Na wewe kama yamekushinda huko Chadema si uhamie kwenye hiki chama kimya?
Bado mnajadili haya mambo tu? you guys .........!
Hivi na leo kasemaje?
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.
Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama, alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
UPDATE:
Kairudia kauli hii Juni 16, 2012 akiwa Iringa (M4C)
Una matatizo mkubwa weye!Wana JF wenye mapenzi mema kwa chadema, nadhani ni muda muafaka sasa kuanza kutoa maoni kuhusu chama chetu hasa uongozi wake maana uongozi ujao ndio utatupa serikali 2015. kwanza nimpongeze sana Mbowe kwa kweli ameonyesha ujasiri mkubwa na ameongoza chama kwa ujasiri na ukakamavu mkubwa. Huwezi kuitaja chadema ya leo bila kumtaja Mbowe. Baada ya kazi kubwa na ili kuonyesha chadema kina watu wazuri wengi wanaoweza kuongoza, ningeshauri tu asigombee tena akae pembeni ila abaki kwenye vikao muhimu vya chama.
Nashauri Dr Slaa sasa angeandaliwa kuwa Chairman, Zitto Kabwe awe makamu Bara, atafutwe katibu mkuu msomi mzuri ambaye anaweza kuratibu shughuli za chama kisomi, Naibu katibu pia awe msomi mzuri, tuwe na graduates makatibu wa kila jimbo la uchaguzi ambapo kazi zao itakuwa kufanya uratibu wa chama, hope chadema tutakuwa tumepiga hatua zaidi towards state house. Ni maoni tu. Peoplessssssssssssss Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Unataka kutuambia kuwa Mbowe pekee ndie anaweza ndani ya Chadema? Chadema ni chama kikubwa kwa sasa nadhani tutakuwa tunaonyesha njia kama tukiendelea na utaratibu wetu wa kubadilishana kijiti hata kama tuna kiongozi imara kama Mbowe. Nyerere alikuwa kiongozo shupavu ila alifika mahali akaonyesha ukomavu wa kisiasa akang'atukaUna matatizo mkubwa weye!
Mbowe aondoke?
Halafu chama amwachie nani?
Maoni yako ni feki, Mbowe elimu alonayo inatosha kabisa kuongoza CDM,wewe yaonyesha humjui Mbowe na CDM. Mbowe ni shupavu, mzalendo, mwaminifu, mhamasishaji na mtu wa watu. Ana umri wa miaka 51 akae pembeni kwa lipi?