Ni matumaini yangu Waziri Kabudi utakuwa umejifunza jinsi ya kutoa Hotuba fupi na yenye Mambo yote Muhimu kama aliyoitoa Rais Mwinyi wa Zanzibar

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,367
2,000
Kwa ninavyokujua Mzee wangu Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi ungepewa Wewe nafasi ya Kuzungumza Zanzibar leo usingetumia dakika 15 tu alizotumia Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi.

Hongera sana Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa Hotuba yako nzuri, fupi, yenye Mambo Muhimu yote pamoja na Msisitizo isiyochosha ambayo imechukua dakika 15 tu ukamaliza.

Natamani mno Profesa Kabudi aje akuone ili uweze Kumfundisha kutoa Hotuba fupi, zisizoboa na zenye mambo irrelevant sana kwa Maisha yetu ya sasa na nyakati hizi tulizopo ambapo kila Mtu anakimbizana na muda huku mambo nayo yakiwa ni mengi.
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,192
2,000
Rais Hussein Mwinyi ni chuma cha pua kile. Msomi mwenye akili na busara. Ana akili, anajua kujiratibu. Yuko focussed. Hana makundi na huyu angetufaa sana Jamhuri ya Muungano baada ya mama Samia. Atakuja kusafisha mioyo iliyopondeka na kuiendeleza Tanzania ya Amani tena baada ya mama yetu kumalizia muda wake.

Mimi sina uvyama maana sina chama ila ninahitaji Rais wa kutuponya Tanzania kwenye baadhi ya maeneo. Yaani tupone tunyanyanyuke na utanzania wetu usiyokuwa tena na:

1. Ukanda na Ukabila.

2. Kesi na manyanyaso.

3. Kuheshimu sheria na taratibu.

4. Kuongoza na Katiba iliyoboreshwa.

5. Kuheshimu Demokrasia ya vysma vingi maana vipo kisheria.

6. Watu wasipotee tena na wasipatikane milele.

7. Kutoadhibu watu kwa fitina na wivu ikisindikizwa na kesi za hukumu uchumi na utakatishaji pesa zenye mashaka.

8. Yako mengi ya kurekebisha na kuponya mioyo ya familia zilizoguswa na mambo mengi mno ya utata.

Nikihakikishieni Mh. Mwinyi ameshaanza kuiponya Zanzibar na ndani ya miaka mitano tutajionea wenyewe huko Zanzibar.

Mama Yetu Mh. Rais Samia Suluhu ninaona kabisa utatuvusha na tunyanyuke tena kwenye baadhi ya maeneo. Hotuba yako ya kuapishwa ilitupa matumaini sana. Mungu akupe nguvu ya kututumikia.
 

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,367
2,000
Hotuba ya Mh. Kabudi jana iliambatana pia na wasifu wa marehemu.

Hivi kutafuta kasoro kwa kila jambo kumbe nao ni ugonjwa?

Pumbavu sijaanza Kumfuatilia Waziri Profesa Kabudi leo na sasa kwa Kukusaidia pia ni Rafiki mkubwa sana wa Baba yangu Mzazi na hizo Kasoro zake za Mistori mingi isiyo na Kichwa wala Miguu hata akija Kumsalimia Baba ( Mzee ) bado huwa ninaziona. Sema lingine tena sasa Mpuuzi Wewe.
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,153
2,000
Mkuu kwa chuki hizi umepitiliza kiwango cha chuki za kawaida cha binadamu. huenda unaumwa ila wewe hujui, tafuta wataalam wa magonjwa ya kisaikolojia ukatibiwe!
Wagonjwa wa aina hii huwa hawajijui! Solution ni kukamata na kufunga mikono na miguu na kusukumiza psychiatric ward😂!
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,153
2,000
Mkuu kwa chuki hizi umepitiliza kiwango cha chuki za kawaida cha binadamu. huenda unaumwa ila wewe hujui, tafuta wataalam wa magonjwa ya kisaikolojia ukatibiwe!
Wagonjwa wa aina hii huwa hawajijui! Solution ni kukamata na kufunga mikono na miguu na kusukumiza psychiatric ward😂!
 

Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
4,893
2,000
Pumbavu sijaanza Kumfuatilia Waziri Profesa Kabudi leo na sasa kwa Kukusaidia pia ni Rafiki mkubwa sana wa Baba yangu Mzazi na hizo Kasoro zake za Mistori mingi isiyo na Kichwa wala Miguu hata akija Kumsalimia Baba ( Mzee ) bado huwa ninaziona. Sema lingine tena sasa Mpuuzi Wewe.
Utoto unakusumbua!
Yaani rafiki ya baba yako ndiyo unaingia jukwaani kumsemea vibaya?
Nonsense!
 

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,367
2,000
Utoto unakusumbua!
Yaani rafiki ya baba yako ndiyo unaingia jukwaani kumsemea vibaya?
Nonsense!
Ulitaka nimseme nikiwa Nakupakuwa Chumbani Kwangu au? Wewe ni nani wa Kunipangia Mimi cha Kuandika na Kuchangia hapa JF? Idiot!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom