Watetezi wa mazingira 4 wanauawa kila wiki duniani

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Shirika la Global Witness limeeleza kuwa watu 197 waliuawa mwaka uliopita kwa kutetea matumizi mazuri ya ardhi, wanyama pori na rasilimali asilia.

Shirika la Global Witness likishirikiana na Jarida la The Guardian limeendesha kampeni ya kulinda na kuhifadhi mazingira duniani kote ambapo lilikusanya data za watetezi wa mazingira ambao walinyanyaswa, kutishwa na serikali zao na mashirika na hatimaye kuuawa.

Kuuawa kwa watu wanaotetea ardhi au rasilimali asilia kulishika kasi mwaka 2017 kuliko wakati mwingine wowote uliopita, ambapo kwa mujibu wa utafiti wa Global Witness unaonesha kuwa watu 4 waliuawa kila wiki duniani kote wakipambana dhidi ya udhalimu unaotokea kwenye machimbo ya madini, mashamba, ujangili na miradi ya miundombinu.

“Hali bado ni tete. Jamii zisipohusishwa kwenye maamuzi ya matumzi ya ardhi na rasilimali asilia, wale wanaotetea wataendelea kuteswa, kufungwa jela na kupokea vitisho vya kuuawa”, amesema Ben Leather, Kiongozi wa Kampeni kutoka Shirika la Global Witness.

Mauaji mengi yalitokea msituni hasa kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Amerika ya Kusini ambako rasilimali nyingi zina mgogoro na mamlaka za kisheria zinazosimamia mazingira.

Sekta ya madini imetajwa kuwa kichocheo kikubwa cha vurugu na vifo vya watu wanaotetea utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi. Mapigano ya migodini yalichangia vifo 36 ambavyo vilihusishwa na ongezeko la mahitaji ya vifaa vya ujenzi.

Zaidi, soma hapa => Mauaji ya Watetezi wa mazingira kikwazo kingine kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi | FikraPevu
 
Back
Top Bottom