Omukitwe
Member
- Mar 29, 2016
- 91
- 91
Barabara ya morogoro ni kiungo muhimu sana kwa magari yanayotoka na kuingia katika jiji la dar es salaam. Lakini hii imekuwa ni barabara yenye foleni kubwa hasa eneo la kibamba mpaka kimara. Hili ni eneo sugu ambalo linahitaji upanuzi wa barabara na si kupanua tu njia ya miinuko. Barabara hii ili angalau kupunguza foleni inatakiwa ijengwe japo njia nne kitoka kibamba mpaka kimara, mbili kwenda na mbili kurudi. Hii itasaidia japo kupunguza foleni ya magari yanayoingia na kutoka dar es salaam na pia itasaidia kupunguza msongamano unaowakuta wakazi wa dar waishio maeneo ya kibamba na mbezi kwa ujumla. Kwa sasa hali ni mbaya sana, na inapelekea watu kutumia muda mrefu kusafiri kutoka mbezi mpaka kimara kwa takribani masaa mawili ambapo inabidi zisizidi hata dakika 15. Hii inaua uchumi wa raia na uchumi wa taifa kwa ujumla. Hivyo basi, mm nashauri serikali iweke nguvu sana kwenye bajeti yake ijayo na kuitengeneza hii barabara kwa njia nne badala ya kufikiria kuipanua tu sehemu za miinuko.