Zuio la VPN: Kwanini Mamlaka zinaikimbia Teknolojia wakati dunia inaelekea huko?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
1697269509325.png

Wadau, bila shaka mmeliona tangazo la TCRA kuhusu onyo la matumizi ya Kipenya Mtando Binafsi (VPN), tangazo ambalo ni dhahiri linaonesha Mamlaka zinaogopa Teknolojia kuliko kuwekeza zaidi katika kutambua fursa zilizoko kwenye uwanda huo.

Katika dunia ya sasa Mamlaka zinapaswa kuweka mazingira rafiki kwenye Teknolojia kuliko kuweka vikwazo katika ufikiaji wake. Kitendo cha TCRA kutangaza kuwa wanaotumia VPN wajisajili kwa Mamlaka hizo ili wajulikane wanachokifanya kwanza ni kuingia uhuru wa watu katika kazi zao na faragha zao. Pia, ni kupoteza rasilimali za Serikali kufuatilia vitu visivyo na impact yoyote kwenye uchumi wala maisha ya Mtanzania.

Sasa sijui kwamba TCRA hawajui au ni kupuuza tu? VPN ni njia moja wapo ya kujilinda dhidi ya mashambulio ya udukuzi mtandaoni, sasa mamlaka zinapozuia inamaana zinataka watu wawe kwenye hatari ya kushambuliwa na kupoteza taarifa zao binafsi

Ni jambo la ajabu kwa TCRA kudhani kuwa kila anayetumia VPN anatafuta mtandaoni maudhui yasiyofaa au yaliyokatazwa. Kitendo cha Mamlaka hiyo kutaka wanaotumia VPN kuzitaja na kutoa anuani zao ni dhahiri kuwa Mamlaka zinataka kujua kila kinachofanywa mtandaoni na watumiaji kwa maanai hiyo inataka kuingilia TAARIFA BINAFSI za watu mtandaoni kitu ambacho si sahihi.

Serikali ina mambo mengi ya kufanya kuliko kuhangaika na masuala haya. Badala ya kupoteza muda kuhangaika na kujua watu wanafanya nini mtandaoni, Serikali ijikite katika kuwawezesha vijana kwenye Start Ups zao. Ikumbukwe VPN ni uvumbuzi, sasa kama Serikali inazuia matumizi yake inamaanisha vijana wabunifu wa programs katika mipango yao wasibuni kitu cha aina hiyo nchini kwasababu hakitapa kibali cha kutumika hapa.

Nashindwa kuelewa mipango yetu kwenye Teknolojia inalenga nini. Anyway niishie hapo.
 
View attachment 2781613

Tuna jambo letu
 
Watawala wenyewe ndiyo hao wanaosema wananchi wasitumie mitandao ila watumie Internet, hivi sasa wamejawa na hofu kutokana na kutoijua teknolojia, fikiria tu wanaikwepa teknolojia ya Starlink ati wanasema haina uhakika sijui huo utaalamu wameupata wapi
 
Back
Top Bottom