Zitto sasa apachikwa jina la 'DOWANS'

Status
Not open for further replies.
Kama mtu kakuboa unaachana nae....

Kuna baadhi yapersonalities [ambazo mara nyingi ni strong and bright] huwa zikipotea njia inawasumbua sana kurudi kundini, mmoja wapo ni ndugu yetu zitto. ana point muhimu kwa anlysis yake na yuko sahihi kwa upande wake, tatizo ametofautiana na wengi na dawa kubwa ni kujirudi; sometimes watanzania huwa inabidi tukubaliane hata kama tunajua kwamba baadhi ya makubaliano hayakuwa sahihi professionally... I hope atajifunza jinsi siasa ya bongo ilivyo-tofauti na za kijeshi

UKIONA NYANI KAZEEKA UJUE KAKWEPA MISHALE MINGI NA SI KACHOMWA MISHALE MINGI

KAAJI KWEIKWEI
 
Hawa jamaa wa KIGOMA wana matatizo ukishawapa pesa kidogo tu wAnasahau...

...Oyaa, 'unaleta utani au unatania'? ...Waha, waManyema, waBwari, toka mkoani Kigoma tumo wengi humu... don't generalized eti "ukishawapa pesa kidogo tu...!"
 
Hawa jamaa wa KIGOMA wana matatizo ukishawapa pesa kidogo tu wAnasahau. INANIKUMNBUSHA YULE DR. WALID KABOURU hivi aliishia wapi? Wahenga walisema ukiwa mwongo usiwe msahaulivu. Jina alilopewa linamfaa kwani huyo DOWANS hatujamwona yeye anasema tununue mtambo kwa manufaa ya taifa basi yeye ndiye Dowans. Kama anabisha atuambie basi nani mmiliki wa DOWANS.


Kuhusu jamaa wa KGM mzee hapo inabidi utuletee statistical data ili kukidhi hypothesis yako. Ila hili la mmiliki wa DOWANS, Mh. Zitto, alishalegea kabisa eti tununue tu mitambo, ishu ya mmiliki SIO MUHIMU KWA SASA.

Hawa ndo watu tuliowakabidhi matarajio yetu.


Kaazi kwelikweli.
 
Hawa jamaa wa KIGOMA wana matatizo ukishawapa pesa kidogo tu wAnasahau. INANIKUMNBUSHA YULE DR. WALID KABOURU hivi aliishia wapi? Wahenga walisema ukiwa mwongo usiwe msahaulivu. Jina alilopewa linamfaa kwani huyo DOWANS hatujamwona yeye anasema tununue mtambo kwa manufaa ya taifa basi yeye ndiye Dowans. Kama anabisha atuambie basi nani mmiliki wa DOWANS.

Mkereme, tafadhali tuombe radhi mkulu au wewe u mtani wetu? Jamaa wengine waliorudi kundini kama vile Danhi Makanga nao ni Wa-Kigoma?

Tafadhali kulu, tuombe radhi.
 
Pengine Zitto amejimaliza kisiasa kwetu wana JF na watanzania wachache waliokuwa wakimwamini. Kule Kigoma ambapo umeme ni mgao myaka nenda myaka rudi... bado anaweza kuwa ni Zitto yule yule ya mwaka 2005.

Nakumbuka alisema hatogombea tena ubunge mwaka 2010. Kama haikuwa strategy ya kuhadaa competitors anapaswa akae sawa .. kwani haka Kadowans kanaweza kutumika kummaliza. Ingawa si kwa Kigoma... bado wapo wapo kule!!!!
 
Mahesabu ya Rostam yalikuwa ni kununuan credibility kwa kumpata mtu kama Zitto kwenye timu yake.

Matokeo yake Watanzania wamestuka, badala ya Rostam kupata credibility kwa sababu ana Zitto, Zitto, kwa kujihusisha na causes za Rostam ndiye anayepoteza credibility.
 
Alianza na ndoto za kuwania rais.... sasa amekurupuka na Dowans....what else is new?amerikoroga alinywe sasa.
 
jina hili litamkumbusha kila siku kuwa makini naam hata sisi vijana wenzake litatukumbusha kuwa tuwe makini. Jina hili laweza kuwa maarufu na likafunika jina lake kizembezembe. Kuna majina yalianza kiutaniutani na mpaka leo vijana hawajui majina halisi ya watu hao.Mr Dowans kubali yaishe hiyo ndo siasa.
 
Hapa kunamchezo mchafu ambapo mafisadi wanataka kuua ndege wawili kwa jiwe moja.
1.Kumaliza Zitto kisiasa
2.Kutumia umaarufu wake kuwashawishi watu kununua mitambo hiyo

Adv. Jasha,
Nakubaliana na wewe kabisaa kuwa jamaa wameweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja na kujeruhi wa tatu (upinzani) vibaya sana.

Binafsi bado ninampa Mh. Zitto nafasi ya kusafisha hili doa alilojipaka mwenyewe.

Makosa makubwa mawili aliyofanya Mh. Zitto sio kuwa on the wrong side bali ni;
  1. Kufikiria kuwa anajua kuliko wengine wote hasa humu JF na hivyo kutosikiliza maoni yao
  2. Kutumia lugha ambayo si ya kistaarabu (iliyoonyesha dharau/ matusi) katika kutetea hoja yake

Utetezi wa Zitto uliofanywa na akina Dr. Slaa/ Mwanakijiji n.k., nao haukukisaidia CHADEMA na upinzani kwa ujumla kwani iliwafanya wananchi kutoelewa iweje wote watetee makosa ya wazi ya Mh. Zitto. Ni muhimu kwa Mh. Zitto kutafuta jinsi ya kujisafisha na angeanza kwa kukubali wazi kuwa alifanya kosa kuitetea DOWANS. Kazi tunayo.
 
Duu?? yameisha kuwa hayo ya Mr DOWANS tena??...
Ila ukweli unabaki pale pale kwamba kwa hili mpambanaji alichemka! Kwa mtu analytical kama yeye sijui alishindwaje kusoma alama za nyakati kwamba tulipo si pale pa mkuu kasema twende tu!

Ila kutenda kosa si kosa kosa ni kurudia kosa.. Zito naamini kwa hili umejifunza ... binafsi sijapoteza imani nawewe japo uliitia doa sana kwa jinsi ulivo kuwa unashupaaa kwa jambo tenge kama hili!.... songa mbele kamanda pengine utarejesha imani ya wengine.
 
Sioni sababu ya kumshupalia Zito.Alilewa umaarufu kiasi cha kutufanya wana JF mabwege na akifikiri kila atakachosema tutamsuport akifikiri JF ni upepo unaolekekea chama fulani,kwa hiyo maamuzi atakayosema na misimamo basi nasi tutaelekea huko.JF haina CHAMA,HAIMBEBI MTU,ila Inasupport,inalinda masilahi ya kila mmoja aliye MTETEZI,MWAJIBIKAJI kwa ajili ya taifa la Tanzania.
Give Zitto a break!Haina haja ya kumwita DOWANS,kwani inawezekana kwa jinsi alivyofikiri ndivyo alivyoona sahihi.Ni vyema aje huku JF ajieleze na kutoa msimamo wake ,na tumkaribishe upya kuendeleza mapambano ya kulijenga taifa.Kutofanya hivyo Automatically atakuwa amejibatiza bila ubishi kuwa yeye ni MR DOWANS
 
Advocate Jasha, mkuu salamu zako! Zitto hajamalizwa kisasa bali kajimaliza kisiasa. Hakuna mtu aliyemtuma ashikilie bango ishu hili la Dowans. Kama alikuwa ana lolote la kusema angesema tu lakini si kulitetea hivyo na kujibu electronically kama vile yeye anajua vyote.
Mi namheshimu sana Zitto lakini katika ishu hii amekosea stepu na ni vyema akikaa kimya akafanya tafakari na ndiyo aandike au aonge hadharani. Maana sasa hivi amejiaibisha!

Hivi mnajua kuwa tunawadai Dowans zaidi ya Bilioni nane? Tutazipataje?

Tukiinunua mitambo hiyo kwa bei chee, tukawakata na hela zetu, si itakuwa bora kuliko kukaa gizani?
Zitto anayafahamu hayo!

Hivi hiyo mitambo imechakaa ikiwa ubungo au ilichakaa kabla haijaletwa ubungo?
Kukodisha chakavu inaruhusiwa isipokuwa kununua chakavu ndo hairuhusiwi?
Wataalam wa manunuzi mnijuvye!
 
Jamaa ndo hivyo kaishakufa kisiasa sasa watakuwa wanamuwinda slaa,chonde chonde tegemeo letu Dr Slaa kuwa makini,mafisadi wana njia nyingi saana.
 
Hivi mnajua kuwa tunawadai Dowans zaidi ya Bilioni nane? Tutazipataje?

Tukiinunua mitambo hiyo kwa bei chee, tukawakata na hela zetu, si itakuwa bora kuliko kukaa gizani?
Zitto anayafahamu hayo!

Hivi hiyo mitambo imechakaa ikiwa ubungo au ilichakaa kabla haijaletwa ubungo?
Kukodisha chakavu inaruhusiwa isipokuwa kununua chakavu ndo hairuhusiwi?
Wataalam wa manunuzi mnijuvye!

Hume mkuu, mi naelewa kuwa unajaribu kuangalia upande wa pili wa shilingi lakini mi naendelea kukuonyesha ya kuwa tatizo ni kuwa the premise of the argument is wrong:
- Dowans ni kampuni halali? Sasa tuta-negotiate vipi na kampuni hewa?
Tunawadai bilioni 8? Sasa tutazipataje? Kwa kutaifisha mitambo yao si kununua mitambo!!!!! Yaani unataka kuniambia mitambo hiyo chakavu ni bilioni ngapi? Come on!
 
Sioni sababu ya kumshupalia Zito.Alilewa umaarufu kiasi cha kutufanya wana JF mabwege na akifikiri kila atakachosema tutamsuport akifikiri JF ni upepo unaolekekea chama fulani,kwa hiyo maamuzi atakayosema na misimamo basi nasi tutaelekea huko.JF haina CHAMA,HAIMBEBI MTU,ila Inasupport,inalinda masilahi ya kila mmoja aliye MTETEZI,MWAJIBIKAJI kwa ajili ya taifa la Tanzania.
Give Zitto a break!Haina haja ya kumwita DOWANS,kwani inawezekana kwa jinsi alivyofikiri ndivyo alivyoona sahihi.Ni vyema aje huku JF ajieleze na kutoa msimamo wake ,na tumkaribishe upya kuendeleza mapambano ya kulijenga taifa.Kutofanya hivyo Automatically atakuwa amejibatiza bila ubishi kuwa yeye ni MR DOWANS

Baba lao, mkuu, Zitto alishakuja hapa na kujitetea siku kadhaa zilizopita nitaomba utafute katika lile thread ndefu la Dowans. Utaona alivyong'ang'ania kutetea Dowans. Ndo maana nasema ni sawa watu kumwita Mr Dowans maana amelishikilia bango na anaonekana kuwa hataki kusikiliza maoni ya watu na kujiona ye ndo mjuaji sana. Tumwache tu ....
 
Wakuu nimeota ndoto kwamba mbali na watu kupiga kelele kiasi hiki hapa JF bado sirikali kwa ubabe imenunua zile machine za Dowans.
Sasa ikitokea hivyo na wengine wote wanaopinga ununuzi huu wakafanya U turn je sie wachukia mafisadi tutajificha wapi?
Hii ilikuwa ndoto tu. Lakini nina tatizo moja ndoto zangu mara nyingi huwa zinatukia baadaye. Ole wako nikiota umekufa! kesho yake twakuchimbia kaburi.
 
Baba lao, mkuu, Zitto alishakuja hapa na kujitetea siku kadhaa zilizopita nitaomba utafute katika lile thread ndefu la Dowans. Utaona alivyong'ang'ania kutetea Dowans. Ndo maana nasema ni sawa watu kumwita Mr Dowans maana amelishikilia bango na anaonekana kuwa hataki kusikiliza maoni ya watu na kujiona ye ndo mjuaji sana. Tumwache tu ....

Utetezi wa Mr Downs uko clear kwa kweli, hana haja ya kuja kujieleza tena na tena, Watanzania wataamua, kishajieleza vyakutosha. uKimsilikiliza vizuri Mr Mwakyembe utaona dhamira ya Mr Downs ilikuwa wazi kabisa, ununuzi wa Mitambo chakavu tena ya Wajina wake Downs. Alifikia hatua ya kutunga UONGO eti TANESCO hawajasikilizwa na Kamati ya Madini kitu alichokikanusha kwa nguvu zote mr Mwakyembe kwa kutaja hata tarehe waliyokutana akiwepo WAziri mhusika na MR Rashid na Timu yake ya TANESCO.

Eti anahoji sheria gani ya manunuzi inayokataza kununua vitu chakavu, anasahau kuwa hakuna sheria inayomkataza waziri kusaini mktaba akiwa nje ya nchi kama alivyomshupalia KARAMAGI na Buzwagi yake.Huyu twawezaje kumuamini tena huyu. Anaonekana ni mtu, Mwongo, Mzushi, Kigeugeu,Mwenye Kiburi,Kejeli,Dharau asiye msikivu na kibaya zaidi mtu mwenye tamaa ya UTAJILI wa haraka, mla rushwa na FISADI anayechipukia.
Anjifanya ni rafiki na mtetezezi wa mastahi ya wanyonge kumbe amebeba Bendera ya MAFISADI kuteka mali ya wanyonge.(Ushauri wangu ni kuwa huyu bwana hatufai na ameonyesha mfano mbaya sana kwa UPINZANI)

Imagine Mr Downs mpaka anatunga UONGO unafikiri hapo kuna nini. Kwa kifupi huyu bwana ZITO->Mr Downs kala hela. No way anaweza kulikataa hilo. Mazingira yote yanaonyesha kala Fwedha!!!!!!!! au kaongezewa hummer ya Pili. Sitaki hata kumsikia, kwanza kisha haribu chama na upinzani kwa ujumla, kauweka upinzani rehani.
 
Yaelekea fweza ni tamu, ni sabuni ya roho na ni wachache sana wasioweza kununuliwa. Zitto katika hili anachemka na umaarufu wake utashuka ghafla, na sijui kampeni za operseheni sangara ataongea lipi ikiwa jina lake ni Dowans.
 
Nilishawahi kuandika hapa kuwa trick ya kwanza ya ku m wine zito ni ile ya kumwingiza ktk kamati ya madini.Tunajua mult national company wamefany nini kwa kijana ili afunge mdomo,kwasababu mtego wa kwanza alisha unasa sasa imekuwa easy ku mfanya mdoli.Kwa maana hiyo hata ktk Dowans kijana anatumika na ma agent wa Mult national company.As you know mkono mtupu haulambwi bwana.Tlio ona mbali hatukupenda kijana akubali ule uteuzi wa JK ktk kamati ya madini.Coz tuliona tatizo litakuja mbele si mmeona sasa kijana kaamua kuwa medium wa RA.
 
Jamani hapa jukwaani kunatakiwa kuwa mahali pa wachambuzi makani.
sasa kama watu humu baso hawajaona jinsi mafisadi wa CCM walivyomwekea Zitto maneno mdomoni na kuyanyumbua basi watu hawa ni below standard kwa jukwaa.

Kwa kweli baada ya siku si nyingi itakuwa wazi kabisa kwamba Zitto alisema nini na maneno mengine yalitoka wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom