Zitto: Vikao na Wanachama wataamua tubaki au tutoke SUK

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kauli ya Zitto imetokana Rais Mwinyi kumteua Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ambapo chama hicho kinapinga kwa madai alihsika kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo, amesema kabla ya kuingia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) walienda kwa wanachama na hivyo wanarudi kwao kupata maamuzi.

Amesema "Tunakwenda kuwapa taarifa hali ndio hii tuendelee tu au tutoke ili tuingie kwenye mapambano ya mabadiliko tunayoyataka, tunawapa mamlaka hayo wanachama na vikao vitafanya maamuzi,".

=======================

Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakioni dhamira ya kweli ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka maridhiano.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kinaenda kukutana na kamati za uongozi za matawi zaidi ya 600 Zanzibar kwaajili ya kuomba taarifa ya hali halisi ya kisiasa kisiwani humo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous Faina ambapo chama hicho kinapinga uteuzi wake kutokana na yeye ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume hiyo wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mchoteka Jimbbo la Tunduru Kusini leo Jumatano, Novemba 16, 2022, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kabla ya kuingia Serikali ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) walienda kwa wanachama.

"Kabla ya kuingia Serikali ya Umoja wa Kitaifa tulienda kwa wananchama kwanza wao wakasema msimuachie nguruwe shamba la mihogo tuingie tufanye mabadiliko," amesema

"Tunakwenda kuwapa taarifa hali ndio hii tuendelee tu au tutoke, tuingie kwenye mapambano ya mabadiliko tunayoyataka, tunawapa mamlaka hayo wanachama yatakuja kwenye vikao tutafanya maamuzi," amesema Zitto.

Zitto ambaye yuko kwenye ziara Wilaya ya Tunduru ikiwa ni muendelezo wa ziara za ujenzi wa chama na kusikiliza kero za wananchi ameseama hiyo ndio hali waliyonayo kwa sasa.

"Tumepambana kweli, napozungumzia tume huru tunaelewa, mama Samia (Suluhu Hassan- Rais wa Tanzania) aliunda kikosi kazi cha kuratibu maoni kuhusu hali ya demokrasia, tume huru iweje ili leo na kesho asije kuchaguliwa mtu ambaye hakupigiwa kura," amesema Zitto

Alipotafutwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alisema hawezi kutolea ufafanuzi suala hilo hadi atakapolifuatilia na kujiridhisha kwa kuwa yuko kwenye mchakato wa uchaguzi wa ndaani ya chama.

Tayari kamati maalumu ya Kamati Kuu ya upande wa Zanzibar imekutana katika kikao cha dharura chini ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud kujadili hali ya kisiasa kisiwani humo.

Kamati hiyo imeiagiza sekretarieti ya chama upande wa Zanzibar kuratibu vikao vya ndani vya viongozi, wanachama na wafuasi kutoa maoni yao.

MWANANCHI
 
Hakuna wa kumsikiliza Zitto naona anatafuta namna ya kurudi tena kwenye kutafuta umaarufu maana sasa hana tofauti na Fahmi Dovutwa wa UPDP.
 
Safi sana jambo hili ndilo ambalo tunalitaka kuvunja kabisa SUK, jamaa kabadilika 100%, rangi zake zote sasa zinaonekana
 
Back
Top Bottom