Zuhura Yunus: Rais Samia alizungumza na Idris Elba kuhusu ujenzi wa studio ya kisasa ya Filamu Nchini Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhuru Yunus amesema moja ya mambo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD alipokuwa Davos nchini Uswizi ni kuhusu ujenzi wa studio kwa ajili ya filamu.

Zuhura amesema kilichofanyika ni mazungumzo ya awali bila kutoa taarifa kwa undani kuhusu mikakati zaidi.

Fm6QsG-X0AE0gOz.jpg
 
Badilisheni Sera za nchi kuhusu mambo mengi ya filamu.

Bado tuna makatazo ya ajabu sana uniform za police, utepe tu wa police marufuku kutumia kwa raia. Kituo cha police huwezi igizia wala lock up zao so tuna safari ndefu sana wakuu
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhuru Yunus amesema moja ya mambo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye
Hivi Idris Elba ni actor au producer? Vitu vingine ni kutafuta tu za photo opportunity na watu unaowachunuku. Kuwa muigizaji maarufu hakukufanyi kuwa producer maarufu, Samia hajui hilo? Mambo ya studio angemtafuta producer maarufu, sio muigizaji maarufu.
 
Back
Top Bottom