Omukitwe
Member
- Mar 29, 2016
- 91
- 91
Ni baada ya kuwekwa kwenye kila bajeti toka mwaka 2013/2014 hadi mwaka 2016/2017 pasipo mafanikio. Nina imani sasa hii barabara siyo kwamba itaegeshwa tena kama miaka mingine iliyopita. Ni barabara mbovu sana inayofanya magari kupelekwa gereji mara kwa mara. Naomba kama kuna mtu amehusika kupanga bajeti ya TANROAD mwaka ujao atueleze kama hii ni moja ya barabara zilizokumbukwa au tutaendelea kupiga mashimo na itaendelea kuwekwa kwenye bajeti kwa kuegeshwa?? Sasa hivi ukiangalia pale mbezi high school ndo barabara imeharibika haswa. Pia kutoka machimbo mpaka mpigi magoe hapatamaniki kabisa kabisa. Hali ni mbaya kweli kweli kwenye hii barabara.