PostGE2025 Tundu Lissu: Nipo tayari kwa mazungumzo nikiwa huru na CHADEMA ikifutiwa kesi zote

PostGE2025 Tundu Lissu: Nipo tayari kwa mazungumzo nikiwa huru na CHADEMA ikifutiwa kesi zote

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,898
Reaction score
16,412
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amewasilisha orodha ya mambo saba muhimu anayoyachukulia kama msingi wa mustakabali wa demokrasia na utawala wa sheria nchini Tanzania.

Soma maamuzi ya Kesi: Mahakama ya rufani yairuhusu CHADEMA kuendelea na shughuli za kisiasa nchini

Ujumbe huo umetolewa, Alhamisi, Aprili 16, 2026, kupitia taarifa kwa umma iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia. Hii ni baada ya Lissu kutembelewa gerezani na Wakili Paul Kisabo.

1776337596105.png

TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawaarifu wanachama wake, wafuasi na umma wa Watanzania kuwa, Wakili Paul Kisabo amemtembelea Mwenyekiti wa chama, Mhe. Tundu Lissu, katika Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, wamejadili kwa kina mwenendo wa kesi mbalimbali zinazomkabili Mhe. Tundu Lissu pamoja na zile zinazoendelea dhidi ya chama.

Aidha, Mhe. Tundu Lissu ameeleza kuwa tarehe 15 Aprili 2026 alipata fursa ya kukutana na Mhe. Lazarus Chakwera, na kuwasilisha kwake masuala yafuatayo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na utawala wa sheria nchini:

1. Kwamba kesi ya Uhaini inayomkabili inatokana na msimamo wake wa No Reforms, No Election, na hivyo kusisitiza kufutwa kwa kesi zote zinazomkabili yeye na chama, pamoja na utayari wake wa kushiriki mazungumzo akiwa huru.

2. Kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu matukio ya Oktoba 2025, kupitia taasisi kama SADC.

3. Uwepo wa mazingira wezeshi kwa mazungumzo ya kweli na utekelezaji wake.

4. Uwajibikaji wa kitaasisi kwa yaliyotokea Oktoba 2025, hususan kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, INEC na TCRA, sambamba na kurejea Ripoti ya Jaji Nyalali (1992).

5. Kufanyika kwa mageuzi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuzingatia Ripoti ya Jaji Chande (2023).

6. Mabadiliko ya mfumo mzima wa uchaguzi, ikiwemo kuundwa kwa chombo kipya huru cha kusimamia uchaguzi, kwa kuzingatia ripoti mbalimbali za waangalizi wa uchaguzi (1995-2025), pamoja na Ripoti za Jaji Warioba na Jaji Nyalali.

7. Umuhimu wa kupatikana kwa Katiba Mpya.

Aidha, Mhe. Lissu amepatiwa nakala ya uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa tarehe 15 Aprili 2026 unaoruhusu chama kuendelea na shughuli zake. Baada ya kuupitia uamuzi huo, ametoa wito kwa wanachama na Watanzania kwa ujumla kujiandaa kwa hatua zinazofuata za kisiasa, akisisitiza umuhimu wa maandalizi ya mikutano ya hadhara.

Chadema kinaendelea kusisitiza dhamira yake ya kupigania haki, demokrasia, utawala bora na maslahi ya wananchi kwa njia za amani na kisheria.

Imetolewa leo Alhamisi, tarehe 16 Aprili, 2026 na;
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi


SnapInsta.to_670661883_18405951169194590_1456568452852532088_n.jpg
SnapInsta.to_670696082_18405951178194590_4962411969441501978_n.jpg
 
Nimetoka Ukonga kumtembelea Tundu Lissu.
Tumepata nafasi ya kujadili kwa kina mwenendo wa kesi zote zinazoendelea na zile zilizo pending. Amenieleza pia kuwa jana, tarehe 15 Aprili 2026, alikutana na Mhe. Lazarus Chakwera na kuwasilisha kwake masuala muhimu yafuatayo:


Nimempatia pia uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa jana kuhusu chama kuendelea kufanya kazi amesema “watu wajiandae, muhimu nijue mkutano utafanyika wapi a day after Ukonga”
mtuhumiwa wa uhaini ni sharti asote mpaka ashike adabu korokoroni
 
Back
Top Bottom