FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 303
- 236
Kwa mujibu wa Jhumpa Lahiri katika kitabu chake cha The Namesake anasema, “ Kusoma kitabu ni kitendo cha kusafiri bila kusogea kutoka pale ulipo”. Naye David Bowie msanii ajulikanaye kama msomaji mkubwa wa vitabu; alipokuwa akijibu maswali mbalimbali aliyoulizwa kwenye dodoso, alipoulizwa kuhusu maana halisi ya “furaha ya kweli ni ipi?”, Bowie alijibu ni kusoma.
Hata hivyo, kuna haja gani kusoma kama huwezi kukumbuka ulichokisoma? Hakuna kitu kinakatisha tamaa kama kuwekeza muda wako kusoma kitabu fulani halafu baadaye ukasahau vyote ulivyosoma. Kuendelea kusoma kitabu fulani ambacho taarifa zake za mwanzo umezisahau ni kama kusoma kitabu kipya kwa kuanzia katikati ya matukio.
Bill Gates husoma vitabu takribani 50 kila mwaka na alitumia njia hizi kuweza kukumbuka yote aliyoyasoma kwenye vitabu hivyo 50;
- Tambua kile kinachokuvutia
- Nakili au andika kile ulichojifunza
- Wasimulie wengine ulichosoma
- Tafakari na husianisha kile ulichosoma na matukio yanayokuzunguka
Zaidi, soma hapa => Fahamu njia 7 za kukusaidia kukumbuka kila kitu ulichosoma