Mataifa Makubwa kama Marekani hukopa wapi fedha?

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Hadi kufikia Januari 2018, Deni la taifa la nchi ya Uingereza lilikuwa limefikia dola za Marekani 2.5 trilioni, Japani dola trilioni 9.5, China dola trilioni 4.6, Marekani yenyewe dola trilioni 20 na India deni lake la taifa ni takribani dola trilioni 1.1, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya www.nationaldebtclocks.org.

Haya ni mataifa makubwa duniani na kulingana na data hizi ni ushahidi kwamba yote yana madeni ya Taifa (national Debt) ambayo ni makubwa sana. Na ili kukukumbusha tu ni kwamba trilioni ina sifuri 12 hivyo viwango hivyo vya pesa hapo juu sio vidogo.

Mara nyingi huwa tunasikia kuhusu madeni makubwa ya nchi mbalimbali kila wakati kwenye taarifa za habari, na huwa tunajiuliza takwimu za madeni hayo ni kubwa kiasi gani?. Pamoja na hayo, Je, umewahi kujiuliza mataifa hayo makubwa duniani huwa yanakopa kwenye nchi gani?. Ni nchi gani huwa zinakopesha nchi hizo ambazo tayari zipo kwenye madeni makubwa sana?.

Zaidi, soma hapa => Mataifa makubwa hukopa wapi?
 
Najua unajifariji kwa taifa lako kuwa na deni dogo kuliko hizo nchi,inamaana hujui kuna World Bank,IMF,nk nk?
 
Back
Top Bottom