JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

MADAI Mdau wa JamiiForums ametoa mkasa mmoja unaomhusisha mume wa rafiki yake wa kike aliyeanza kuonesha dalili za ujauzito kwenye ujauzito mchanga wa mkewe. Mdau anaeleza kwamba shemeji yake huyu ilikuwa kila asubuhi anatapika njano, na homa za hapa na pale na kila alipoenda hospital Ugonjwa haukuonekana, ilifikia wakati mwanamme akawa hawezi kufanya shughuli zake kwa sababu ya kutapika sana. Baada ya kupima ilikuja kugundulika kuwa mkewe alikuwa na ujauzito. Ikasemekena kwamba kuna nyakati fulani ujauzito anabeba mwanamke Ila mabadiliko na dalili za ujauzito anakuwa nazo mwanaume. Jambo hili ni kweli au uzushi?
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati akizindua ripoti maalumu iliyoundwa ili kuimarisha uadilifu wa habari kwenye majukwaa ya kidijitali. Kengele ya hatari kuhusu tishio linaloweza kusababishwa na maendeleo yanayokuwa kwa kasi ya Akili Bandia (AI) haipaswi kuficha uharibifu ambao tayari unafanywa na teknolojia za kidijitali zinazowezesha kuenea kwa matamshi ya chuki mtandaoni, pamoja na taarifa potofu na za uongo, alisema. Muhtasari wa sera ya uadilifu wa habari unasema kunapaswa kuwa na wahusika muhimu katika kuhakikisha usahihi unadumishwa, uthabiti na uaminifu wa taarifa zinazosambazwa na watumiaji. “Ni matumaini yangu kwamba (sera hii) itatoa kiwango cha dhahabu kwa ajili ya kuongoza hatua ili kuimarisha...
Salaam Wakuu, Kupitia WhatsApp yangu nimetumiwa ujumbe wa tahadhari kuhusu kuwepo kwa Mvua katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Ujumbe huo unaeleza: Shinyanga, Dar, Pwani, Mafia,Tanga, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kigoma na Kagera tujiandae, kutakuwepo na Pacific El nino na Atlantic El nino, mvua zitakuwa kubwa na hatari sana, Mungu atunusuru. Hali ya hewa tayari imebadilika kuanzia juzi, upepo umeanza katika bahari za Atlantic, Pacific na Hindi, Wavuvi wameanza kuzuiwa kwenda kuvua na Meli za tafiti zimeanza kukumbana na dhoruba kali sana Baharini, picha za satellite sio nzuri kabisa. Tunatarajia magonjwa ya Kuharisha, Dengue, Malaria na Homa kuongezeka, tuchukue tahadhari mapema. Tuangalie nyumba zetu kama zinavuja...
Nimekuwa nikisikia kuwa Rais wa zamani wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi kuwa Daktari wa Malkia wa Uingereza na alihasiwa asije akatembea na Malkia Elizabeth na kuzaa naye. Kuhasiwa kwake huko kulipelekea Dkt. Kamuzu Banda mpaka anafariki dunia mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 99 kutobahatika kupata mtoto yeyote. Malkia Elizabeth ii akiwa na Dkt. Kamuzu Banda (Mwaka 1985)
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume. Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo. Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
Beki wa Simba Che Malome,siku ya tarehe 05.11.2023 wakati wanakandwa kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwaa watani zao Yanga, alionyeshwa kadi mbili za manjano. Kitu ambacho kilipaswa kupewa card nyekundu, lakini refa na wasaidizi wake hawakuliona hili sijui hawakuwa na kumbukumbu vizuri, Che Malome hakutoka nje kwa adhabu ile, alicheza tu. Juzi kati, kati ya Mechi ya Simba na Namungo,Che Malome alicheza tena, Simba walimchezesha mchezaji mwenye card nyekundu kwa sababu zipi? Bodi ya Ligi mko wapi? TFF mko wapi? Wapeni Namungo ushindi wa point tatu na magoli mawili kama kanuni inavyotamka.
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele. Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria. Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar. Huu Muungano ni wa kishenzi sana.
Tulianza na shopping mall Dodoma, sasa tena ni kiwanda cha Tumbaku. Yasemekama wahusika ni wale wale! Ukiingia mjini Morogoro, umbali kidogo kutoka mzunguko wa Msamvu kuelekea Iringa, unakutana na daraja la reli na pembeni yake unakuta shughuli za ujenzi wa kiwanda kipya cha Tumbaku. Eneo hili kwa miaka mingi lilieleweka ni eneo la wazi, na kwa sheria zetu za ardhi, hakuna aliye na madaraka ya kubadili matumizi ya eneo la wazi.
Wakati napitia pitia mitandaoni kutafuta style mpya kwa ajili ya shangazi yenu ndio nikakutana na hili bandiko kuwa aina ya kujamiiana huku mwanamke akiwa amemkalia mwanaume juu ('woman on top' or 'cowgirl' or 'reverse cowgirl'), hatari kwa afya ya mwanaume kwani hupelekea maumivu makali kwani hupekelea fracture ya uume kwa asilimia kubwa wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Inashauriwa mwanaume ndio akae juu ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…