BASATA Watangaza kusitisha Shughuli za Sanaa na sherehe katika kumbi 504 Tanzania bara

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHA SHUGHULI ZA SANAA, SHEREHE NA BURUDANI KATIΚΑ KUMBI 504 ΤΑΝΖΑΝΙΑ BARA.​
Mnamo tarehe 19 Februari, 2024 Baraza lilitoa tamko la nia ya kusitisha huduma kwa kumbi 653 ndani ya siku 14 kwa wadau wote ambao hawatatimiza vigezo vya kuhuisha vibali vya kufanya shughuli za Sanaa, Sherehe na Burudani nchini.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, ni kumbi 149 tu ndizo zimetekeleza. Hivyo basi, Baraza kupitia masharti ya usajili ya Kanuni ya 59 linasitisha rasmi shughuli za Sanaa, sherehe na burudani katika kumbi 504 Tanzania Bara (Orodha ya kumbi 504 imeambatishwa) kuanzia tarehe 28 Machi, 2024 mpaka watakapolipia vibali kupitia kiungo AMIS. Baraza litashirikiana na mamlaka nyingine za Serikali wakiwemo Maafisa Utamaduni kote nchini ambao kimsingi ni Wasajili Wasaidizi kufuatilia watakaondelea kukiuka Sheria na Kanuni za BASATA.

Ofisi za BASATA zitakuwa wazi kwa siku ya Jumamosi na Sikukuu kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita mchana kwa ajili ya kutoa huduma.

Aidha, Baraza linawakumbusha wamiliki wa kumbi ambao hawajasajiliwa/hawanavibali HAI vya kuendesha shughuli za Sanaa, starehe na burudani wajisajili mara moja ili kuepuka usumbufu. Umuhimu wa kuwa na KIBALI cha BASATA ni pamoja na kuzitambua na kuzisimamia kumbi ili zitimize matakwa ya Kisheria ikiwemo kuzingatia usalama wa watu. Kwa msaada piga simu 0759942512.


1711661922138.png

1711661976668.png

1711662013355.png

1711662084163.png

1711662126896.png

1711662154960.png

1711662181355.png

1711662208115.png

1711662233492.png

1711662263867.png

1711662301487.png

1711662326624.png

1711662356921.png

1711662382650.png

1711662409078.png

1711662432045.png

1711662467602.png
 
BASATA iseme tu inazikumbusha, kumbi hizi watu wameshalipia kwa shughuli mbalimbali in advance
 
Back
Top Bottom