Zitto: Tunapokea bil 640 na tumepoteza tril 1.8 ya capital gain ya makinikia kwa ubabe usio na tija

Zitto kitu ambacho hajui ni kwamba Acacia bado inaweza kununuliwa na kampuni nyngne tukapga ndege wanne kwa jiwe moja,tukapa tax gain ya tr 1.8 ,plus bil 700 za sasa ,bado tukawa na 50/50 pamoja na 16%,Magu piga kazi baba tuko nyuma yako
To buy acacia at this moment is risky business.
 
Cha kushangaza hata hizo bil 640 zinatolewa kwa grounds zipi? Tunapoozwa tu au ndio tuliomba "msituache mikono mitupu"
Kama ulimsikia bwana J. Thornton, alisema wanazitoa kwa nia njema, labda kutupunguzia makali ya umasikini. Mkuu kasema anataka zilipwe haraka, sasa sijui alichosema bwana Thornton kimekuwa nadhiri?
 
Stock ya acacia ilivyoshuka unadhani bei itakua ileile?
Alafu sasa hivi wanasema tunaenda 50/50 profit usidhani kuna kampuni itatoka nje ije kununua acacia tena. Labda iwe kwa bei ya kutupa ambapo hatutoweza kupata hata hiyo robo ya 1.8.

Kitu kizuri kilichotoka kwenye haya mazungumzo labda ni huko kugawana profit 50/50 na hapo ni kama kila kitu kitaenda sawa, labda na kutuma message kwa makampuni bongo kua Tanzania sasa haitaki mzaha. Japo tumetuma pia message kua hatujielewi so tunafukuza investors.

BAHARI,
Graph,Nimekuelewa lakini kuna vitu amtu anaweza kukuringia kama mwekezaji sio gold Ndugu leo kila nchi inayo endela inataka kuweka reserve ya gold wachina,Brazil,Vietnum,India NK.Na hisa zilishuka sawa ila kupanda kwake haita chukua muda Gold ni bidhaa nyingine sio pamba wala kahawa inaitwa GOLD.Dini lenye thamani namba tano duniani.

LUMUMBA
 
Zitto kitu ambacho hajui ni kwamba Acacia bado inaweza kununuliwa na kampuni nyngne tukapga ndege wanne kwa jiwe moja,tukapa tax gain ya tr 1.8 ,plus bil 700 za sasa ,bado tukawa na 50/50 pamoja na 16%,Magu piga kazi baba tuko nyuma yako
Ni kweli kabisa unapokuwa mpinzani si kila jambo lazima jambo upinge kuna mambo mengine unatakiwa kupongeza kwa hili rais amethubutu na faida kubwa inaonekana kwa taifa.
Tumepata bilion 700 pamoja na mazagazaga yake lakini pia bado biasha ya kuuza inaweza ikafanyika na huku mazungumzo yakiendelea kwa manufaa ya watanzania na taifa kwa ujumla nikukumbusho Mhe. Zitto kwa hili umechemka,
Mwanasiasa aliyeiva huwa hapingi kila jambo ila pele mwana siasa mwenzako anapofanya jambo zuri unapaswa kumpongeza na huo ndiyo uungwana, uzalendo na kujali inchi yako hongera JPM

WAVEJA SANA NKOI.
 
Nyie kina Zitto ndio eti viongozi tunaowategemea!!!! utaendelea kuwadanganya hao hao ACT waliobakia.
"Eti kuna maaongezi yalikuwa yanaendelea ya kuuziana Accacia.... kweli mmeshikwa pabaya. yaani unatuaminisha matarajio hewa.
 
Hatuna rais bali mkurupukaji asiyetaka ushauri
Angeachia mchanga huku mazungumzo yakiendelea ila kama kweli tumepoteza hizo trilioni 1.8 kwa kuzuia makinikia then tukapata bilioni 700 tu ni zaidi ya upuuzi na phd zetu ni feki kabisa

Hii kweli Tanzania ya viwondor
Samani Ipi hiyo wakati makinikia yanyewe ilikua licha ya underpriced madini menge yaliyokuwepo kwenye makenikia hayakutajwa? Je kwako ni furaha makenikia yangeendelea kusafishwa tukisubuli hiyo timu yako? Hii n
 
Lakini Mimi naona makubaliano mengine ni zaidi ya pesa ambapo nchi inaweza kunafaika zaidi kwa muda mrefu zaidi kama vile 50 kwa 50 na serikali kumiliki hisa ya asilimia 16 Mimi naona si haba ungawa zitto anabeza kila kitu
 
Zitto angesubiri hiyo week moja halafu ule mchanga ungekuwa wapi? Wote kusema kweli hatupendi wizi wa kupindukia na uzembe ulifanywa na chama tawala mpaka inafika tunaomba kinga ya marais wastaafu iondolewe. Lakini kwa mapenzi ya nchi tunaunga mkono juhudi zo zote za kweli kupigania haki yetu na maendeleo ya kweli. Sasa nyie wapiga dili kwa kupitia siasa msituchanganya kabisa. We wala huwezi kujinadi kama kiongozi wa mfano. Wacha Kamba hapa unapinga kwa sababu ya kupinga uonekane umesema na wala si kwa uchungu au imani na mapenzi ya nchi, wacha kubabaika.
 
Hizi pesa ni kama zimeombwa angalau kufuta aibu .ndio maana ataa kifungu cha kampuni ya barick cha kuidhinisha kutolewa pesa kilicho tumika ni Good Faith kifungu hiki utumika kutoa misaada .fungu la kumi kanisani na kadhalika .Ndio maana kimetajwa wazi na kwa msisitizo na kampuni ya barick kwa sababu ndicho atakacho tumia kuelezea na kuombea pesa hizo kwa wanahisa wa barick ambao ndio wenye mali .kama alivyo jieleza kwamba anakwenda kupata ruksa baada ya kuwakilisha makubaliano kwa wenye hisa .kwa maana nyingine wenye hisa wanaweza kukataa makubaliano hayo na sii ajabu na mbaya zaidi hakuna kosa walio patikana nalo zaidi ya kwamba tumewatia hasara kuwasimamishia biashara yao .kwa lugha ingine hii ngoma bado mbichii
Vyovyote iwavyo mabadiliko yaliyofanyika yana manufaa kwa siku za

usoni
 
Zitto tatizo unaendeshwa na matukio, ifike wakati muweke wazi hoja zenu,
Je, rais alikosea kuzuia makinikia?
Je, Rais alikosea kuunda kamati za uchunguzi wa mchanga na madini?
Wewe kama zito ungefanyaje ili Tanzania inufaike na madini yake?
# upinzani wa kijinga sana huu
 
HABARI,
Ndugu wacha kutudanganya watanzania kama toka mwezi march tumepoteza hiyo pesa sasa kwa mwaka mzima utataka kusema tulikuwa tunapata trillioni zaiidi ya trillioni 5 hakuna njiga wa kumdanganya tanzania na kweli magufuli alisema hivi ni vita vya uchumi na bado atawanika machafu yote na uzembe mliokuwa mnaufanya .
Wewe ni JF-Expert Member toka mwaka 2012 miaka yote wakati jamaa wanachukua madini yetu mlikuwa wapi au ndio mlikuwa na mirija humo.

Watu wamebanwa mpaka wamekubali kutoa 50/50 na 16% ya hisa juu jiulize kama toka mwazo wangebanwa kwa mkataba kama huo tungekuwa tumepata kiasi gani cha fedha .Watanzani hatujalogwa ila kuna walafi wachache ambao kwa sasa wamebanwa ndio hawa wanaopingana na matendo ya JPM.

Nyie tukaneni andikeni chochote ila idadi kubwa ya watanzania tuko upande mmoja na Raisi wetu kwa maslai ya nchi Hizo dolla m.300 kama angekaa kimya mngezipata wapi ni zaidi ya bilioni 700tsh,Sasa kwa kuwa nyie ni watu wa kupiga mahesabu vizuri changanueni ni zahanati ngapi hapo zinaweza kujengwa ni pesa ya kulipia wanafunzi wa elimu ya juu karibia miaka 2 ukiongeza hela kidogo hapo.Na bado tunaanza kupata pasenti yetu juu.
Nyie mnaopinga ni nini kingine mnataka Raisi afanye njue ndio anauchungu na nchi yetu .

LUMUMBA
Wewe ni Lumumba wa Congo eeh!
Unauliza uwepo wa Zitto kwenye hoja za madini,are you ok kweli au?
Zitto alikuwepo kutafuta maslahi bora ya madini kwa watanzania wakati LUMUMBA ya Tanzania inamtoa nje bungeni.
Ni kama Tundu Lissu alivyotokwa na jasho huko kanda ya ziwa akiteteta wenyeji wa maeneo ya madini na Taifa linufaike,na kwa hoja zilezile tena za sasa ni dhaifu munakuja kumpigia mtu makofi aonekane ni mkombozi wakati Lumumba wenzio walikuwa watokwa na jasho kuzuia mijadala yebye maslahi na "masiah"akiwemo.
 
Nadhani lugha za staha zingetujenga zaidi katika kuwasilisha hoja zetu. Pia tukumbuke kuwa akili ni nywele kila mtu ana zake.... Tujikite muda wote kwenye hoja. Kugawana profit 50/50 kwangu mimi naona inaweza kutuingiza kwenye shida kubwa kama taifa. Ikumbukwe kuwa kuna wakati kampuni inaweza kupata "negative profit" kwa kiswahili tunaita hasara. Faida hii nayo kama wanahisa ambao tunagawana 50/50 ni lazima pia tuigawane kwa uwiano huo huo. Wasomi na wachumi hasa wale wenye phd ebu tusaidieni hapa hesabu hii haili kwetu? Nawasilisha.
 
Tumepoteza uaminifu kwa wawekezaji igawa tumelipwa kifuta jasho sio deni afadhali wangesema tumelipa kodi tuliyokwepa hili ni baya kwa kundi la wafanyabiashara duniani kumbe tulikuwa waongo ila tunataka kupewa sehemu ya faida katika biashara ambayo hatujawekeza jamani
 
Back
Top Bottom