Maadhimisho ya miaka 70 ya kujitawala kwa Israel kuchochea uhasama Mashariki ya Kati

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Leo Mei 14, Taifa la Israel linaadhimisha miaka 70 ya uhuru wake. Lakini sherehe hizo huenda zikachochea zaidi uhasama wa kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati ambalo limekuwa na migogoro isiyoisha.

Miaka 70 iliyopita (14 Mei 1948), Waziri Mkuu wa kwanza wa Israel, David Ben-Gurion alisaini azimio la uhuru wa nchi hiyo katikati ya vita vya Waarabu na Wayahudi ambayo ilikuwa inapigania ardhi ya Jerusalemu na ukanda wa gaza.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati, wanaeleza kuwa sherehe hizo zitazidisha uhasama kati yake na Palestina ambazo zimekuwa na ugomvi wa kihistoria kugombania ardhi ya Jerusalem.

Kuchochewa kwa ugomvi huo kunatokana na hatua ya Israel kuhamishia makao makuu ya serikali katika jiji la Jerusalemu kutoka Ter Aviv, wakati bado haijamaliza uhasama na Palestina ambayo ina miliki sehemu ya Mashariki ya jiji hilo.

Zaidi, soma hapa => Israel yaadhimisha miaka 70 ya kujitawala. Tanzania yaendelea kuitambua Palestina
 
Sisi kama Wamarekani wa nchi ya Jiwe kesho tutazindua Ubalozi Jerusalem na tumetia sahihi ya kutohamishwa kutoka hapo.

Watakao leta fyoko fyoko watajuta
 
Israel ni taifa la ajabu sana kila tasnia ya taaluma ulimwenguni hauwakosi ukianza madawa, kilimo, teknolojia siasa kiuchumi lazima tu utakutana na kichwa kimoja cha kiyahudi kimevumbua kitu

Na hii ndio inafanya wayahudi kukumbatiwa na mataifa yote yenye nguvu duniani si ulaya urusi wala marekani

Halafu idadi yao hawafikii hata asilimia moja ya watu ulimwengu kote

70 years anniversary
 
Back
Top Bottom