Unafahamu kuwa mafuta ya Lavenda, chai huchochea wanaume kuota matiti?

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Pamoja na kukosekana kwa idadi kamili, lakini ukweli ni kuwa Tanzania, kama ilivyo kwa nchi zingine, kumekuwepo ongezeko la wavulana na hata wanaume, kuonekana kuwa na matiti makubwa.

Kawaida, maumbile ya wanaume hayaruhusu kuwa na matiti makubwa. Kwanza yawepo kwa ajili gani?

Matiti makubwa ni maumbile ya wanawake, wanapopevuka na hii hutokea kwa sababu maalum, kwamba msichana anakuwa tayari amebalehe.

Sababu za wanaume kuota matiti zimekuwa zikikanganya; watu wa kawaida na hata wanasayansi, hata hivyo katika siku za hivi karibuni, matokeo ya utafiti ulifanywa Marekani yamekuja na sababu ya kisayansi.

Taasisi ya Mazingira ya Sayansi ya Afya ya Marekani (NIEHS) katika utafiti wake imebaini kuwa kemikali katika mafuta hayo huchochea ongezeko la homoni za kike na kuharibu homoni za kiume kwa wanaotumia.

Uhusiano kati ya ukuaji wa matiti kwa wanaume na matumizi wa mafuta ya mti wa lavenda na ule wa chai, unaonesha kuwa kemikali nane zinazopatikana katika mafuta ya miti hiyo uharibu kazi za homoni za kiume.

Mafuta ya mimea hiyo hupatikana katika bidhaa tofauti kama vile sabuni, mafuta ya kujipaka, mafuta ya kuosha nywele pamoja na bidhaa za kutengeza nywele za bandia.

cape.PNG
cape.PNG

Kemikali hizo zilichunguzwa maabara kwa kuwekwa ndani ya mwili wa binadamu ili kuona ni kwa kiasi gani zinathiri homoni za ‘estrojeni’ na ‘testosteroni.’

Watafiti walibaini kwamba mafuta hayo yamekuwa yakichochea ongezeko la homoni za kike na kuharibu zile za kiume.

Watafiti kutoka NIEHS kwa mara ya kwanza waligundua ushahidi wa madai haya mwaka 2007 ambapo walifanya utafiti wao kwa watoto wa kiume watatu ambao walikuwa wameanza kuota matiti kabla ya kufika kwenye kipindi cha kubalehe.

Watoto hao hawakuwa na matatizo yoyote kiafya, lakini wote walikuwa wakitumia mafuta au bidhaa zenye mafuta ya lavenda na mchai ndani yake. Na pale walipopewa maelekezo ya kuacha kutumia mafuta hayo, ukuaji wa matiti yao ulikoma.

Hivyo matokea ya utafiti yakahitimishwa kwamba kemikali ndani ya mafuta hayo huharibu homoni mwilini ambapo huongeza homoni ya estrojeni na kupunguza kiwango cha testosteroni na hali hiyo huchochea matiti kukua.

Zaidi, soma hapa => TAHADHARI: Mafuta ya lavenda, chai huchochea wanaume kuota matiti | FikraPevu
 
Kuna magonjwa pia ambayo huchochea kuotea matiti kwa wanaume kama vile
1. Kansa ya ubongo
2. Umri kuanzia miaka 50
3. Baadhi ya madawa n.k.
 
Back
Top Bottom