Vitalu vya uwindaji: Kagasheki ashitakiwa Mahakama Kuu

Vitalu vya uwindaji: Kagasheki ashitakiwa Mahakama Kuu

Mwitongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2009
Posts
312
Reaction score
362
Wadau, hii habari ilishawekwa mtandaoni na katika magazeti. Naileta kwenu baada ya kupata taarifa kwamba leo kampuni 4 zimefungua kesi kutaka kutengua uamuzi wa Serikali wa kugawa vitalu. Kesi imefunguliwa Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Imeahirishwa hadi kesho Jumanne.


Kagasheki atiwa majaribuni

*Fedha zachangwa ugawaji vitalu urejewe
*Zitatolewa kwa kisingizio cha uhifadhi
*Mahakama, Ofisi ya AG walengwa wakuu

Na Mwandishi Wetu

Kundi la wafanyabiashara kadhaa wa tasnia ya uwindaji wa kitalii limekutana nchini Marekani na kuendesha mchango wa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhakikisha zinafanikisha ugawaji upya wa vitalu vya uwindaji.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii zimesema fedha hizo zimechangwa kwa kivuli vha kusaidia shughuli za uhifadhi nchini, lakini ukweli wa mambo ni kwamba zimepangwa kutumiwa kuwarubuni baadhi ya viongozi waandamizi wa Wizara hiyo pamoja na vyombo vya dola, hasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mahakama.

Kiasi cha dola za Marekani zaidi ya 600,000 kimekusanywa kuhakikisha mpango huo unafanikiwa wakati wowote kuanzia sasa. Dola moja ya Marekani ni wastani wa Sh 1,600.

Mpango huo unasukwa ilhali Ikulu, na baadaye Wizara ya Maliasili na Utalii mnamo Januari, mwaka jana zikitoa taarifa ya kutorejewa ugawaji vitalu.

Sehemu ya tangazo la Wizara ya Maliasili na Utalii kwa umma, kupitia kwa Msemaji wake, George Matiko, lilisomeka, "Wizara ya Maliasili na Utalii haina mpango wa kurudia ugawaji wa vitalu. Mchakato wa ugawaji ulikamilika mwezi Septemba mwaka jana (2011) na matokeo yake kutangazwa wazi.

Mapema mwezi Septemba 2011, Wizara ilitoa orodha ya kampuni 60 zilizofanikiwa kugawiwa vitalu. Kati ya kampuni hizo, kampuni 51 ni za kizalendo na kampuni 9 za kigeni kwa kuzingatia kifungu 39(3)(b) cha sheria ya wanyamapori Na. 5, ya 2009.

Hata hivyo, kumekuwa na taarifa mbalimbali zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kuwepo kwa harakati zinazofanywa na waombaji waliokosa vitalu zikihusisha kuchafuana baina ya kampuni zilizopata na zilizokosa kwa nia ya kuzorotesha sekta ya uwindaji wa kitalii kwa ujumla. Vyombo hivyo vimeripoti kuwa mchakato wa ugawaji wa vitalu utarudiwa.

Wizara inasisitiza kuwa mchakato wa ugawaji wa vitalu hautarudiwa na watanzania wanahakikishiwa kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali za kuleta mabadiliko kwenye sekta hii tangu mwaka 2008, zimesaidia sana kuimarisha usimamizi wa Sekta hii."

Uchunguzi wa Jamhuri umebaini kuwa mkakati huo umeratibiwa na mmoja wa wadau kwenye tasnia ya uwindaji mwenye ushawishi mkubwa ambaye anaishi mkoani Arusha.

Mdau huyo ambaye anashirikiana na baadhi ya raia wa kigeni, amekuwa akihaha kupata vitalu ambavyo kwenye mgawo halali uliokwishafanyika walipewa Watanzania wazawa.

Tangu wakose vitalu hivyo, mdau huyo ambaye kwa sasa jina lake tunalihifadhi, amethubutu kutumia njia mbalimbali zikiwamo za kuwaghilibu wabunge pamoja na viongozi waandamizi serikalini katika kuhakikisha anapata vitalu hivyo. Moja ya sababu zake ni kwamba kugawanywa kwa vitalu kulikofanywa na wataalamu katika maeneo kadhaa, hasa katika mikoa ya Arusha na Manyara kunaathiri ikolojia.

Kwa kuamini kuwa mpango wake wa kupata vitalu kutoka kwa wazawa wenzake utafanikiwa, hadi sasa kampuni nne alizo na uhusiano nazo wa karibu hazijakabidhiwa barua.

Chanzo cha habari kimedokeza kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, licha ya kutamka mara kwa mara, na hata kutoa taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari kwamba ugawaji vitalu hautarejewa, sasa anaelekea kukubaliana na kundi linaloshinikiza kurejewa upya ugawaji huo.

Imeelezwa kwamba ameshauriwa kuwa ili kutojiweka kwenye utata na mgongano wa kauli, suala la ugawaji upya wa vitalu sasa liamuriwe na Mahakama Kuu. Wiki iliyopita kundi la wafanyabiashara hao lilikuwa, ama likutane na viongozi waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma, au jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka sawa mambo.

"Mikutano ya Dodoma na Dar es Salaam ililenga kuwahakikisha Mahakama inatumiwa kutengua uamuzi wa awali wa ugawaji vitalu. Hawa watu wanajiamini sana. Wakiwa Marekani wakawa wanawatisha watu wasiuze safari wakisema ugawaji vitalu unarudiwa.

"Njia nzuri iliyoonekana ni ya kuitumia Mahakama kubadili uamuzi wa awali. Fedha zilizochangwa zimelenga kutolewa kwa viongozi kadhaa waandamizi ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na pia ikiwezekana zitumike kuweka mambo sawa mahakamani. Haya mambo ni ya siri sana, lakini ukweli ndiyo huo," kimesema chanzo chetu cha habari.

Habari zilizovuja kutoka kwa mmoja wa viongozi wakubwa kabisa wizarani humo zimesema kwamba kigogo huyo amewataka wafanyabiashara hao wakae kimya, wahakikishe mkakati huo hautolewi kwenye vyombo vya habari.

Aidha, katika kuupa nguvu mpango huo, mmoja wa watoto wa viongozi waandamizi serikalini anayesifika kwa kujiingiza kwenye kila biashara iliyo mbele yake, anatajwa kutumika. Mtoto huyo hivi karibuni alisafiri kwenda Uarabuni ambako alikutana na koo za kifalme zinazosaka kwa udi na uvumba vitalu vya uwindaji wa kitalii.

Wakati mpango huo ukisukwa, imebainika kuwa kampuni kadhaa za Watanzania zilizopewa vitalu, zimeviuza kwa matajiri raia wa kigeni. Mmoja wa wanaotajwa kuviuza ni mtu wa karibu na mmoja wa mawaziri walioondolewa wizarani hapo.

Pamoja na ukweli kwamba jambo hilo ni kosa lwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2010, Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuwa kimya.
 
Wizara ya mali ya asili, haishi vituko na vioja...
 
Kama katibu mkuu wa chama kilichoshika dola anatuhumiwa kusafirisha pembe za ndovu nje sasa tutegemee nini kama si madudu zaidi katika hii IMPOTENT GOVERNMENT.
 
Tue, Apr 23rd, 2013


A company dealing with hunting blocks business, Foa Adventure Safaris Limited, has filed a suit at the High Court in Dar es Salaam challenging a decision by the Minister for Tourism and Natural Resources regarding allocation of hunting blocks.


In particular the applicant is challenging the minister's decision to deny the company an opportunity to renew ownership of the hunting blocks and granting the same to four other companies.

The case comes for mention before High Court Judge Zaibabu Mruke today.


While the applicant is seeking the court's redress on the matter, the deadline by the applicant to leave the hunting blocks in controversy was April 1. Already the applicant had complied with the deadline before the disputed hunting blocks were allocated to four other companies.


The hunting blocks which are subject in the case are Rungwa Mwamagembe Game Reserve, Luanda Mkwambi Game Controlled area (North), Rungwa Rungwa Game Reserve (East) and Rungwa Rungwa Game Reserves (West).


In the case, the applicant is seeking for an order for mandamus to compel the Minister to perform the ministerial duties conferred upon him under Section 38 (16) of the Wildlife Conservation Act to consider and decide on an application for review submitted to him by the applicant.


The applicant made an application for administrative review following the decision by the Minister not to allocate him with the hunting blocks and for failure to follow hunting blocks allocation procedures provided for under the law.


Accordance to the law, a party aggrieved by the decision (by the minister) in allocation of hunting blocks may seek for the minister to conduct administrative review of his decision. On October 26, 2011, the applicant lodged their application for the said administrative review which was, however, not granted.


The applicant alleges in the plaint of the suit that the minister's failure to make such a decision has left hanging the company's fate regarding the hunting blocks, the licences for which expired in March 2013.


The applicant further laments that as a result it is unable to pursue further remedies provided by the law to challenge the hunting blocks allocation process, including appeals to the court. According to the plaint of the suit, the last application for administrative review was submitted (by the applicant) on November 15, last year and to date the minister has failed to make a decision notwithstanding various reminders.


Other respondents in the matter are Attorney General, Bushman Hunting Safaris Limited, who had been included in the matter for being allocated with the Rungwa Rungwa Game Reserve (East), Merera Lodges and Tours Limited, who has been given the Rungwa Rungwa Game Reserve (West), Mwanauta Company Limited allocated with Rungwa Mwamagembe Game Reserve and Go Wild Hunting Limited, which has been given the Luanda Mkwambi Game Controlled area (North).



By FAUSTINE KAPAMA, Tanzania Daily News
 
Yaani kila anayepangwa Wizara ya Maliasili na Utalii lazima awe MWIZI?
 
Kama alikuwa in default? Lazima anapewa mwingine.

Afu ni high time waweke wazi hizi taarifa za mipaka, maana ngumu sana kudeal nazo na kujua nani anaishia wapi.
 
Back
Top Bottom