo anaweza kununuliwa na watoto wake ambao wengine ni Marais.

Mbaya zaidi unalifocus tukio lenyewe kwa kuahirisha mechi pendwa sana.

Tunaomtetea mama mtandaoni hatumwelewi.
 

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,410
2,000
Mbona hukuhoji pale Mwendazake alivyonunua jogoo kwa laki moja? Mbona hukuhoji source ya hela ambazo Mwendazake alikuwa anatapanya hovyo kwa kuwazawadia watu mikutanoni?

Vitu kama si vyote alivyofanya Mwendazake Kama hivi hukutia neno na ulipotaka kusema ulileta ki complicated English ili ku blur intention 😃😃

Mtulie, rais Samia ametoa kwa niaba yetu zawadi kwa rais mstaafu. Ulitaka akodishiwe gari na serikali aliyoitumikia kwa 10 years kama kiongozi mkuu.

MATAGA kubalini bhasi
 

msabillah

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,337
2,000
Unajua Mzee Mwinyi alikuwa champion besti besti, tena waziwazi wa JPM. Sasa Bi Mkubwa atamchumbiaje basi!??? Ndiyo maana ya zawadi hiyo mujarabu. Umenipata!??? Hiyo ni namna moja ya Bi Mkubwa kumwambia: ^Achana na zilee kauli zako on behalf of Bulldozer. Rudi huku maana ndiyo direction kwa sasa!^
Unaona mbali sana mzee
 

msabillah

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,337
2,000
Kwanza serikali inahaizna ya magari kama yale mengi, wamechagua tu moja wamempa wala hajanunuliwa.

Halafu gari walilompa sio hisan sabab ya uzuri wake au urefu au uzee wake, kama hivo basi kuna wazee wengi na kuna watu wafupi wengi , ila kapewa sabab alikuwa ni raisi wa jamhuri ya muungano na gari anayotumia inampashida.
Kikwete naye apewe au kwakuwa yeye ni wa bara!
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,990
2,000
Mbona hukuhoji pale Mwendazake alivyonunua jogoo kwa laki moja? Mbona hukuhoji source ya hela ambazo Mwendazake alikuwa anatapanya hovyo kwa kuwazawadia watu mikutanoni?

Vitu kama si vyote alivyofanya Mwendazake Kama hivi hukutia neno na ulipotaka kusema ulileta ki complicated English ili ku blur intention 😃😃

Mtulie, rais Samia ametoa kwa niaba yetu zawadi kwa rais mstaafu. Ulitaka akodishiwe gari na serikali aliyoitumikia kwa 10 years kama kiongozi mkuu.

MATAGA kubalini bhasi
Ndo maana sasa naamini hata nyumbu anawazidi akili!

Mimi sikuhoji hela alizokuwa anagawa Rais Magufuli?

Huyu alieandika hivi ni nani?

467EDB1A-662D-4DED-8C22-22F5A4566AC8.png
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,389
2,000
Sina tatizo na Mzee Mwinyi kupewa gari. Mzee Mwinyi anastahili kupewa gari ya kutembelea na serikali wakati wote. Siyo hisani wala haiwezi kuwa zawadi. Ni stahili yake.

Ila nina tatizo na Mzee Mwinyi kupewa gari kama zawadi. Ingekuwa ni vyema angetafutiwa kitu kingine kama zawadi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom