Omukitwe
Member
- Mar 29, 2016
- 91
- 91
Najiuliza hata sipati jibu. Ni nani aliplan barabara ya mwendo kasi iishie kimara mwisho na si mbezi mwisho? Hapo ndo nakosa jibu kabisa. Hii barabara ya morogoro ni barabara pekee inayopeleka magari mengi sana ikiwemo mabasi, maroli, na magari ya watu binafsi yanayoenda na kutoka mikoani na nchi jirani. Lakini ebu fuatilia shida iliyopo kuanzia kimara mwisho mpaka mbezi mwisho. Mtu unaweza kutumia zaidi ya saa moja kutoka mbezi kwenda kimara. Hapa najiuliza, hivi serikali haioni umuhimu wa kupanua hii barabara angalau kuwa njia nne?? Ninaomba kuuliza kama kuna yeyoye ana taarifa za kuwekwa kwenye mpango wowote wa serikali kwa kuondoa hii kero anajuze.