Zitto: Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara!

Zitto: Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara!

Kama viongozi wa juu wapo kimya....wacha ZZK aongee yumkini ana jambo linaloweza kuwacomfort watu wa Mtwara. Ikumbukwe kwa sasa wanaMtwara wamejiunga wakiamua kufanya jambo lolote wanafanya..mf kuweka vizuizi barabarani. kupiga mawe magari ya serikali n.k....wanajaribu kufikisha ujumbe kwamba wanataka kusikilizwa......
 
Muda mfupi ujao Mheshimiwa Zitto Kabwe atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mgogoro wa gesi, na kutoa mapendekezo kuhusu namna ya kupata suluhu. Utafanyika katika Hotel ya JB Belmont, Benjamin William Mkapa.
Mohamedi Mtoi naona na wewe ushanunuliwa na kambi ya Zitto mara hii. Kweli Pasco alikuwa sahihi kuwa "penye udhia, penyeza rupia..."
 
Last edited by a moderator:
Zitto ni waziri wa hiyo wizara anahusika na ni vyema atoe ufafanuzi chawene jana kaongea hutumbo
 
Muda mfupi ujao Mheshimiwa Zitto Kabwe atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mgogoro wa gesi, na kutoa mapendekezo kuhusu namna ya kupata suluhu. Utafanyika katika Hotel ya JB Belmont, Benjamin William Mkapa.

katiba inamruhusu kufanya hivyo,kujua au kuelewa kitu haina uhusiano na muda uliokaa darasani ni vyema hata ma prof nao wakakubali kufundishwa pale wanapokuwa awaelewi they cant be jack of all trade
 
Hivi tatizo liko wapi Zitto hapewi nafasi na chama?Au yeye ni mbinafsi?Nasikitika sana kuona kiongozi wa ngazi ya juu mara kwa mara akitoa hoja binafsi sio kwa maslahi ya chama bali kujikweza binafsi.
 
Binafsi sioni mantiki ya huyu Mheshimiwa kuzungumza kwa leo halafu kesho Mkiti wake Mbowe atoe tamko la Kamati kuu kuongelea kitu hicho hicho.

Huo ni ushauri wangu tu lakini
 
Hivi vikao vyao vimeisha na yeye ndio anatoa tamko ama kaamua kupre empty tamko la chama chao baada ya baraza kuu lao kesho? Hapa ndio mimi simuelewagi huyu jamaa , ama anataka kutoa tamko la kuinfluence maazimio ya hivyo vikao vyao? Dahhh......CDM kuna kazi kuba mbele yenu....
 
Mohamedi Mtoi naona na wewe ushanunuliwa na kambi ya Zitto mara hii. Kweli Pasco alikuwa sahihi kuwa "penye udhia, penyeza rupia..."

Mkuu.
Huu ni ukame wa maono ulio pitiliza ila kwa sababu una uhuru wa kuandika ume wiwa kufanya hivyo! Kwa kuwa nimeleta taarifa ya kulisha jukwaa ndio nimenunuliwa! Ningeiona taarifa hii na kukaa kimya ndio nisinge kuwa na bei?!

Endelea kusubiri...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mohamedi Mtoi naona na wewe ushanunuliwa na kambi ya Zitto mara hii. Kweli Pasco alikuwa sahihi kuwa "penye udhia, penyeza rupia..."
Tuache hizi wakuu. Hazijengi chama. Wewe, mohamed mtoi, zitto, wote ni wapiganaji, hata kama kuna mahali mnatofautiana kimsimamo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.
Huu ni ukame wa maono ulio pitiliza ila kwa sababu una uhuru wa kuandika ume wiwa kufanya hivyo! Kwa kuwa nimeleta taarifa ya kulisha jukwaa ndio nimenunuliwa! Ningeiona taarifa hii na kukaa kimya ndio nisinge kuwa na bei?!

Endelea kusubiri...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu mi nakupongeza sana maana we ni mmojawapo wa wapiganaji uliyeonyesha neutrality ya hali ya juu. Hawa wenzetu wanaojenga siasa za chuki hawalisaidii chama.
 
Moddy,
Siku zote mko mstari wa mbele kuwaita wenzenu masalia just because ni marafiki wa Zitto au wameongea jambo zuri kuhusu Zitto.
Sasa ni dalili nzuri kama umeanza kutambua kuwa kuongea nazuri kuhusu Zitto siyo kuwa masalia. Asante na hongera...
 
Asubiri wenzake watoe tamko la Pamoja baada ya kikao cha Kamati Kuu.Ana haraka za nini? Anataka kukipiku chama? Anataka kuonyesha yeye ni zaidi ya Mkiti wake Mbowe?

Isitoshe msemaji rasmi wa wizara hii kutoka upinzani ni John Mnyika.Kwanini asimheshimu mwenzie mwenye wizara?

Haya ndiyo mambo yanayofanya Zitto aonekane ana agenda ya siri dhidi ya wenzake chamani.
 
Hapo ndipo tunapokosea watanzania. Hii tabia ya kila kitu lazima mwanasiasa azungumze itatuletea matatizo. mimi naamini Ndugu Zitto hata Ohms law hajui ku state, sasa atawezaje kutuambia namna ambavyo gas itazalisha umeme.

Wake up! Anaenda kuzungumzia mgogoro na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kupata suluhu! Haendi kuzungumzia jinsi ambavyo gas itazalisha umeme!
 
Mkuu mi nakupongeza sana maana we ni mmojawapo wa wapiganaji uliyeonyesha neutrality ya hali ya juu. Hawa wenzetu wanaojenga siasa za chuki hawalisaidii chama.

Nashukuru mkuu! Tatizo la wengi naona ni kujenga uadui na mtu/watu ambao wanatofautiana ki-mawazo na ki-fikra na wakati mwingine kufanya hukumu ya majumuisho (collective judgement) mimi napenda tutofautiane kwa hoja, tupingane bila kupigana huku tukilinda misingi na itifaki za chama.

Nimefundishwa kukubaliana kutokukubaliana kwa hoja na mantiki,Unishawishi kwa hoja na mantiki nikukubali, lakini tukitofautiana kwa hoja na mantiki imaanishe kuwa umeshindwa kunishawishi na nimeona ombwe la kimantiki ndani yako.

Kushutumiana na kusingiziana kwangu hakuna nafasi maana kuna minya fursa ya kujifunza. MPAKA KIELEWEKE!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Naweka wazi siungi mkono hii press conference ya Zitto . Huu ndio utafutaji wa umaarufu uchwara kupitia media ,acha afurahishe fikra na tabia zake za ubinafsi .Watanzania wa Mtwara na Lindi hawapo /hawasimami na wanaojitafutia umaarufu kwa swala la GAS ,HAPA INASUBIRIWA KAULI YA RAISI JK PEKEE....

GAS KWANZA SIASA ZA VYAMA BAADAE
 
Back
Top Bottom