Zitto: Wapambe wametufitini na Mbowe

Zitto: Wapambe wametufitini na Mbowe

Aje Sumbawanga akikusanya watu maelfu ya watu kwenye mkutano kama kipindi kile ,natembea mtupu.

Hahaha dogo hata lema arusha mikutano yake inakosa watu kabisa..Chadema imepoteza mvuto kabisa..Hakuna kiongoz wa Chadema anaejaza watu kwenye mikutano sasa hivi
 
I kind of agree with you. Zitto amekuwa akimstahi sana Mbowe wakati mwenzake ametumia kila aina ya fursa kummaliza kisiasa. Angalau angeanza na hili dili la hela za Singasinga wa Escrow. Angeweka wazi kabisa jinsi Mbowe na cronies wake akina JJ walivyovuta mlungula ili watu wajue aina ya upinzani uliopo nchi yetu.
Nyie ndio wapambe nuksi anaowasema Zitto.
 
Nimesoma hii kitu binafsi nimeumia na kujifunza kweli wapambe Nuksi,mtu muliyekuwa munasota wote na kugonga viepe bwenini leo marafiki wanakutenga naye.......Zitto anajutia hili kutoka ndani ya moyo, Naomba Kamanda Mbowe ukilipitia mwamanchi la leo tafakari juu ya huyu Kijana ikabidi muyamalize Chama kisonge mbele.....
 
ebu hata siku moja badilika, mbona mnapenda sana siasa za ubaguzi, wakati si misingi ya taifa letu, nilishawahi kusema hapa nyerere aliona mbali kutuunganisha kuwa wamoja bila kujali makabila na dini, sasa nyie mnaleta hivi mnajua madhara yake? hakuna vita mbaya kama ya ukabila na udini. mfano kenya na nigeria. tafakari.

Mkuu umeshauri vyema lkn huyo unayemshauri hashauriki,hapo utakuja mpk na matarumbeta lkn hazibuki masikio...... Udini na ukabila ndio formular ya hoja zake.
 
Zitto You are pathetic on this issue, kindly refrain yourself, Una Maana Gani wapambe ndio wamewachomganisha, kama wewe na Mbowe mmekuwa akili ndogo hadi vifaranga wanaweza kunmichonganisha, jee ikiwa hamuwezi kutofautisha uongo na ukweli jee mtaweza kuongoza nchi nzima, ambapo mtakuwa na mamilioni ya wapambe.

This is very cheap Politics from an astute politician like yourself, This is the time for you to come clean and expose the weakness and shortfalls of Mbowe, as the opposition needs clean, fair and Nationalistic Leaders, Weka wazi maoni yako kuhusu nia ya Mbowe kugombea Kiti chake kwa mara ya tatu tofauti na constitution ys Chama. Waelimishe wana Chadema ili wasimchague kiongozi batil, kama unao ushahidi kama huo, na kama una imani ya kuwa ana haki ya kugombea basi unapaswa kusema ukweli hapo....

sio cheap mkuu, intention nyuma ya hayo maneno ndio kila kitu....hii ndio siasa haswa!!!

historia inajiandika hapa.
 
kwa mtu anayekipenda chadema na kuitakia heri siasa ya upinzani tanzania, ni bora chadema wayamalize na zitto kwa mustakabali mwema siasa za upinzani waombane misamaha yaishe, maisha ndivyo yalivyo.
Naunga mkono hoja Kamanda........jamaa amejuta na kutubu,japo kiutu uzima lkn msj imefika,Hatuwezi kuZuia humu Jf kumshambulia Zitto lkn ningeomba baada ya kumaliza mashambulizi tutafakari mañeno yake na kuyapima......
 
Hivi kwanini Kabwe anapenda kurudia rudia kuelezea alichofanya CDM? mara nilifanya hiki na Mbowe wengine wakiwa CCM nk..

Namfananisha na mtu flan mcha Mungu sana ambaye amepigania sana imani yake,,kajenga makanisa/misikiti,,kawavutia wengi katika imani,,kaaminiwa sana na waumini wenzie,,lakini bahati mbaya kajaribiwa na kukengeuka ,,

Wakati mcha Mungu huyo akiwa siku za ubora wake katika imani yake,,kuna watu walikua walevi, vavuta bangi, washerati, wachawi na mengine yafananayo na hayo,,waovu hawa wakapata neema ya kuujua ukweli,,wakaamua kuacha dhambi zao na kuifuata imani ya mcha Mungu huyu,,

Kwakushindwa kustahimili majaribu,, mcha Mungu anaangukia katika dhambi. Wale waumini walioingia katika imani kwa influence yake wanabaki thabiti kiimani,,huku wakijitahidi kumuombea labda anaweza kujirudi,,

Ibilisi alivyonanguvu katika dunia hii,,anaendelea kuvita zaidi katika dhambi,,jamas anaanza kuwachukia waumini wale,,kila akiwaona wanaendelea vizuri katika imani roho inamuuma,,anaanza kuropoka hovyo, bila mimi msingeijua imani hii, wakati najenga msikiti huu flani na flani walikua majambazi,,sasa wanasauti nk,,nk,,
 
Sasa Chadema si mali ya Mbowe.? Chadema ni taasisi ya mbowe wengine ni misukule tu.
Wapambe nuksi, mmemponza mwenzenu hadi anatia huruma,

alifikiri ACT itavuma haraka kama uyoga leo kagundua kina Mwigamba, Kitila, Shonza, na nyie ndio mliomwingiza choo cha kike.
 
Binafsi naiona ni dalili ya ukomavu kwa Zitto. Ameeleza hali halisi baada ya tafakali ya kina. Hii ni changamoto kwa Mbowe. Naye anyoshe mkono wake wa kuume apokee salaam ya Zitto. Ni uungwana tu.

Kuna watu huwa hawajui kuwa mambo ya siasa yanaendeshwa na binadamu .Kila mtu anapaswa kujiangalia kama kweli yu malaika au ni binadamu wa kawaida. kuna watu leo wanamhukumu Zito kwa sababu tu ya mapenzi kwa chama lakini undani wa uendeshaji shughuli za chama hawaujui. Kila mamlaka hupata kudumu kwa sbb ya wigo mzito. Kuna siku wigo utavunjika.
 
Wapambe waliwafitinisha na Mbowe..... OK.. So what is the way forward?
 
Zitto bado ni maarufu. "Maua-ridi yaliyooza yananuka vibaya kuliko nyasi za kawaida" Ikiwa zitto atashindwa kutumia kipaji na akili alizonazo kutatua tofauti zake na chama chake harufu yake katika medani za siasa itaendelea kutoa uvundo. Lakini bado ninamatumaini na zitto.

- Lilies that fester smell far worse than weeds
 
Iangalie nafsi yako kwanza kabla ya kuhukumu wenzako.

Zitto alishajihukumu mwenyewe ni wa kutupa kwenye ziwa la moto tu, huyu angekuwa mfuasi wa Islamic state adhabu yake ingekuwa ni kuchinjwa tu kama kuku.
 
Mnaosema jamaa asamehewe huku anasema yeye ni mfwasi wa siasa za ACT mnasoma vizuri kweli, yaan wewe uwe chademe alafu unapenda siasa ya chama kingine kisa kunarafk zako zitto atamdanganya mjinga, kwa nini anataka watu wamuone anaugomvi na mbowe na kwanin anapenda kujiweka kundi moja na mbowe.amesahau chadema ndio ilimsaidia pia kuingia bungeni akiwa bado kijana.nafikiri kunakitu anakitafuta na hao waliompa ukurasa wakujielezea.
 
Back
Top Bottom