Chama ni watu na Zitto ni miongoni mwa wanaokijenga Chama Cha Demokrasia na Maendeleo- Kusema anautaka urais hakibomoi chama. Mwentekiti na Katibu na Baraaza la Wazee watakuwepo kukikuza chama Zitto ataongoza Nchi kupitia CHADEMa tatizo liko wapi? Au kuna mtu mmesha muandaa kugombea urais 2015? The early the better tukuze emokrasia ndani ya chama. wajitokeze wanaotaka watangaze nia, tuwachuje mapema kama walikuwa na madhambi wapiga kura tujue. Mnaogopa chama kitasambaratika, hamjakomaa kupambana na misukosuko ya kisiasa? Lazima tutofautiane mawazo, fikra, mitazamo na hisia mwisho wa siku tukubaliane kukubaliana. MAMBO YA ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI HATUZITAKI.
Zitto kaona isiwe taabu maana ilikuwa too much sasa wengine wakawa wanampa sifa za kumsanifu hadi wana CCM wakajiunga ikawa kama kum kejeri vile, lengo kumchonganisha na viongozi wakuu. Eti uongozi wa juu haufai ni Zitto tu anaweza kuwa mwenyekiti. Zitto kaliona hilo vibaraka wameachwa peupe wamebaki kulalamika pembeni labda waje na singo nyingine.
Unaonesha uko so desperate, sawa na mtu aliyekata tamaa kwa kukosa kitu alichotumaini. Pole sana.Unalalamika post ndefu eeh...acha kusoma vichwa vya habari na magazeti ya udaku.Ndiyo maana wamewagundua wakaamua kuwatumia tu kuchafua watu hovyo hovyo.Ninyi mnakubali tu
Infact,your posts are laden with so much bigotry that it rarely makes sense for those who do not live in your mind there. only sycophants will support your malicious and scandalous post that can never make impact in the general view anyways.
You are worth to be ignored for now.....! endeleeni kumfanyia Ben monitoring!
Kuutaka urais si dhambi na hakusema yeye ndiye anayefaa kuliko yeyote ndani ya chama chake, alichosema ni kwamba katiba iliyoko inawanyima fursa vijana kugombea urais na kama fursa hiyoingekuwepo naye angejitosa kuuwania. Kwa hiyo silioni kosa hapo. Nature ya binadamu ni progressive yaani ni endelevu kwa hiyo si vibaya na kuwa na malengo ya baadae. Baada ya kumpima sawasawa kijana huyu imegundua ni makini kwelikweli na yuko commited na chama chake kulikowatu wanavyofikiria. Ni mkweli, jasiri na mvumilivu na ni hazina tosha ndani ya chama chake, chama cha ukombozi mpya wa Tanzania - CHADEMA.
Kasoma alama za nyakati kajifunza kwa kakaye shibuda mambo ya kuropoka ropoka yamemgharimu na chama kipo juu kina naelekea ikulu. Kafulila kafulia vibaya na njama za kumpindua chairman, hakuna rafiki labda magamba.
Kamanda Zitto hongera kwa ujumbe wako ila inabidi na ww ujirekebishe mienendo yako ya kuwa na kauli tata kama za huko nyuma pia jitahidi safar hii uwe na teamwork na sio kushinda na magamba manafiki kama jmakamba na lile limbunge la kigoma mjini ambao hutumia daraja la ukijana kuhadaa wananchi, pia Zitto hakikisha misimamo yako iliyotofautiana na chama chako unaitolea huko huko chumbani kwako au bafuni ukiwa unaoga kuliko kuitoa hadharani na kuwapa magazet ya magamba haedlines.
Ni hayo tu.
Zinamyeeshea kutokea Kaskazini.
Kasoma alama za nyakati kajifunza kwa kakaye shibuda mambo ya kuropoka ropoka yamemgharimu na chama kipo juu kina naelekea ikulu. Kafulila kafulia vibaya na njama za kumpindua chairman, hakuna rafiki labda magamba.
Na angethubutu kugombea tu angeundiwa TUME. Kasoma alama za nyakati. Bora awe nje ya uongozi wapange wanayoyataka.
ZZK ni mtu makini sana, anajua fika kwamba nafasi pekee anayoihitaji ni uenyekiti wa chama, na kwa kutumia makundi hasimu ndani ya chama inngemuwia vigumu sana kupata nafasi hii, pia anaelewa kabisa kugombea uongozi chadema ni kujitangazia uadui maana nafasi za uongozi zina hati miliki.
NI uamuzi wa busara sana, lakini hautokani na ZZK kutopenda uongozi isipokuwa kuelewa kitakachomtokea.