Unafiki wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,600
11,253
Kitendo cha serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, kupitia Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na utamaduni la Zanzibar, kumfungia msanii Zuhura Othman Masoud (Zuchu), kutojihusisha na shughuli za muziki kwa miezi sita pia kutaka vituo vya runinga na redio kutopiga Wala kuonesha wimbo wowote ni uamuzi ambao niwa kinafiki wa serikali ya Zanzibar.

Madai ya kwamba maudhui yalikuwa kinyume na maadili, niya kweli kabisa na yasiyo tia shaka, lakini toka lini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikawa mlinzi wa maadili ikiwa yenyewe ndo kinara wa kupotosha maadili, wanayodai kuyalinda kwa nguvu zote.

Kupitia Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, walimualika shoga Richard Quest kutoka Uingereza kwa lengo la kunadi shughuli mbalimbali za utalii ndani ya Zanzibar.

Hapa ndiyo unafiki wa SMZ, unapokuwa wazi na dhahiri bila shaka yoyote. Serikali inamfungia Zuchu kwa madai ya kulinda maadili na wakati huo huo wanatumia watu wasio na maadili katika shughuli rasmi za kiserikali.

Kama serikali ya Zanzibar, ina wajibu wa kulinda maadili ndani ya Zanzibar, haina budi kutenda yale yenye maadili pia, sio unafiki kama huu kutenda yaliyo kinyume.
 
Ushauri wangu, Zanzibar nawaomba mfuate tamaduni za kiislamu, na sio maadili au tamaduni ya kizanzibari. Huwezi ukamfungia miezi 6 zuchu kisha anarudi tena kazini kuonyesha mwili wake kwa umati wa Wazanzibari na waislamu kwa ujumla, maanake mmehalalisha miziki, ngumi n.k. Hapo mnachotakiwa fungieni kila kitu kilichoharamishwa na Mwenyezi Mungu, na sio kusema utamaduni mara sijui maadili ya yakizanzibari, itapendeza sana mkafuata tamaduni za kiislamu. Ni hayo tu.
 
Hakuna watu wachafu kimaadili ya ngono kama waarabu...no wonder mwizi huwa anajilinda sana asiibiwe...
 
Hakuna watu wachafu kimaadili ya ngono kama waarabu...no wonder mwizi huwa anajilinda sana asiibiwe...
Waarabu wameingiaje tena hapa sheikh!!?
Mana kama unazungumzia zanzibar ya waarabu kwa miaka hii haipo tena. Hata hio SMZ labda katika viongozi 100 mmoja ndio mwarabu.
 
Hakuna watu wachafu kimaadili ya ngono kama waarabu...no wonder mwizi huwa anajilinda sana asiibiwe...

Mhhm! Waarabu wameingiaje tena hapa! Chuki mbaya sana mkuu, matokeo yake ndio haya unaandika bila kujua mada inahusu nini!
 
Tuna ongozwa na viongozi wa ajabu sana.Ndio maana linaitwa bara la kiza.
Kwa hili ambalo nimeshuhudia clip ya huyo msanii akiimba mambo yasiyo faa publicly nawaunga mkono na miguu , wako makini sana hata kutushinda huku Bara ambako wao wako bize kuwafungia akina Ney wa mitego...
 
Kila siku nasemaga tatizo la nchi hii sio CCM bali ni raia wapumbavu walio jaa ndani ya nchi hii akiwemo mleta mada, kwahiyo suala la Zuchu kufungiwa limekuwa jambo zito sana na muhimu sana kwa nchi mpaka ligeuke kuwa mjadala wa kitaifa?
 
Ushauri wangu, Zanzibar nawaomba mfuate tamaduni za kiislamu, na sio maadili au tamaduni ya kizanzibari. Huwezi ukamfungia miezi 6 zuchu kisha anarudi tena kazini kuonyesha mwili wake kwa umati wa Wazanzibari na waislamu kwa ujumla, maanake mmehalalisha miziki, ngumi n.k. Hapo mnachotakiwa fungieni kila kitu kilichoharamishwa na Mwenyezi Mungu, na sio kusema utamaduni mara sijui maadili ya yakizanzibari, itapendeza sana mkafuata tamaduni za kiislamu. Ni hayo tu.
Ni ngumu sana mkuu,kulinda maadili wakati huo huo pesa zinapatikana kwenye mambo yasiyo ya maadili,wewe huoni namna serikali isivyo na usemi juu ya ushoga na mashoga sababu ya pesa za mabeberu.
 
Kwa hili ambalo nimeshuhudia clip ya huyo msanii akiimba mambo yasiyo faa publicly nawaunga mkono na miguu , wako makini sana hata kutushinda huku Bara ambako wao wako bize kuwafungia akina Ney wa mitego...
Ndio maana nimeuliza kama Zuchu kafungiwa sababu ya kuongea mambo yasiyo faa kwa umma kwa kile kinacho daiwa sio maadili kwa sasa serikali hiyo hiyo inayo jinasibisha kulinda maadili ina tenda yasiyo ya kimaadili mfano ni hilo la kumpa mwaliko shoga Richard Quest kutangaza utalii.
 
Kila siku nasemaga tatizo la nchi hii sio CCM bali ni raia wapumbavu walio jaa ndani ya nchi hii akiwemo mleta mada, kwahiyo suala la Zuchu kufungiwa limekuwa jambo zito sana na muhimu sana kwa nchi mpaka ligeuke kuwa mjadala wa kitaifa?
Hii ni JF,nyuzi zipo kibao,nenda kachangia nyuzi zenye mijadala ya kitaifa,ni ajabu kujiona mwenye akili kubwa kuliko wengine.
 
Back
Top Bottom