Mh Zitto Kabwe Mbunge wa Kikoma Kaskazini
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hali ya vurugu zinazoendelea Mtwara katika sakata la mradi wa gesi asilia kuja Dar es Salaam. Picha na Venance Nestory
Na Boniface Meena na Aidan Mhando (email the author)
Posted Jumatatu,Januari28 2013 saa 9:0 AM
Kwa ufupi
Mradi huu ungegharimu Dola za Marekani 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka. Huu mradi haijulikani umeishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya katika mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara?
SHARE THIS STORY
0
inShare
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kuwa majibu ya tatizo la wananchi wa Mtwara analo Rais Jakaya Kikwete hivyo ni muhimu akarudi nchini mapema na kuyatoa majibu hayo.
Wakati Zitto akisema hayo, Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amesema njia pekee ya kumaliza mgogoro huo unaondelea ni Rais Kikwete kutoa tamko la kukubali kufuliwa umeme katika Mikoa ya Kusini.
Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamano, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kutokana na wananchi wa Mtwara kutaka kujua ujenzi huo utawanufaisha vipi.
Akizungumzia hali hiyo, Zitto alisema ni muhimu Rais Kikwete akaeleza baada ya kuagiza kufufuliwa kwa mradi wa kufua umeme wa Mnazi Bay utekelezwe mara moja.
Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme megawati 300 eneo la Mnazi Bay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida umeishia wapi, alisema Zitto na kuongeza;
Mradi huu ungegharimu Dola za Marekani 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka. Huu mradi haijulikani umeishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya katika mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara?
Alisema ni muhimu Rais Kikwete akarudi kutoka huko aliko ili kuwapa majibu hayo wananchi wa Mtwara ambao wamekuwa wakiandamana kutaka kujua hatma yao.
Zitto alisema kwa hali ilivyofikia ni muhimu vilio vya wananchi wa Mtwara wakasikilizwa na madai yao kueleweka na majibu ya maswali yao yasiwe ni ahadi bali vitendo.
Kwa upande wake, Mtikila alisema Rais Kikwete analazimika kutamka bayana kipaumbele kwa uboreshaji wa Bandari kuu ya Mtwara, ikibidi hata kwa kusitisha mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Tunatoa tahadhari kwamba hali inayoendelea kuwa mbaya huko Kusini inazidishwa na ukosefu mkubwa wa uzalendo na hekima katika utawala wa CCM, alisema Mtikila.
Mtikila alibainisha kwamba ni vyema ikaeleweka kwamba madai ya umeme wa gesi ufufuliwe Kusini yanatokana na uchungu wa wananchi wote wa Kusini mwa Tanganyika Mtwara Corridor.
Kitu cha msingi kinachotakiwa kufanyika ni kuwasikiliza watu wa Mtwara wanataka nini lakini, siyo kutumia nguvu katika maamuzi (uamuzi) ya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo la gesi kwani kufanya hivyo ni kuzidi kuwaongezea uchungu Wanamtwara, alisema
BONYEZA WEB HII
MICHUZI: MASASI YAZIDI KUCHAFUKA,WATU SABA WADAIWA KUPOTEZA MAISHA