Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,830
VPN(Virtual Private Network) huwa inaficha utambulisho wa vifaa vya mtandaO(IP address) na kuimarisha hata usalama wa mtumiaji kuingiliwa mawasiliano yako na mtu mwenye nia ovu.
Serikali nyingi duniani hazijakataza matumizi ya VPN ikiwemo Ulaya na Marekani lakini zipo Serikali chache zimeweka adhabu kali watakaokiuka masharti yaliyowekwa kwenye matumizi ya VPN.
Baadhi ya Serikali katika nchi tajwa zimekuwa zikiwajua watumiaji hao kwa kumtumia ISP(Mtu anayesambaza internet) ambae anawachunguza watumiaji wa mtandao wake kama wanajiunga na VPN.
Namna ya pili ni ukaguzi wa vifaa, unaenda polisi na wakikagua simu yako linakuwa kosa tayari au ukaguzi wa ghafla mitaani.
Tanzania
Mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania imetumia Kanuni ya 16(2) ya mwaka 2020 kwenye kanuni za Posta ambayo inakataza matumizi ya kitu chochote kinachoruhusu au kumsaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyodhibitiwa.
Tanzania ilianza kwa kuzuia tovuti za ngono kama Urusi walivyofanya na baadae kufuta na matumizi ya VPN.
Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Serikali nyingi duniani hazijakataza matumizi ya VPN ikiwemo Ulaya na Marekani lakini zipo Serikali chache zimeweka adhabu kali watakaokiuka masharti yaliyowekwa kwenye matumizi ya VPN.
- China
Serikali ya China imetenga bajeti kubwa sana kwaajili ya ujasusi wa ndani na matumizi ya mtandao. Pamoja na hayo hamna sheria inayokataza matumizi ya VPN China lakini Serikali ya China inataka useme matumizi ya VPN ili upewe leseni ya matumizi na Serikali
- Urusi
Baada ya maandamano ya 2012, Serikali ya Urusi ilitoa orodha ya tovuti na kuzipiga marufuku na mwanzo walianza na kupiga marufuku tovuti zinazohusika na video za ngono za watoto kama geresha lakini ghafla zikaingizwa tovuti nyingi sana zenye mlengo tofauti na Serikali ya Urusi iliyo madarakani. Mwaka 2017 VPN zilikatazwa rasmi nchini Urusi
- Korea Kaskazin
Korea wana internet inayodhibitiwa vikali na Serikali inayoitwa "Kwangmyong". VPN hamna kabisa na mitandao ya Maghribi marufuku.
- Belarus
Sheria yao haijakataza matumizi ya VPN lakini imekataza teknolojia zote zinazomficha mtumiaji mtandaoni. Serikali ya Belarus haina aibu katika kutumia nguvu zilizopitiliza kuzima maandamano ikiwemo kuzima kabisa internet. Pamoja na faini kubwa za kutumia VPN nchini Belarus, wananchi wake wengi wanatumia.
- Turkmenistan
Serikali ya Turkmenistan ilipiga marufuku VPN mwaka 2019, Serikali ililazimisha wananchi kuapa kwa kutumia kitabu cha Quran kwamba hawatatumia VPN. Kati ya wananchi milioni 6.3, ni milioni 2 tu wanaoweza kuwa na mtandao wa Internet, unatakiwa kuomba na kupitia 'vetting' kabla ya kupata ruhusa ya kutumia mtandao.
- Iran
VPN imekatazwa tangu 2013, zinaruhusiwa zilizoruhusiwa na Serikali pekee ambazo wana udhibiti nazo. Serikali ya Iran ilizima kabisa mtandao mwaka 2022 baada ya kutokea maandamano.
- Iraq
Mwaka 2014 walipiga marufuku na hamna udhuru wowote unaoruhusiwa kutumia VPN
- Uturuki
Mwaka 2016 ikitoa sababu ya kupambana na ugaidi, Serikali walipiga marufuku ya matumizi ya VPN.
- Mnyanmar
Mwaka 2021 nchi hiyo ilipitia mabadiliko makubwa ya kisiasa baada uongozi wa kidemokrasia kufurushwa na mapinduzi ya kijeshi. Januari 2022 Serikali ya Kijeshi ilitengeneza Sheria ya kukataza matumizi ya VPN, sheria hiyo iliruhusu wananchi kukaguliwa simu zao mitaani kuangalia kama wanatumia VPN.
- Pakistan
Ili uweze kutoa huduma ya VPN lazima usajiliwe na Serikali ya pakistan, watoa huduma wanazimika kupeleka taarifa za watumiaji wake Serikali ikizihitaji.