McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 993
- 3,152
Rais. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma, tarehe 08 Mei, 2026 amesema matukio yaliyotokea nyuma hayakuwa na manufaa kwa mtu yeyote na yalisababisha vijana wengi kuingia kwenye matatizo kwa kufuata mkumbo bila kuelewa madhara yake.
"Nililolotokea nyuma halikuwa jema kwa yeyote yule. Na mtego ule anaingia aliyekuwemo na asiyekuwemo... Kumbukumbu lile lilikumba vijana wengi sana na wengi waliingia kwa kutokujua kwa mkumbo. Lakini walivyokamatwa kama mama nikasema waachieni... waachieni watajifunza."
"Niwaombe sana vijana... katika vijiwe vyenu, katika kazi zenu, katika shughuli zenu zote, ambizaneni yasitokee tena. Yale yaliyotokea yametia doa kwenye taifa letu. Tanzania ni nchi ya amani, hayajawahi kutokea yale."
"Sasa tuonyeshe ulimwengu kwamba yaliyotokea si ya Kitanzania na si Utanzania. Ni mambo ya kupandikizwa yaliyotokea. Kwa hiyo sasa tuonyeshe ulimwengu, na nawashukuru mmesema hapana tena, Never Again, hatutaki kuyasikia."