Zuchu ataweka rekodi mpya kwenye project yake mpya ya 4-4-2

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,522
7,370
20220629_184007.jpg

Zuchu anaenda kuachia project mpya ya 4-4-2.

Kama kawaida queen huyu wa bongofleva na msanii namba moja wa kike Africa mashariki na kati anaenda kuandika rekodi mpya kama kawaida yake.

Huyu mtoto ni wamoto sana na anaubeba kwa mikono miwili muziki wetu wa Africa mashariki ndio maana sina shaka anaenda kuandika rekodi mpya mbali na rekodi mbalimbali alizoandika tayari.

Ikitokea asiandike rekodi yoyote mpya basi mniite mbwa mtanikuta Sinza kwa remmy nimekaa.
 
Tulia uone maajabu ya Zuchu alafu ndio mtaelewa watu walivyo serious na huu muziki
Sasa wewe sinza pazuri kweli umeona huyu ni mwanamziki au msanii? Kuna tofauti kubwa kati ya hivi vitu. Kimziki watu siku hizi wanabebwa na usanii ila hata tuzo za BET hatutoi 🧐 Sasa huyu atavunja record kumshindanisha na nani?

Tuanzie hapa.
 
Yaan shogaa angu unavojitahidi kumpamba huyo Zuhura utadhani ana cha maana, ko akikupa bundle basi wee unaweweseka mnooo.
Lol
 
Hahahaha, M bongo ni mtu pekee ambae hajui anataka nini.

Watu wanakuponda kwa kumtabilia mema msanii mzawa, ila hawahawa badae utawakuta wanasema wanaijeria wanabebana kimuziki ndomana wanafanikiwa.

Tutafikaje akati hatutaki hata kupongeza hatua ndogo ambazo wasanii wetu wamesogea? Kila kitu tunabeza.

Mwingine anasema hakuna mwanamziki hapo, mwingine anasema avunje record kwa mziki gani anaoimba, alafu hawahawa wanataka mziki wetu ufike mbali kama wanaijeria.
 
Sasa wewe sinza pazuri kweli umeona huyu ni mwanamziki au msanii? Kuna tofauti kubwa kati ya hivi vitu. Kimziki watu siku hizi wanabebwa na usanii ila hata tuzo za BET hatutoi 🧐 Sasa huyu atavunja record kumshindanisha na nani?
Tuanzie hapa. .
Bado masaa machache mkuu vuta subira uone moto wa Zuchu.

Tuzo ya BET tunayo moja ipo Wasafi pale
 
Hahahaha, M bongo ni mtu pekee ambae hajui anataka nini.

Watu wanakuponda kwa kumtabilia mema msanii mzawa, ila hawahawa badae utawakuta wanasema wanaijeria wanabebana kimuziki ndomana wanafanikiwa.

Tutafikaje akati hatutaki hata kupongeza hatua ndogo ambazo wasanii wetu wamesogea? Kila kitu tunabeza.

Mwingine anasema hakuna mwanamziki hapo, mwingine anasema avunje record kwa mziki gani anaoimba, alafu hawahawa wanataka mziki wetu ufike mbali kama wanaijeria.
Kinachowasumbua ni wivu na roho mbaya
 
Back
Top Bottom