figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
abdallah zombe amerudi tena.mara hii adai serka fidia ya bil5 na mil200 kama fidia ya ile kesi ya kuua wafanya biashara.
Watanzania tutaendelea kulipa fidia hizi zinazotokana nauzembe wa watendaji na viongozi wa serikali mpaka lini? ukichukua hili suala la Zombe, huyu bwana alipona mkono wa sheria kutokana na sababu za kiufundi; hivi sasa serikali italazimika kumlipa mabilioni ya fedha za walipa kodi. Zipo fidia nyingi zinazulipwa kwa makondrasi wa barabara kwa uzembe kama huo. Leo serikali inadaiwa fidia nyingi zinazotokana na mikataba mibovu. La kushangaza ni kwamba wakati watanzania masikini wanalazimika kukosa matibabu na elimu kutokana na matumizi hayo mabaya ya raslimali ya taifa, wale wanaosababisha hasara hiyo wanaendelea kupeta.
Abdallah Zombe afungua kesi ya madai akidai fidia ya shs bilioni 5.2. Wakati huo huo Jerry Muro na washtakiwa wenzake wamekutwa na kesi ya kujibu. RADIO1 STERE
Si mnataka haki za binadamu na demokrasia? mtu kakamatwa na madawa ya kulevya airport tena kayahifadhi kwenye rectum anapewa juice ya kuharisha anamwaga pipi kadhaa lakini utasikia tunafanya upelelezi ukikamilika atapelekwa mahakamani, huku nyuma mtu anaandaa namna ya kujitetea. wanasheria wanatuambia "somebody is not guilty until proved guilty and shall proved guilty in the court of justice" mimi si mwanasheria ila naamini nimeeleweka. Sasa kwa mtu aliyekamatwa na dope, bunduki na risasi bila kibali, pesa za moto nk kwanini wasinyongwe kama ilivyo Iran, Saudi Arabia, Syria na China? au akapelekwa jela moja kwa moja kuna haja gani ya kuanza kusikiliza kesi?
Kwa zombe askari wenzie walikiri kura jamaa alikua na mtandao wa majambazi na ndiye aliyeamuru wale mabwana wauawe na madini alichua yeye badala ya kifungo bila kesi au kungongwa ndiyo hayo sasa yanakuja na lazima alipwe kama akishinda kesi dhidi ya serikali. Cha msingi ni kuandamana kutaka sheria ya kumnyonga mtu pale anapopatikana na kosa la wizi, mauaji, rushwa na madawa ya kulevya. palepale amekutwa na pesa za moto au unga asomewe hukumu ya kunyonwa bila kujali ni ndugu yangu au ni nani itakua fundisho kwa wengine. Ukiandamana kupinga mtu kulipwa wakati mahakama yako imeshahukumu hivyo katika rufani zote itakua ngumu hata iwe ni chama gani kiko madarakani, njia ya kupinga hukumu ni kukata rufaa pekee na siyo tofauti ama la Zombe anyamazishwe kwa kuondolewa katika sura ya dunia.
Mkuu, sina uhakika kama walikata rufaa, ninachokumbuka mimi JK alisema wahajaridhika na hukumu ya mahakama kipindi ANAONGEA na wananchi kupitia runinga ya TBC1.lakini serikali ilikata rufaa kwenye kesi ya zombe baada ya kubwagwa. sasa atafunguaje kesi wakati rufaa haijaamuriwa?