Hii ndio tiba ya maumivu, kuvimba kwa viungo vya mwili

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Ipo dhana kuwa maumivu ya viungo vya mwili ni maradhi yanayowapata watu wenye umri mkubwa pekee. Lakini maumivu hayo yanaweza kumtokea mtu yoyote bila kujali umri.

Kitaalamu maradhi hayo hujulikana kama ‘Arthritis’ ambapo maungio kwenye magoti, mikono, kiuno hupatwa na maumivu, kukakamaa na kuvimba kwa ngozi ya sehemu husika na wakati mwingine kuwaka moto.

Maumivu hayo hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kulingana na athari aliyopata. ‘Arthritis’ inajitokeza kwa namna mbalimbali kulingana na maumivu yalipojitokeza ikiwemo kukakamaa kwa magoti (osteoarthritis), kuwaka moto (bursitis), kuvunjika na kulegea kwa mifupa (osteoporosis) na kuvimba (rheumatoid arthritis.).

Licha ya arthritis kuhusishwa na umri, kuna sababu zingine hatarishi ambazo zina mahusiano ya karibu na maradhi hayo ikiwemo jinsia. Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha nchini Marekani kinaeleza kuwa asilimia 52 ya watu wazima wanaopatwa na arthritis ni wanawake. Wanawake wako katika hatari zaidi ya kupatwa na maradhi hayo kuliko wanaume.

Sababu nyingine ni uzito kupita kiasi. Watu wenye uzito kupita kiasi wako hatarini kupata maumivu kwenye maungio hasa magotini. Waatalamu wa afya wanaeleza kuwa miguu huelemewa na uzito wa mwili wakati wa kutembea ambapo mifupa husigana na ngozi kuvimba.

Pia baadhi ya kazi zinaweza kuwa kichocheo kwa mtu kupata maumivu hasa ya magotini. Kwa kazi ambazo mtu anatumia muda mwingi kuinama, kuchuchumaa na kusimama, hii zaidi huwapata wafanyakazi wote wa viwandani na bustani.

Hata hivyo, hakuna jambo la kufanya litakalo kulinda dhidi ya arthritis kwa asilimia 100, japokuwa zipo hatua unazoweza kutumia kila siku kupunguza hatari ya kupata maumivu kwenye maungio. Jiepushe na uzito uliopitiliza, kuvuta sigara na kula mlo kamili unaozingatia afya ya mwili.

Zaidi, soma hapa => Arthritis: Maumivu ya viungo yaliyokosa tiba ya uhakika | FikraPevu
 
Back
Top Bottom