Si bado kesi yake iko mahakamani? Sidhani chama makini chenye wanasheria mahiri kama kinaweza kuidharau mahakama na kuendesha mambo kama Club ya Yanga.
Ndio kesi yake ipo mahakamani lakini kumbuka chama kilimvua nyadhifa zake kupitia Kamati kuu ya watu 10 kwa kuhofia kushindwa jaribio lao kwa kuitisha Baraza Kuu lililokua na wajumbe wengi wanaomuunga mkono Zitto. Kwa maana hiyo kupitia Baraza Kuu isingewezekana kumuondoa Zitto Chadema na zaidi huenda hicho ndo kilimpa kiburi na kujiamini.
Kama ilivyo ada kwenye Siasa kucheza michezo michafu ikabidi kanuni na taratibu za chama zikiukwe kwa kuitisha Kamati Kuu la mtu 10 fasta bila kuhusisha Baraza na kumvua nafasi zake zote.
Ikabaki kazi moja tu ya kumvua uanachama. Kama unakumbuka ndo viongozi waku wakaenda mikoani. Slaa akaenda Kigoma na Tabora na Mbowe akaenda Mwanza kisingizio ikiwa ni kwamba wanaenda kukiimalisha chama lakini ukweli ni kwamba walienda kuwaandaa wanachama na viongozi Kisaikolojia na kupunguza damage ndani ya chama kwa kupiga propaganda.
Wakarudi dar kwenda kutoa hukumu wao kama Kamati Kuu pasipo kulihusisha Baraza Kuu ambako tayari zitto ashakata rufaa kuwa kesi yake ikasikilizwe huko. Zitto akawa ashausoma mchezo akajiwahi mahakamani na kwenda kuweka pingamizi juu ya uanachama wake kujadiliwa na Kamati kuu bila kusikilizwa Rufaa yake aliyokata kwenda Baraza Kuu.
Hapo kumbuka wakati wanamvu Zitto nyadhifa zake ndani ya chama na ile ya uwaziri kivuli alikata rufaa ndani ya chama kuomba kesi yake ikaamuliwe na Baraza Kuu badala ya Kamati Kuu.
Baada ya Kamati Kuu kukaa yakutokea yakawa yametokea ndo yaliyopelekea Kitila na Mwigamba kufukuzwa na Zitto akawa ametengwa na chama chake baada ya kuweka pingamizi mahakamani.
Muda wote ambao kesi ipo Mahakamani viongozi wamekuwa wakifanya kazi moja tu. Kuhakikisha wanafagia watu wote wanaomuunga mkono Zitto ndani ya Chama hasa wale walioko Baraza Kuu. Kila wanapojua kuna mtu anayemuunga mkono zito ni kumuundia zengwe na kumchafua. Na wengine wakawa wanajiudhulu kila wanapoona hali si shwari ndani ya chama. Baada ya uchaguzi zimekuja au kuletwa sura mpya zinazoamini kwenye zidumu fikra za Mwenyekiti either kutokana na wengi ushindi wao umetokana na nguvu au sapoti ya makao makuu.
Hii ichukue na uiweke kwenye kumbukumbu yako.Baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na genge lake nakuhakikishia ndani ya siku mbili hata kabla wajumbe wa Baraza Kuu kurudi mikoani mwao hapohapo ndo itapita na agender ya kumvua uanachama Zitto kwani tayari Mbowe alichokua anakiogopa tayari keshakitanzua kupitia uchaguzi.
Na msingi wa kesi iliyoko mahakama kuu ni kuwa Zitto anataka Rufaa ya kesi yake isikilizwe na Baraza Kuu. Ina maana Chadema itakuwa inatekeleza agizo la mahakama. HAPO UPO????
Huo ndo mchezo unavyochezwa kama ulikua hujui na ujue. Zitto ana akili sana ashasoma mchezo wote usishangae kusikia kauri zake kama hizi kwasababu anajua ni nini kinaenda kutokea tarehe 16 au baada ya hiyo tarehe. Kwani watu aliokua akiwategemea Baraza Kuu kuu kutoka mikoa mbalimbali tayari hawapo tena wameshafagiwa kwa 80%.
HIZI NI SIASA CHAFU SANA KWENYE CHAMA KINACHOJINASIBISHA NA KUJIPAMBANUA KAMA CHAMA CHA DEMOKRASIA.