Zitto: Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara!

Zitto: Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara!

Lema yuko kamati kuu amenitumia meseji ili niweze kumrushia , amesisitiza kuwa zit to anakiherere

Wewe ni mchochezi, Lema aje aseme mwenyewe usimweke maneno mdomoni. Mimi nilivyomuelewa Zitto anajibu mashambulizi yalioelekezwa kwake moja kwa moja na naibu waziri.
 
Nafikiri kila mtu anakushangaa. Kuna uhusiano gani Kati ya Ohms law na madai ya wananchi kuhusu raslimali na hasa gesi. Au ni ya Prof anayewataadharisha wananchi wasiwasikilize watu walioudhuria mafunzo ya wiki mbili kuhusu gesi lakini wakati huo huo anawaomba watoe maoni kwenye sera ya gesi (iliyoandikwa kwa kiingereza)! Wananchi ambao hata hayo mafunzo ya wiki hawajapata!

Sera hazitengenezwi na watu waliosoma Ohms law ndugu yangu.
Safi mkuu mimi mwenyewe siielewi hayo madudu na sidhani mwananchi wa kawaida anahitaji kuyajua ili achangie mjadala wa gas.
 
Ndugu zangu Hakuna sababu yeyote ya kuweka tafsiri nyingi kuhusu suala hili. Najua kwamba chama chetu kitatoa msimamo wa chama kuhusu suala hili. Press yangu wala haina nia ya kuharibu tamko la chama. Mie nimejibu mapigo ya Simbachawene. Suala hili lina baraka za chama na Kwa kweli Hakuna sababu ya sisi kama chama kutofautiana kwenye suala hili.

Kauli ya chama itatoka


Kamanda kama ndivyo nakupongeza,ila heading ya Press release yako ingemlenga moja kwa moja Simbachawene .Hayo mengine ningependa niyaone kwenye press release ya chama . Ama umeyaweka ili tukiyaona kwenye press release ya chama tujue Zitto ndio alichangia haya !
Pia sio kila Waziri anapokubeza ujibizane naye ,wananchi na wapenda mageuzi tutapima na kumpa majibu huyo kiongozi kwa vitendo kama Hawa Ghasia ,Mkuchika ,Kasembe na Anna Abdalah wanavyopewa majibu kwa vitendo .

Badilika kamanda ,ur falling hawakwambii ila wanakusifia kinafiki wakifurahia anguko lako .
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Zitto yuko sahihi kwa mtizamo wangu.

Kafanya consultation within the party na karuhusiwa kutoa tamko lake dhidi ya shutuma zilizoelekezwa kwake na naibu waziri Simbachawene.
 
Statement kama hii ilitakiwa itolewe na chama na sio individual. Kama hivi ndio ZZK kasema, jee kesho M/Kiti wake atasema nini?.

Mkuu ZZK, japo ulikiri wazi kuwa hutauzungumzie tena urais 2015, kitendo hiki cha kutoa hii " presidential stetement" iliyokuwa well crafted as if wewe ndio rais, hauoni ni kama kuuzungumzia urais kwa mlango wa nyuma?. Nilikushauri fanya mambo ya kuwadhibitishia Chadema, wewe ndio unae fit kuipeperusha bendera from within, ili Wachadema ndio wakuone unafaa na kukuomba ugombee!, hivi kwa mfano, statement kama hii, ungempa M/Kiti wako aijumuishe kwa press conference yake, huoni ingekuongezea mileage ndani ya chama kuliko kutoka solo?!.

Binafsi ZZK namkubali sana kama ninavyomkubali EL na ikitokea tunatofautia huwa namwambia kama nilivyo mshauri EL asiende Arumeru, angemponza Sioi, alienda na kweli akamponza!, ZZK nilimshauri "" sasa anaendelea, licha ya yeye kuwa ndie the best that Chadema has so far, kama asiposimamishwa kuwa mgombea wa Chadema 2015, asimlaumu mtu, "anayakoroga mwenyewe",atakuwa hana budi, "ayanywe".
Pasco.

hapa kazi ipo
yaani kiongozi unamaanisha kuwa Mh Zitto kayaongea yote na hakuna jipya litakaloweza kuongelewa na M/Kiti? lakini mbona kila mbunge ktk Tanzania kayasema yake juu ya Gesi ya Ntwara,sasa kayasema Zitto imekuwa ni tatizo?
navyoona mimi Mh Zitto kajibu hoja ya mNaibu waziri ambaye amemtaja zitto kwa jina kuwa mchochezi ktk swala la gesi na zitto ana haki ya kujibu hilo maana lime elekezwa kwake na si kwa CDM kama chama.
 
Wewe ni mchochezi, Lema aje aseme mwenyewe usimweke maneno mdomoni. Mimi nilivyomuelewa Zitto anajibu mashambulizi yalioelekezwa kwake moja kwa moja na naibu waziri.

Mkuu,
Hiyo isikusumbue, JF kwa sasa imeingiliwa. Kuna conspiracy humu hata kama hujawahi pata mafunzo ya sarakasi za ulinzi haiwezi kukupa shida kubainisha.

Watu wako kazini bana.

Flip flop your mind, hii ndiyo Tanzania ya leo.
 
Tufike mahali tuache ushabiki wa kitoto. Mkapa aliongea, Mnyika aliongea, Dr Slaa aliandika mtandaoni, na sisi tunaandika kila siku humu mtandoni maoni yetu. Mbona sijasikia mtu akisema Mkapa au Mnyika au Slaa au Simbachawena wana viherehere kwa kutoa maoni yao kabla ya vyama vyao? Why Zitto? Tuache chuki, hazijengi chama.
 
Zito katamka: Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara?
Ni kweli Serikali ikieleza ukweli wa mambo hakutakuwa na shida yoyote. Hivi si inajulikana kuwa umeme wa kwenda Singida ungekuwa ni DC na unabadilishwa ukifika Singida. Just imagine ingekuwa ni 300kv lakini wa kinyerezi utakuwa ni 900kv. Wapi na wapi. Inavyoonyesha ni vita kati ya big shot na Wachina. Its time now wajuzi wa mambo hasa TANESCO kueleza hali halisi. Umuhimu na faida za kuzalisha umeme kinyerezi upo wazi ila inaumiza unapoona wanasiasa wakakaa kimya. Hivi unajua kuwa kama mpango wa awali ungefanyika umeme ungekuwa senti 12 na huu wa sasa umeme utakuwa senti 8? Hivi ni nani asiyejua kuwa makampuni ya nje yangefurahi kuuza hii gesi nje kama India na China baadala ya kutengeneza umeme ambao utainufaisha TZ. Hold on jamani, acha wenye data wamwage hapa JF.
 
Kamanda kama ndivyo nakupongeza,ila heading ya Press release yako ingemlenga moja kwa moja Simbachawene .Hayo mengine ningependa niyaone kwenye press release ya chama . Ama umeyaweka ili tukiyaona kwenye press release ya chama tujue Zitto ndio alichangia haya !
Pia sio kila Waziri anapokubeza ujibizane naye ,wananchi na wapenda mageuzi tutapima na kumpa majibu huyo kiongozi kwa vitendo kama Hawa Ghasia ,Mkuchika ,Kasembe na Anna Abdalah wanavyopewa majibu kwa vitendo .

Badilika kamanda ,ur falling hawakwambii ila wanakusifia kinafiki wakifurahia anguko lako .
utayaonaje kwenye tamko la chama,wakati Mh amejibu hoja iliyopelekwa kwake,Naibu waziri hakutaja chadema kama chadema,yeye ametaja jina la Mh Zitto na kikawaida Mh Zitto amejibu kile kilicho upande wake na chama kitasemea yaliyo ya chama,acheni kuona kila anachokisema Mh Zitto kina kasoro,hivi umejaribu kusoma zile makala zake? unataka kusema hakutakiwa kutoa makala hizo hadi chama kiridhie?
tupunguze chuki na tuwe waungwana wadau
 
Wewe ni mchochezi, Lema aje aseme mwenyewe usimweke maneno mdomoni. Mimi nilivyomuelewa Zitto anajibu mashambulizi yalioelekezwa kwake moja kwa moja na naibu waziri.
Mimi nawashangaa sana hawa watu mkuu, maana juzi tu yaliletwa maoni ya dr Slaa aliyopost mtandaoni kuhusu hili suala. Sote tuliyaunga mkono na hakuna alosema Dr ana kiherehere. Why Zitto?
 
Mkuu Pasco;
Mahaba yako kwa ZZK yamevuka mpaka. In actual fact sio mahaba kwa ZZK tu, ila ni lengo lango na dhamira yako ya kuona CDM inavurugika ili kuwaondolea vizuizi maCCM! Yaani unajifanya hukubaliani na hatua ya ZZK kutoa tamko kabla ya chama lakini at the same time unampigia ZZK debe la kutosha. Acha unafiki Pasco, ZZK is wrong!
Mkuu Chigwiyemisi, nakiri udhaifu wa kuwa too frank to speak my mind regardless mawazo yangu yatamfurahisha nani na kumuudhi nani!. Kama una uwezo wa kuona lengo langu na dhamira ni kuona CDM inavurugika ili kuwaondolea vizuizi ma CCM, then naomba nikupongeze. Wewe ni bonge la psychic!, una uwezo mkubwa kuona malengo na dhamira yaliyo mioyoni mwa watu!, big up!.
Pasco.
 
utayaonaje kwenye tamko la chama,wakati Mh amejibu hoja iliyopelekwa kwake,Naibu waziri hakutaja chadema kama chadema,yeye ametaja jina la Mh Zitto na kikawaida Mh Zitto amejibu kile kilicho upande wake na chama kitasemea yaliyo ya chama,acheni kuona kila anachokisema Mh Zitto kina kasoro,hivi umejaribu kusoma zile makala zake? unataka kusema hakutakiwa kutoa makala hizo hadi chama kiridhie?
tupunguze chuki na tuwe waungwana wadau
Umenena kamanda. Mbona wengine wengi ndani na nje ya cdm wameshaongea? Kunya anye kuku....
 
Kaka Zitto taarifa yako haina ubaya wowote bali tatizo wewe huaminiki kabisa, kwani tulishang'atwa na nyoka sasa hata tukiguswa na jani ni lazima turuke,

Pia kilewo naye ameksoa busara ktk hii thread.
 
Last edited by a moderator:
Umenena kamanda. Mbona wengine wengi ndani na nje ya cdm wameshaongea? Kunya anye kuku....
mkuu
kuna watu humu wanataka kutufanya watanzania ni wajinga sana,wanataka kutufanya kuwa hatuwezi kusoma na hata picha hatuoni pia.Mh Zitto sio mjinga,anaelewa nini kinaendelea na hawezi kufanya mambo kwa kukurupuka maana anaelewa ipo chuki na upotoshaji unaoendelea,sasa walitaka maneno aliyoyasema Naibu waiziri juu ya Zitto yaende bila kujibiwa na yasubiri kujibiwa na chama,kuna mawili hapa,kuna ya chama na kuna ya mtu binafsi
katajwa Zitto inabidi ajibu yeye kama zitto,kingetajwa CHAMA msemaji wa chama angekisemea chama.huwezi subiri msemaji wa chama aje kumsemea zitto.
Tubadilike,kila mtu atimize wajibu wake
 
Muda mfupi ujao Mheshimiwa Zitto Kabwe atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mgogoro wa gesi, na kutoa mapendekezo kuhusu namna ya kupata suluhu. Utafanyika katika Hotel ya JB Belmont, Benjamin William Mkapa.

===========
Update:

Ifuatayo ni kauli ya Zitto Kabwe katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam, leo. Chini yake kuna kauli ya Ikulu iliyowahi kutolewa pia katika vyombo vya habari Oktoba mwaka juzi Katika kulinganisha kauli hizi mbili, Zitto anaona serikali inajikanganya, na inatafuta wachawi wa mgogoro wa Mtwara, badala ya kutafuta suluhu. Zisome mwenyewe.

TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA
MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA



Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara

Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko miradi mingine yote ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini. Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani 1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China.

Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27 Desemba 2012 wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na mradi huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.

Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya wananchi wa Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa ikijaribu kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya habari.

Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya hadhara na hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo, kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.

Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikia tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.

Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaani matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara si Utanzania. Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa kuwashirikisha, hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.

Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro huu.

Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala hili limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakichochea wananchi wa Mtwara.

Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press conferences’ jana Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawene aliwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.

Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika Mtwara. Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu, kama Mtanzania kuhusu suala hili.

Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa nchini na kwenye blogu yangu (zittokabwe.com).

Niliandika: Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Nikaandika tena: Tusipuuze mandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji; Nikaandika tena: Mtwara : Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi; ni baadhi ya makala nilizoandika kuhusiana na suala la Mtwara.

Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na kurushiana maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.

Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya iwapo tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.


Rais Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara

Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa.

Tufanyeje?

Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio cha wananchi wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia suala hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize kwanza.

1. Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi itakapopatikana.

2. Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.

3. Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za orodha ya miradi isiyotekelezwa.

Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama vita vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu wa chama kutoa ridhaa.


ZITTO KABWE

Mbunge, Kigoma Kaskazini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni

=============

Zitto ameambatanisha na statement ya Ikulu hii hapa -> https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...waambia-nini-wananchi-wa-lindi-na-mtwara.html
TAARIFA YA DEMOCRATIC PARTY (DP) KUHUSU
GESI NA MASLAHI YA MTWARA CORRIDOR
DP tunatoa tahadhari kwamba hali inayoendelea kuwa mbaya huko Kusini mwa Nchi yetu, inazidishwa na ukosefu mkubwa wa uzalendo na hekima katika utawala wa juu wa CCM, kiasi cha kuzidi kuumwagia gesi moto unaowaka badala ya kutumia historia ya tatizo lenyewe ambayo peke yake ndiyo inayoweza kuwapa busara ya zimamoto! Tunapenda ieleweke kuwa madai kwamba umeme wa gesi hiyo ufuliwe kule kule Kusini yanatoka katika uchungu wa wananchi wote wa Kusini mwa Tanganyika yaani Mtwara Corridor, uchungu wa kudhulumiwa, kudhalilishwa na kusahauliwa kabisa kimaendeleo tangu tulipotapata uhuru mpaka leo. Serikali ndiyo chombo hasa cha kuzungushia gurudumu la maendeleo, ambalo lilielekezwa Kaskazini tu mpaka Kusini kukabaki pori na giza nene, kiasi kwamba watumishi wa umma walipokuwa wanapangiwa kufanya kazi Kusini, mara nyingi ikiwa kama adhabu, waliamua kuacha kazi. Kupuuza upande mmoja wa nchi kimaendeleo huwa ni bomu la hatari litakaloteketeza hapo baadaye, kama inavyokuwa hivi leo Wananchi wa Mtwara Corridor wanafahamu kwamba sumaku ya wawekezaji wa miradi mikubwa ya kuwaletea maendeleo ni nishati na miundombinu, lakini watawala wa CCM waliwanyang’anya Reli ya Kusini kwa uharamia wa kung’oa mpaka mataruma na kufutilia mbali hata na tuta lenyewe! Wananchi wa Kusini ni binadamu wanaoumia kwamba hata barabara ya kuwaunganisha na dunia nyingine haijaisha mpaka leo, lakini wanayaona makufuru ya ufujaji wa kutisha wa serikali ya CCM hiyo hiyo wa mabarabara ya Jijini Dar es Salaam sasa kukwanguliwa lami nzuri kabisa ya mabilioni ya fedha, ambayo ingeishi zaidi ya miaka saba mingine! Serikali ndiyo yenye jukumu la kuweka misingi yote ya uchumi wa nchi, kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na maisha bora ya wananchi wenyewe, lakini mbali ya ule uharamia wa kuwang’olea ile reli, fungu la uboreshaji wa Bandari ya Mtwara ambayo ndiyo yenye kina kikubwa zaidi cha asili kinachofaa zaidi kuliko hata bandari ya Dar es Salaam, sasa ni fungu la kujengea bandari ya Bagamoyo nyumbani kwa Kikwete, ambapo ni hatua kadhaa tu jirani ya Dar es Salaam! Zao la pamba ambalo utawala wa mkoloni ulilijengea msingi imara kwa ajili ya uchumi wa nchi na wananchi wake, lilishamiri vizuri zaidi Kusini kama ulivyoshamiri hata mkonge. Lakini kwa kutowathamini watu wa Kusini na kutojali kabisa hatima yao kiuchumi na kimaisha, utawala wa CCM uliyanyima mazao hayo kipaumbele kule na hata ule msukumo unaopasa, wakati kule Kaskazini mwa nchi hiyo hiyo umeme ulisha sambazwa mpaka migombani! Zao la korosho lililobaki angalau katika uwezo wao ulio duni, limekuwa kama mnyororo wa utumwa, kwa sababu wakivuna hawapati kitu bali kupunjwa kabisa bei kama zikinunuliwa. Ni zao linalotajirisha sana ma--------- kwa kuwakondesha vibaya sana walalahoi wa Kusini.
KUHUJUMIWA KWA MAONO YA SHUJAA OSCAR KAMBONA
Watu wa Mtwara Corridor wanafahamu kwamba shujaa Oscar Kambona ndiye hasa aliyefanikiwa kuiombea Nchi yetu msaada wa China wa Reli ya Uhuru, na uwezo wake wa kisiasa na hasa baada ya kung’ara katika ukombozi wa Afrika na uhusiano wake binafsi na Chou en Lai ulivyotusaidia. Tunajua kwamba kwa ajili ya hazina za Taifa letu za mafuta na gesi kule Kusini, pamoja na rutuba isiyo kawaida kwa ajili ya kilimo, pamoja na raslimali za madini ya thamani njia yote, achilia mbali wanyamapori Selous, na chuma cha Liganga na mkaa wa mawe Mchuchuma, reli hiyo ilikuwa ianzie Bandari ya Mtwara iliyopangiliwa pia uboreshwaji wa nguvu, na ilikuwa iende mpaka Ziwa Nyasa baada ya kona ile ya kwenda Liganga na Mchuchuma hadi Rukwa kwenye shaba. Hauwezi kusahaulika ushuhuda kwamba baada ya shujaa Kambona kuelezea baraza la mawaziri mafanikio haya ya safari yake China, na hasa Bandari ya Mtwara na reli ya uhuru wetu wa kiuchumi, alitukanwa na mkuu wake kwamba ni mkabila sana, kwa ‘kosa’ la kutaka hiyo miundombinu ya bandari na reli iwe Kusini! Mzalendo Oscar Kambona alijitetea kwa hekima ya rohoni kiasi cha kuwatoa machozi baadhi ya wenzake kwamba, “Mimi si mkabila wala sina kosa, kama kuna mwenye makosa basi ni Mwenyezi Mungu”. Alipotakiwa aeleze ana maana gani alisema, ‘Kwa sababu Mungu angetuwekea kule Kilimanjaro au Musoma hizi hazina za gesi, mafuta, madini ya thamani na Selous ya wanyamapori, chuma na mkaa wa mawe na shaba reli ingepita, lakini sasa alikosea akaweka Kusini. Hakuna mwehu wa kubisha kwamba maono haya ya hayati Oscar Kambona yalikuwa ya uzalendo wa hali ya juu kwa ajili si ya watu wa Kusini, bali kwa muujiza wa maendeleo ya kiuchumi ya Taifa la wana wa Tanganyika kuwa katika kilele cha Afrika na hata dunia. Hatushangai kwamba ingawa shujaa Oscar Kambona ndiye aliyeanzisha Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), kwa maono yake binafsi ambayo Nyerere ilibidi ayaafiki, Kambona akayauza kwa rafiki yake mpenzi Ahmed Sekou Toure aliyempa cheki tupu ya kwanza, wakamhusisha shujaa Kwame Nkurumah aliyetoa cheki ya pili, na walipomshirikisha Mfalme Haile Selasie naye akatoa cheki ya tatu, shujaa Oscar Kambona akaupambisha moto wa ukombozi wa Afrika, mpaka wivu ulipompiga vita kali hadi akaikimbia Nchi yake. Ni dhahiri kwamba watu wa Kusini ya Tanganyika au Mtwara Corridor walikuwa na sababu ya kumpenda na kumheshimu hayati Oscar Kambona, kwa sababu maono yake kwa ajili ya hatima ya Taifa letu yalikuwa baraka kwao. Lakini hakuna hata choo ya Jiji iliyoweza kuitwa jina la shujaa Oscar Kambona, licha ya sifa na heshima aliyoiletea Nchi yetu, hii ni aibu! Nyerere alipogeuka kuwa adui mkuu wa shujaa Oscar Kambona watu wengi wa Kusini waliteseka kwa ajili hiyo, na koroboi ya maendeleo Kusini ilionekana kuzimika kiaina, hadi ilipoibuliwa upya na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) mikakati mipya ya maendeleo ya Kusini, kwa jina la Mtwara Corridor, iliyofanyiwa kazi kwa dhati na mzalendo Simbakalia ambaye sasa ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Koroboi hiyo ikazimika tena alipoondolewa huyu kutoka NDC.
UFUMBUZI WA MOTO WA HASIRA ULIOLIPUKA KUSINI
Moto huu usipozimishwa kwa hekima ya hali ya juu, si ajabu ukaimeza mikoa yote ya Kusini yaani Mtwara, Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro na hata Rukwa, tukakuta yanazaliwa mataifa mawili mpaka ukiwa Reli ya Kati! Tumeeleza kwa kifupi sana historia na sababu za msingi za hasira za watu wa Kusini, kwamba wao pia ni binadamu, na kwamba lugha yao ya amani ilipuuzwa kwa miaka yote 52 tangu nchi yetu ilipopata uhuru. Lakini tunapinga propaganda za uwongo za watawala waliosababisha hasira hii, kwa ukweli kwamba: 1. Watu wa Kusini hawazuii gesi isitoke kwa sababu ni nyingi sana na hazina yetu ni ya pili duniani kwa uwingi. Wao wanataka umeme ufuliwe kule kule kwa sababu utaleta mapinduzi ya maendeleo kule. 2. Faida ya pili ni kwamba nyaya zitakazo zoubeba umeme kuupeleka mpaka Kenya na Uganda tukitaka, lazima njia nzima zitakuwepo transfoma za kuusambaza mpaka miisho yote ya nchi mpaka vitongoji vyote. Kwahiyo wananchi wa Kusini ndio wazalendo na siyo watawala wa CCM. 3. Wanataka mabomba ya gesi yaanze kuisafirisha baada ya kufuliwa umeme, ili na yenyewe pia humo njiani yachomekwe mabomba yatakayoieneza nchini kote, kusudi iwe nishati mbadala ya Taifa kwa ajili ya kuiokoa miti yetu kwa ajili ya vizazi vyetu vyote vijavyo. Mungu ametuzibulia hazina ya gesi wakati nchi yetu inaelekea kuwa jangwa kutokana na kuteketezwa miti yote kwa kutumiwa kama nishati. Hawa ndio wazalendo na siyo watawala wa CCM. 4. Ukweli kwamba ufisadi wa kutisha umetembea katika mikakati hiyo ya kuufulia hapa Jijini umeme wa gesi ya Kusini, hivyo kwamba kiburi cha watawala na kutojali maslahi ya Taifa kama umeme utafuliwa kule kule Kusini, ni kwa sababu mafisadi hawana jinsi kwavile mabilioni ya watu walishakula sehemu kubwa, na sasa wanatafuta kulazimisha ili wapate lile fungu nono la mwisho. Saa ya ukombozi ni sasa! Njia pekee ya kuzimisha moto huu kule Kusini na kurejesha amani ni Rais Jakaya Kikwete kutoa Tamko la kukubali kufuliwa umeme kule kule Kusini kwa sababu ni kwa maslahi ya Taifa. DP tupo tayari kufanya usuluhishi kama kutakuwepo uwazi kwa upade wa serikali, kwa ajili ya hatima ya Nchi yetu. Rais Jakaya Kikwete analazimika pia kutamka bayana kipaumbele kwa ubereshaji wa Bandari kuu ya Mtwara, ikibidi hata kwa kusitisha mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Hii ni kwa maslahi ya Taifa letu. Rais Jakaya Kikwete anapaswa kutamka bayana kuhusu ukamilishaji wa barabara ya Kusini. Rais Kikwete anakabiliwa na utanguaji wa ufisadi wote uliofanyika Mtwara Corridor mpaka Ludewa kwenye miradi ya Chuma cha Liganga na Mkaa wa mawe Mchuchuma. Saa ya ukombozi ni sasa! Mchungaji C. Mtikila, Mwenyekiti 0713 430516
 
Umenena kamanda. Mbona wengine wengi ndani na nje ya cdm wameshaongea? Kunya anye kuku....

"Huwezi ukawa mshabiki au mfuasi wa Zitto alafu uchadema na ukamanda wako ukabaki salama"
 
Last edited by a moderator:
Another individualism ya Zitto. Namshauri akae na wenzake watoe as a team

Kama angekuwa na busara wangefanya na Mnyika.


Inawezekana isewe kweli!
Hizi chuki zitazaa kitu tu,tuendelee kuwepo na kushuhudia madhara ya chuki hizi ndani na nje ya ulingo wa siasa.
msimfanye Mh Zitto ni mjinga,mpaka kafikia kufanya hiki ni lazima amefuata protokali zote za kichama,maana anaelewa kuwa kuna chuki na wapo wasiotaka yeye kufanya kile kilichoelekezwa kwake kama zitto kwa jina na sio chama,wapo waliofurahi kauri kutoka upande wa pili juu ya maneno ya kumwelezea Zitto na ugumu wa mambo Ntwara,mlitaka akae kimya asijibu,amejibu anaonekana ni kiherehere,angekaa kimya mngemwona ni mjinga,akilalamika mngesema analalamika sana,nini mlitaka afanye ili mridhike na je mmeulizia ktk chama chenu kuelewa kama amevunja sheria,taratibu na kanuni za chama chenu?
Mnatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuzi na chuki zenu.sisi tusio na mapenzi na siasa mnatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuzi kweli na ubaguzi wenu.
 
Zitto your an enemy of the people? Badilika acha ubinafsi.
ubinafsi upi amefanya,je umewasiliana na chama na ukaelezwa kuwa Mh Zitto kavunja sheria furani? tueleze ni sheria ipi aliyovunja,ili nasi tujue.
je ktk maelezo yake,kakisemea chama ama kasemea yanayomhusu yeye zitto kama zitto?
 
Back
Top Bottom