Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa akifanya mahojiano na Bongo FM leo Mei 15, 2026
Mwandishi: "Kwenye hili swala la uhuru, wakosoaji wengi wamekuwa wakikosolea nje ya nchi huku kukiwa na taarifa za watu kutekwa na mambo mengine. Je, huu uhuru una kigezo gani katika vitendo kama hivyo?"
Msigwa: Mtu anayeamua kwenda nje ya nchi na akaanza kukosoa, kwanza kwa tathmini ambayo sisi tumeifanya, wengi ni wale ambao wanataka kuutumia uhuru vibaya. Au kutumia uhuru kudhalilisha watu, kuhatarisha usalama wa nchi, kupotosha, au kuzua taharuki; mambo ambayo kwa mujibu wa sheria hayaruhusiwi. Kwa sababu uhuru nao una mipaka yake.
Na kwa bahati mbaya, kwa sababu mbalimbali, wengi wao wamekuwa katika miradi au mipango ya watu wenye malengo hasi dhidi ya nchi. Na huo ni ukweli wa wazi kabisa kwa sababu tunao watu ambao tumeona wanavunja sheria wakitumia fursa ya teknolojia, iwe ni mitandao ya kijamii au vyombo vya habari, kuleta taharuki ndani ya nchi na kutoa taarifa za upotoshaji.