Utafiti uliotolewa hivi karibuni umebaini kuwa watu wanaochelewa kulala wana uwezekano mkubwa wa kufa mapema kuliko wale wanaoamka mapema wakati wa usubuhi.
Watafiti walibaini kuwa watu ambao walikuwa wanachelewa kulala walikuwa na hatari kwa asilimia 10 kufa mapema katika kipindi cha utafiti...
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Isdor Mpango amemuomba Balozi wa Switzerland hapa nchini, Florence Tinguely Mattli, kuishawishi nchi yake iwekeza katika sekta ya mifugo ili kuongeza tija kwa wafugaji na wakulima nchini.
Aidha waziri Mpango aliongeza kuwa Tanzania ina mifugo mingi lakini...
Leo Mei 14, Taifa la Israel linaadhimisha miaka 70 ya uhuru wake. Lakini sherehe hizo huenda zikachochea zaidi uhasama wa kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati ambalo limekuwa na migogoro isiyoisha.
Miaka 70 iliyopita (14 Mei 1948), Waziri Mkuu wa kwanza wa Israel, David Ben-Gurion alisaini...
Kwa mujibu wa Jhumpa Lahiri katika kitabu chake cha The Namesake anasema, “ Kusoma kitabu ni kitendo cha kusafiri bila kusogea kutoka pale ulipo”. Naye David Bowie msanii ajulikanaye kama msomaji mkubwa wa vitabu; alipokuwa akijibu maswali mbalimbali aliyoulizwa kwenye dodoso, alipoulizwa kuhusu...
Hadi kufikia Januari 2018, Deni la taifa la nchi ya Uingereza lilikuwa limefikia dola za Marekani 2.5 trilioni, Japani dola trilioni 9.5, China dola trilioni 4.6, Marekani yenyewe dola trilioni 20 na India deni lake la taifa ni takribani dola trilioni 1.1, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya...
Tunaishi katika dunia ambayo watu wengi wanapenda kujipiga picha ‘selfie’na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Tabia hiyo ya kujipiga selfie inatajwa kuwa ni mapinduzi makubwa ya tasnia ya upigaji picha duniani. Pamoja na uzuri wake kuna matokeo hasi ambayo yanaweza kujitokeza kwa mtu pale...
‘Chloroform’ ni dawa isiyo na rangi na yenye harufu nzuri yenye jina la ‘IUPAC’ lijulikanalo kitaalamu kama ‘Trichloromethane’ na ina fomula ya CHCl3. Chloroform inaweza kukufanya usinzie hata kama itatumiwa kwa dozi ndogo.
Chloroform ni kimiminika chepesi na chenye harufu nzuri ambacho...
Nchi 32 za Afrika ikiwemo Tanzania zimeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kusitisha biashara ya pembe za ndovu ili kuokoa tembo waliosalia barani humo.
Makubaliano hayo yalifikiwa nchini Botswana hivi karibuni katika kongamano la Ujangili wa Tembo na Biashara Haramu ya Wanyamapori ambalo lilijikita...
Pamoja na kukosekana kwa idadi kamili, lakini ukweli ni kuwa Tanzania, kama ilivyo kwa nchi zingine, kumekuwepo ongezeko la wavulana na hata wanaume, kuonekana kuwa na matiti makubwa.
Kawaida, maumbile ya wanaume hayaruhusu kuwa na matiti makubwa. Kwanza yawepo kwa ajili gani?
Matiti makubwa...
“Wananchi wanataka maendeleo. Wanataka huduma bora za jamii. Wanataka maji safi na salama, wanataka elimu bora, huduma za afya, na miundo mbinu bora. Katiba mpya si kipaumbele cha Watanzania. Wananchi wanataka ‘Ukatiba’ na sio katiba. Wananchi wanataka maendeleo”.
“Serikali ya awamu ya Tano...
Machi 22 ya kila mwaka ni siku ya maji duniani. Hii ni siku ya kukuza uelewa kuhusu janga la maji ulimwenguni na kuchukua hatua thabiti za kuleta mabadiliko katika jamii. Kulingana na Shirika la Afya duniani (WHO) asilimia 37 ya Watanzania wanategemea vyanzo vya maji visivyo salama.
Mwenendo...
Hatari ya kupata Ugonjwa wa figo ni kubwa zaidi kwa wanawake kuliko ilivyo kwa wanaume. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali ugonjwa wa figo unawakumba zaidi wanawake tofauti na wanaume ambapo hatari kwa wanawake kupata ugonjwa huo ni asilimia 14 ambapo kwa wanaume ni asilimia 12.
Katika orodha ya...
Shirika la Global Witness limeeleza kuwa watu 197 waliuawa mwaka uliopita kwa kutetea matumizi mazuri ya ardhi, wanyama pori na rasilimali asilia.
Shirika la Global Witness likishirikiana na Jarida la The Guardian limeendesha kampeni ya kulinda na kuhifadhi mazingira duniani kote ambapo...
Baadhi ya watu wamekuwa wakijenga hoja kuwa kuishi, kutembea au kusoma karibu na minara ya simu kunawaweka watu katika hatari ya kupata kansa au matatizo mengine ya afya.
Lakini mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja juu ya hoja hiyo. Katika nadharia za afya kuna sababu chache ambazo...
Ipo dhana kuwa maumivu ya viungo vya mwili ni maradhi yanayowapata watu wenye umri mkubwa pekee. Lakini maumivu hayo yanaweza kumtokea mtu yoyote bila kujali umri.
Kitaalamu maradhi hayo hujulikana kama ‘Arthritis’ ambapo maungio kwenye magoti, mikono, kiuno hupatwa na maumivu, kukakamaa na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.