Zombe Aishitaki serikali, adai 5.2 Billion!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zombe Aishitaki serikali, adai 5.2 Billion!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Msharika, Jan 19, 2011.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapa Muheshimiwa Zombe anaelekea kulamba fidia ya 5 bilioni. Je huu ni udhaifu wa serikali kugeuka shamba la bibi?
  Source: Zombe sasa kuishitaki serikali

  Nani alaumiwe katika hili?
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duu, hii kali.... bado mramba, yona na mgonja wakishinda!!!!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Let me see. This guy killed. There was enough evidence to convict him but had a vital witness killed in jail. And now he wants $5 million?
  These types of people should be shot on sight. Na serikali yetu ilivyo jinga italipa.
   
 4. czar

  czar JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Saafi shitaki chota pay anza zako kwa amani TZ ni shamba la bibi. Kukurupuka kushtaki watu ili serikali ionekane inafanya kazi kutatufilisi, bado kina Mramba na wenzake sikilizieni. Hafu unakuta m2 kavaa shati, kofia, khanga za ccm. Bongo lala.
   
 5. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  "...karata ya kwanza ya kumtest kama anaingilika kwa gia ya 'mwenzetu' ndio iliyomtoa Zombe pangoni..." Wenye kutafakari wanaelewa....
   
 6. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kama kawa
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  .............. usingoje kesho
   
 8. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Wakupe tuu fidia na waje wengine wakina mramba etc, nao wapewe hii serikali kila mtu anajijichotea kweli watawala wetu most of them are useless
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  mchezo hatari huu mara kesi ije imgeuke...
   
 10. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Akina mgonja na mramba nao tunawasubiri kuchuma 'maembe' kwenye shamba la bibi jk.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  The guy has some nerves, lakini all in all mi naamini malipo ni hapahapa.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135

  It is Time now to kill Zombe and close the Case. Just one Bullet just one.

  I have a gun, can someone give me ammunition?
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Zombe sasa kuishitaki serikali
  • Aidai fidia bil. 5/- kwa kukiuka Katiba na sheria

  na Happiness Katabazi


  [​IMG] HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Mohamed Zombe, ametangaza rasmi nia yake ya kuishitaki serikali kwa hoja kuwa ilikiuka sheria na Katiba ya nchi wakati ilipomkamata na kumfungulia kesi ya mauaji.
  Zombe alikamatwa mwaka 2006 na kufunguliwa kesi ya mauaji ya watu wanne lakini aliishinda serikali katika kesi hiyo.
  Uamuzi huo ameutangaza baada ya siku 90 alizotoa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwomba radhi na kumlipa fidia ya sh bilioni tano kumalizika.
  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, kamishina huyo wa zamani kupitia kwa wakili wake, Richard Rweyongeza, alikabidhi notisi hiyo ya siku 90 kwa IGP Mwema Septemba 27 mwaka jana, akisisitiza atakwenda mahakamani iwapo masharti hayo ya kuombwa radhi na kulipwa fidia hayatatekelezwa.
  Alisema siku tisini hizo zilimalizika rasmi Desemba 25 mwaka jana huku IGP Mwema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa hawajamjibu chochote mpaka sasa.
  Kwa mujibu wa hati hiyo ambayo gazeti hili linayo nakala yake, Jeshi la Polisi lilikiuka sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 inayotaka kabla ya mtu kukamatwa ni lazima aelezwe anakamatwa kwa sababu gani na akifikishwa kituo cha polisi ni lazima ahojiwe na kuchukuliwa maelezo yake ambayo baadaye hutumika mahakamani kama kielelezo.
  Mbali na hilo, Jeshi la Polisi lilikiuka pia haki za msingi za binadamu na Ibara ya 15(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayosomeka kama ifuatavyo:
  “Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-
  “(a) Katika hali na kwakufuata utaratibu uliowekwa na sheria.”

  Akiongea kwa kujiamini huku akilionyesha gazeti hili hukumu mbalimbali ambazo Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa zilizokuwa zimekatwa na serikali dhidi ya wananchi walioshinda kesi za mauaji katika mazingira kama aliyoshinda yeye, Zombe alisema serikali kama serikali ni nzuri ila kuna baadhi ya watendaji wana hulka za kinyang’au na hawatimizi wajibu wao kama inavyotakiwa.
  “Nafahamu kwamba DPP amekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati, ambayo ilituachilia huru mimi na wenzangu tisa….hilo halinitishi.
  “Nimewasilisha hati hiyo ya nia ya kutaka kuwashitaki na hawajanijibu, hivyo imeonyesha wazi wapo tayari kwenda mahakamani, na mimi na wakili tupo tayari na muda wowote kuanzia leo tunakwenda Mahakama Kuu kufungua kesi ya kudai sh bilioni tano ikiwa ni fidia ya usumbufu na kunyanyaswa kipindi kile nilipokuwa nakabiliwa na kesi ile ya mauaji.
  “Sasa kitendo cha Jeshi la Polisi kunikamata na kunifikisha mahakamani na kwenda kuishi gerezani kwa miaka minne bila kuhojiwa na polisi, je, si ndiyo lilikiuka sheria na Katiba zilizotungwa na Bunge, ambapo na huyu huyu IGP aliapa kuilinda Katiba hiyo?” alihoji huku akionyesha kukerwa na jambo hilo.
  Zombe ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake zinazomuingizia kipato huko mkoani Morogoro, alisema anataka hilo liwe fundisho kwa Jeshi la Polisi ambalo baadhi ya askari wake wamekuwa wakikiuka taratibu kwa makusudi na kuonea wananchi wasio na hatia.
  Agosti 17, mwaka 2009, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwachilia huru Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.
  Serikali ilikata rufaa Oktoba 7 mwaka 2009 katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachilia Zombe na wenzake.
  Akisoma hukumu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, alibaini kuwa serikali ilishindwa kuthibitisha mashitaka na kuwa kamwe mahakama haiwezi kumhukumu mshitakiwa kwa ushahidi dhaifu na wa kusikia kama uliowasilishwa mahakamani hapo, kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria.
  Kwamba washitakiwa hao si wauaji na aliliagiza Jeshi la Polisi liwatafute wauaji halisi wa marehemu wale.
   
 14. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Dowans nyingine shamba la bibi hilo kula
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Inaelekea Zombe ushindi alioupata pale High Court ulikuwa ni wa mezani kwa nini hasubiri mpaka Mahakama Ya Rufaa iamue suala lake kabla ya kuanza kesi ya madai................Hizo hoja anazotaka kuzianzisha zitaingilia uhuru wwa Mahamaka ya Rufani na kamwe kugoinganisha mahakama hairuhusiwi.............................

  Swali ni je ni kwa nini ZOmbe anaanza hiki kiherehere...............................ninaamini kuwa anajaribu kuwatisha ili wamfutie ile rufani na wala siyo vinginevyo jambo ambalo haliwezekani kabisa....................
   
 16. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  du mkuki kwa nguruwe,hivi zombe alivokuwa mafia anakamata wa2 na kuwasingizia kesi pia kuuwa wengi leo hii naye kasema hakutendewa haki! ye2 majicho ka si macho
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Mtuhumiwa ana haki gani anapokamatwa na polisi?
  [​IMG]

  Allan Kajembe

  [​IMG] HABARI za wakati huu msomaji wa Tanzania Daima. Nakutakia mwaka wenye amani na mafanikio.
  Kwa kuanza ni vizuri tukatupa jicho letu katika haki za msingi za mtuhumiwa wa kosa au makosa ya jinai pindi anapokamtwa na polisi.
  Kuna mambo kadhaa unayotakiwa uyajue, ambayo mtuhumiwa wa kosa la jinai anatakiwa afanyiwe wakati wa kupekuliwa au kukamatwa.
  Kwanza, kumkamata mtuhumiwa kunaweza kuwa kwa kutumia hati ya kumkamata au inaweza kufanyika bila kutumia hati ya kumkamata.
  Kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, iwapo mtuhumiwa atakuwa ameshafunguliwa mashitaka, basi mahakama kwa kutumia hakimu wake itamuita kwa kutumia hati ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kama mtuhumiwa huyo atakuwa hajafunguliwa mashitaka kabla hajakamatwa, basi samansi itatumika na wakati mwingine mtuhumiwa anaweza kukamatwa bila hata kutumia hati ya kukamata.
  Kumkamata mtuhumiwa bila kutumia hati ya kukamata kunaweza kufanywa na mtu yeyote, si lazima ofisa wa polisi kama ambavyo kifungu cha 16 na 14 cha sheria hii kinavyotamka bayana.
  Miongoni mwa watu ambao pia wanaweza kumkamata mtuhumiwa wa kosa la jinai ni pamoja na hakimu wa mahakama yoyote iliyowekwa kisheria, walinzi wa amani, yaani wajumbe wa nyumba kumi/mabalozi wa nyumba kumi na ofisa watendaji wa kata na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa.
  Hata hivyo, watu hawa watamkamata mtuhumiwa ikiwa tu kama mtu huyo atakuwa anafanya kosa la jinai lililo ainishwa chini ya kifungu cha 18 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  Kimsingi ni jukumu la ofisa wa polisi au mtu yeyote anayemkamata mtuhumiwa, kumtaarifu mtuhumiwa huyo sababau ya kumkamata na si kumkamata kiholela kama ambavyo wakati mwingine inafanyika.
  Hali hii wakati mwingine inasababisha watuhumiwa kukataa kukamatwa na hivyo kuleta mtafaruku baina yao na mtu/watu wanaoenda kutimiza wajibu wao wa kisheria kuwakamata watuhumiwa hao.
  Hiki ni kigezo muhimu cha kisheria kwa watu wanaokwenda kuwakamata watuhumiwa wao kukitimiza kabla ya kuwakamata.
  Kwa upande wa watu wasio askari wanaokwenda kuwakamata watuhumiwa, inawalizimu kuwakabidhi watuhumiwa hao katika mamlaka zinazohusika bila kuchelewa.
  Na kwa mamlaka husika tuna maanisha ampeleke mtuhumiwa kituo cha polisi au mahakama iliyo karibu naye.
  Hii ni muhumu kwa sabababu watu binafsi hawana nyenzo au mahala panakokidhi viwango vya kuwaweka watuhumiwa na zaidi ya yote kuna uwezekano mkubwa kwa wao kutozingatia kanuni na vigezo muhimu vya kisheria katika kuwahifadhi watuhumiwa wao.
  Mfano mzuri tunaupata katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Dastur, A.L.R 421, ambapo mtuhumiwa aligoma kukamatwa kwa kutoambiwa sababu ya kukamatwa.
  Zaidi ya hapo, mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma nacho askari mmoja wapo kati ya watatu waliokwenda kumkamata.
  Mahakama baada ya kuridhika na maelezo yake, ilisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na haki ya kuelezwa sababu ya kukamatwa.
  Kitu kingine cha msingi ambacho unatakiwa kujua ni kwamba mtu anayetakiwa kumkamata mtuhumiwa ni kwamba anatakiwa kutotumia nguvu za ziada wakati wa kumkamata mtuhumiwa.
  Hii inamaana kwamba, vitu kama pingu, kumshika mtu kibindo na kadhalika, vinatakiwa kutumika ikiwa tu mtuhumiwa mwenyewe atakuwa anakataa kukamatwa kihalali.
  Hii ndiyo maana ya nguvu za ziada kama zilivyoelezewa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  Kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama katika kesi ya M'bui dhidi ya Dyer,(1967) E.A 315, ikiwa kama ofisa wa polisi (au mtu yeyote anayemkamata mtuhumiwa) atatumia nguvu za ziada kumkamata mtuhumiwa, basi mtuhumiwa huyo anaweza kumfungulia madai ya kutumia nguvu za ziada kumkamata.
  Hata hivyo, suala la kuamua kama nguvu za ziada zimetumika au la, litaamulia kutokana na mazingira
  ya kesi yenyewe.

  Sheria hii pia imetoa mamlaka kwa polisi kuvunja nyumba ili kumkamata mtuhumiwa aliyejifungia ndani, kama ambavyo kifungu cha 19 na 20 cha sheria hii kinavyoelekeza.
  Hii ni kwa sababu inawezekana kwa mtuhumiwa wa kosa la jinai akajifungia ndani ya nyumba au jengo ili akimbie mkono wa sheria.
  Hivyo kwa kutambua hilo ndipo chini ya kifungu cha 20 cha sheria kikatoa msimamo huu.
  Pamoja na hayo yote, sheria hii imekataza kitendo cha kuwakamata watoto au mke/mume wa mtuhumiwa kwa madhumuni ya kumshurutisha mtuhumiwa ajisalimishe katika mkono wa sheria.
  Kitendo hiki ni kinyume cha sheria kama ilivyoamriwa katika kesi ya Lulu Titu dhidi ya Jamhuri (1968), H.C.D 30 ambapo mke wa mtuhumiwa alikamatwa na polisi kwa nia ya kumshurutisha mthumiwa ‘ajisalimishe' polisi.
  Katika maamuzi yake , mahakama ilisema kwamba kitendo hiki ni kinyume cha sheria na kanuni za msingi za haki na kwamba mke wa mtuhumiwa anaweza kuwafungulia polisi shauri la madai kwa kudai fidia.
  Kwa upande wa kumpekua mtuhumiwa au nyumba yake, kitendo hiki pia kinaweza kufanywa kwa kutumia hati ya kupekua au bila hata kutumia hati ya kupekua.
  Ndugu msomaji unatakiwa kujua kwamba kuna mazingira yanayoweza kumlazimisha askari kukupekua bila kuwa na hati ya kukupekua, na hii mara nyingi hutoke pale ambapo suala lililokuwepo ni dharura.
  Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai pia imeiingiza dhana hii katika vifungu vyake. Hata hivyo, mtu mwenye jinsia ya kike ni lazima apekuliwe na mwanamke mwenzake na hivyo hivyo kwa mwanaume ambaye naye ni lazima apekuliwe na askari mwenye jinsia ya kiume.
  Hii ni katika kulinda heshima na utu wa mtuhumiwa anayepekuliwa.
  Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria hii. Kitu cha msingi kuhusu kupekuliwa ni kwamba, kwa mujibu wa sheria, mtu anatakiwa kupekuliwa kati ya mchana hadi jioni, yaani kipindi ambacho jua linachomoza na pale jua linapokuchwa tu, na si vinginevyo.
  Kwa maneno mengine ni kwamba mtuhumiwa haruhusiwi kupekuliwa wakati wa usiku isipokuwa kama mahakama imeruhusu hivyo chini ya kifungu cha 40 cha sheria hii.
   
 18. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Mtenda hutendwa bila shaka na yeye alikuwa polis tena ngazi ya juu..
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Mijitu hii hatari sana. Zombe ni proven criminal. Nilikuwa na rafiki yangu Arusha aliwahi kupitia kadhaa za kuchunguzwa na Zombe....kwa kweli ni mtu hatari sana maana waliwatesa kwa dhalili za ajabu sana. Ni mtu katili, mwenye kiburi na ambaye ni mmoja wa wahusika wakuu wa mtandao wa uhalifu wa kipolisi (uliasisiwa na kukuzwa na rtd O. Mahita).

  Inajulikana vema kazi za mtandao huu Tz. Ni visa na rekodi chafu ya ujambazi katika mikoa ya Arusha, Dar, Mwanza, Tabora, Kagera, Shinyanga, Kilimanjaro na Tabora.

  Alipaswa awe hamna siku nyingi tu.
   
 20. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Ndio taabu ya kuwa na sheria mbovu...yaani hata Zombe anazungmzia "haki"? Katika jamii nyingine wangekuwa eliminated ila ninyi Tz ni tofauti
   
Loading...