NDAGU, KITALA NA ADHABU YA MCHAWI
NDAGU maana yake ni ‘ramli'. Kwa desturi, baada ya kuondoa matanga, ndugu waliofiwa huenda kwa mganga wa ramli ili awajulishe sababu ya kifo kilichotokea. Ziko namna nyingi za ndagu, kwa mfano, ndagu ya kifo, ndagu ya ugonjwa, yaani ramli ya kubashiri maradhi...