Search results

  1. Mwitongo

    JWTZ wazindua 'Operesheni Tokomeza'

    Jeshi la Wananchi wa Tanzania limezindua Operesheni Tokomeza inayolenga kuwamaliza majangili katika mapori ya akiba, mapori tengefu na hifadhi za taifa. Katika Operesheni hiyo, tayari Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makuyuni, Monduli mkoani Arusha, Bakari Salim (Mpemba) amekamatwa akiwa na kilo 40 za...
  2. Mwitongo

    Rushwa Trafiki Kibamba Hospotali inatisha!!

    Ndugu zangu, trafiki kutoka Kituo cha Kwa Yusuf, na wakati mwingine Kibaha, kila siku yanapotoka maji hapa Kibamba Hospitali. Maji hutoka Jumapili na JUmatano. Hivi leo ni Jumatano,kuanzia sasa hivi wapo hapa wamejaa tele. Kila gari la maji wanachukua Sh 2,000. Kwa siku mapato yao yanazidi Sh...
  3. Mwitongo

    JAMHURI yataja matajiri matapeli Tanzania

    Gazeti la Jamhuri leo limekuja na orodha ya majina ya matajiri matapeli wa madini Tanzania. Wamo kina Rashid Ntimizi (mtoto wa waziri wa zamami), familia ya Aurora, Roger David Mawelle, Tambwe Moses, Papa Msofe, John ChizumoNaftari Njoree (Mmasai), David Kazibwe na wengine wengi. Wanatapeli...
  4. Mwitongo

    Nyerere alivyoomba kuhusu Omba-Omba

    CHANZO: Gazeti Jamhuri Mwalimu Nyerere alijua ujio wa Obama tangu mwaka 1967 Mwaka huu pekee, Tanzania imepokea marais wa mataifa mawili makubwa yanayoongoza kwa uchumi imara duniani. Rais Xi Jinping wa China alikuwa wa kwanza, na baadaye amefuatiwa na Rais Barack Obama wa Marekani...
  5. Mwitongo

    Ufisadi wa kutisha ujio marais/Obama: Zaidi ya Bilioni 8 zatumika!

    Ufisadi ujio wa marais *Hazina yatumia Shilingi bilioni 8 *‘Wajanja’ watafuna mamilioni *Vifaa vya Obama vyaokoa jahazi *Vinyago vyagharimu Sh milioni 30 *Sare, mikoba, vyagharimu mil. 400/- *Karamu, chupa za kahawa, miavuli mil. 390/- *Burudani ya muziki yatafuna milioni 195 Na Waandishi Wetu...
  6. Mwitongo

    Vitalu vya uwindaji: Kagasheki ashitakiwa Mahakama Kuu

    Wadau, hii habari ilishawekwa mtandaoni na katika magazeti. Naileta kwenu baada ya kupata taarifa kwamba leo kampuni 4 zimefungua kesi kutaka kutengua uamuzi wa Serikali wa kugawa vitalu. Kesi imefunguliwa Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Imeahirishwa hadi kesho Jumanne. Kagasheki atiwa...
  7. Mwitongo

    Ufisadi: Viongozi wote Serikali ya Kijiji cha Butiama wafukuzwa

    Nipo hapa Butiama, uongozi wote wa Kijiji chini ya Mwenyekiti Zacharia Wambura (Debe Tupu), umefukuzwa. Waliofanya kazi hiyo ni wananchi wenyewe baada ya ufisadfi kuvuka kiwango. Source: Mimi mwenyewe
  8. Mwitongo

    Picha: Ofisi ya CCM, sioni kupona!!!

    Waungwana, hii ni Ofisi ya Chama Tawala (CCM) Tawi la Chamakweza, Chalinze! Kila nikitazama hali ya chama hiki naona kinaelekea kaburini tu! Tehe tehe tehe!
  9. Mwitongo

    Majina ya uswahilini vs Masaki & Oysterbay

    Nimeishi Mikocheni na Msasani kwa miaka mingi, lakini sikubahatika kumsikia msichana akiitwa Chausiku au Havijawa. Sana sana niliwajua kina Karen, jacquline, Linah, nk. Kwanini kuwepo tofauti kubwa ya majina kwa wasichana wa uswahili na kwenye mageti makali?:phone:
  10. Mwitongo

    Misaada mingine ya Marekani ni fedheha!

    Chanzo: Wavuti ya Gazeti JAMHURI Misaada mingine ya Marekani ni fedheha Na Manyerere Jackton Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alizungumza neno zuri. Sina hakika kama viongozi wetu waliweza kulisikia na kulitafakari kutoka kwenye hotuba ya kiongozi huyo wakati akizindua Chuo Kikuu...
  11. Mwitongo

    Tume ya Utumishi wa Mahakama yamjibu Tundu Lissu

    Ndugu zangu, angalieni utumbo huu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama! Eti majaji wote wamepatikana kwa kufuata taratibu, na wote wana sifa!! Hata yule anayesoma Chuo Kikuu Huria, ambaye kawa jaji kinyume cha Katiba, naye ni safi kabisa!! Nchi hii imepigwa laana?
  12. Mwitongo

    Waziri Mwakyembe aunda Bodi Mpya ya Bandari; avunja bodi ya zamani

    Habari za uhakika kutoka Wizara ya Uchukuzi zinasema kwamba Waziri Mwakyembe amefukuza wajumbe wote wa TPA na kuteua wapya. Source: Wizara ya Uchukuzi
  13. Mwitongo

    Simu za Makamanda wa Polisi Mikoa yote hizi hapa

    Kuwa na namba hizi kunaweza kuwasaidia kuwasiliana na hawa makamanda japo imani yetu kwa Polisi imeshuka sana! NAMBA ZA SIMU ZA MAKAMANDA TANZANIA (RPCs) MKOA JINA LA KAMANDA SIMU Arusha ACP Liberatus Sabas 0713 269 232 Dodoma ACP David Misime 0754 470 959 Manyara ACP Akilimali...
  14. Mwitongo

    Mtikisiko mkubwa CCM

    CHANZO: Gazeti JAMHURI Mtikisiko CCM *Msekwa, Karume kutemwa rasmi, vigogo kuangukia pua *Wasira, Lukuvi, Membe, Makamba, Mukama wapambana *Balozi Seif, Shamsi, Khatib, Mbarawa, Samia, Mwinyi vita kali Na Mwandishi Wetu WIKI hii Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa katika hatua za mwisho za...
  15. Mwitongo

    CRDB wakataa fedha za mteja!

    Ndugu zangu, katika hali isiyo ya kawaida, leo nimeshuhudia tukio la kusikitisha. Nilikuwa katika Benki ya CRDB, Tawi la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam; nimeshuhudia mhudumu wa dirisha namba 2 akikataa kupokea fedha za mteja mmoja kijana. Kisa ni kwamnba kijana huyo alikuwa na fedha nyingi...
  16. Mwitongo

    Picha: Nyerere mdogo!

    Wadau, nimekutana na picha hii ya mtu anayefanana sana na Baba wa Taifa. Wapo wanaosema ni yeye, lakini wengine wanasema ni mdogo wake. Mwenye kumjua atusaidie.
  17. Mwitongo

    Picha: Dawasco imekufa? Siku tatu maji mengi yanamwagika

    Leo ni siku ya tatu DAWASCO wakiwa hawajafika kuziba bomba hili la maji katika eneo la Luguruni Stendi (Makondeko. Maji yanamwagika usiku na mchana, hakuna hatua zozote za kuziba bomba hili wakati maelfu ya watu Dar wakikosa maji. Hii inaashiria nini? Mdau
  18. Mwitongo

    Kura ya kutokuwa na imani na rais kikwete huu ndiyo wakati wake

    Mod, naomba usibanie uzi huu kwa sababu si uchochezi, bali ni uhalisia unaotokana na Katiba yetu.Nadhani huu ndiyo wakati kwa wabunge kuajiandaa KUPIGA KURA ya kutokuwa na imani na Rais Jakaya Kikwete kwa sababu ameshindwa kuongoza. Haiwezekani vurugu zote hizi nchini ziendelee, si yeye, Makamu...
  19. Mwitongo

    Picha: Huyu ndiye farid wa uamsho

    Sheikh Farid (wa pili kutoka kushoto) ndiye kiongozi wa Uamsho anayeifanya Zanzibar na Tanzania kwa jumla isipate usingizi.
  20. Mwitongo

    Rushwa kibaha maili moja

    Wadau, nchi hii imeoza kabisa. Najiandaa kuandika kitabu chenye picha za upokeaji rushwa unaofanywa na trafiki katika Stendi ya Mabasi Kibaha Maili Moja. Trafiki wanapokea rushwa nje nje kila siku asubuhi. Wanapokea bila aibu. Jamani, nchi hii tunakwenda wapi? Hofu yangu ni kwamba naweza...
Back
Top Bottom