Ni baada ya kuwekwa kwenye kila bajeti toka mwaka 2013/2014 hadi mwaka 2016/2017 pasipo mafanikio. Nina imani sasa hii barabara siyo kwamba itaegeshwa tena kama miaka mingine iliyopita. Ni barabara mbovu sana inayofanya magari kupelekwa gereji mara kwa mara. Naomba kama kuna mtu amehusika...
Story ya mbuzi wa dar kuzurula na kuvuka wenyewe kwenye zebra imeandaliwa na bbc na kurushwa na bbc asubuhi ya leo tarehe 13/04/2017. Lakini kwenye amplifaya ya clouds na huyu dada plus milard ayo wanatoa hii habari na kudanganya kuwa kuna ripota wao ndo kaandaa hii habari wakati ni yule wa bbc...
Naomba wahusika wanisaidie. Ni sababu zipi zinazosababisha mabasi ya mwendo kasi kutokulala kwenye vituo pale yanapotakiwa kuanzia safari? Watu wanasubiria magari kimara mwisho alafu yanakuja yamejaa tayari. Hapa sijaelewa kwanini kulala Jangwani na si Kimara??
Naomba wahusika wanisaidie,
Ni sababu zipi zinazosababisha mabasi ya mwendokasi kutokulala kwenye vituo pale yanapotakiwa kuanzia safari? Watu wanasubiria magari Kimara Mwisho alafu yanakuja yamejaa tayari.
Hapa sijaelewa kwanini kulala Jangwani na si Kimara.
Naomba kama kuna mtu ana access plan ya hii barabara anisaidie. Je hii barabara itakayojengwa kuanzia pugu kwenda bunju kupitia mbezi mwisho itapita barabara zipi kati ya hizi mbili?? Ile iliyopo pale kwa Yusuph kupitia mbezi high school au ile inayokwenda na ile iendayo goba ikachepuka pale...
Barabara ya morogoro ni kiungo muhimu sana kwa magari yanayotoka na kuingia katika jiji la dar es salaam. Lakini hii imekuwa ni barabara yenye foleni kubwa hasa eneo la kibamba mpaka kimara. Hili ni eneo sugu ambalo linahitaji upanuzi wa barabara na si kupanua tu njia ya miinuko. Barabara hii...
Nimesoma gazeti la habari leo la leo tarehe 16/11/2016 mkurugenzi wa bodi ya mikopo anasema kuna watu wa kozi za vipaumbele wamenyimwa mikopo kwa sababu wazazi wao wana uwezo.
Je wamepita kwa wazazi wao kuthibitisha hili wanalolisema au kigezo cha uwezo wa mzazi ni mtoto wake kusoma o level...
Nimenukuu maneno yaliyopo kwenye bageti ya wizara ya ujenzi ya mwaka 2015/2016 iliyoandaliwa na rais wa sasa ambaye alikuwa waziri wa ujenzi.
Naomba kujua mambo yafuatayo:
1. Alimaanisha nini aliposema barabara ya Pete?
2. Kwa wenyeji wa Dar es Salaam na wanaoijua vizuri ramani ya Dar naomba...
Hii barabara kwa kweli ni kero mpaka basi. Mvua ikinyesha ndo usiseme, daladala wanashindwa kwenda mpigi magohe kisa utelezi, na hii inasababisha nauli kupanda mpaka elfu 1 na mia 5 kutoka shilingi mia 5. Kwa kuwa hii barabara iko chini ya tanroad, basi tunaomba serikali iiweke kwenye budget...
Najiuliza hata sipati jibu. Ni nani aliplan barabara ya mwendo kasi iishie kimara mwisho na si mbezi mwisho? Hapo ndo nakosa jibu kabisa. Hii barabara ya morogoro ni barabara pekee inayopeleka magari mengi sana ikiwemo mabasi, maroli, na magari ya watu binafsi yanayoenda na kutoka mikoani na...
Hivi serikali kuwanyima mkopo mwaka wa kwanza madaktari watarajiwa ambao wanagusa moja kwa moja maisha ya wananchi ina maana gani? Haiwezekani serikali itumie kigezo cha o level kuwanyima hawa vijana mikopo.
Kijana kusoma o level private haina maana kuwa huyo mzazi ni tajiri. Maisha yanapanda...
Naomba msaada wa kujua juu ya barabara inayoanzia mbezi mwisho kwa yusufu kupita mbezi high school mpaka mpigi magoe mpaka bunju.
Hivi hii barabara serikali kweli ina mpango nayo kuijenga kiwango cha lami?
Kwa maana mimi naiona hii barabara kwamba ni msaada mkubwa kwa watu wa Mbezi, kibamba...
Mimi najua mfanyakazi ambaye ameajiriwa na serikali hasa katika ngazi ya halmashauri masaa ya kufanya kazi ni manane. Lakini katika kada ya uuguzi na kada nyingine ambazo zina night shift siyo rahisi kufanya masaa manane tu hasa kwa usiku. Nahitaji kujikita kwenye kada ya uuguzi, na ninaomba...
Naomba msaada kuhusu kutambaa kwa mtoto. Mtoto wangu ni wa kike ana miezi tisa lakini bado anajivuta kwa tumbo. Sasa hivi ndo naona anashika kwenye kiti au meza anasimama mwenyewe. Je ni muda gani sahihi kwa mtoto awe ameshaanza kutembea?
Wapendwa naomba kujua habari za Saida Karoli. Kwa sasa yuko wapi na kama bado anajihusisa na muziki?
Naombeni pia mwenye namba yake anipm kwa maana mbali na kujua hayo nayouliza hapo juu nilipenda nifanye nae biashara. Naomba msaada wenu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.