Zitto sasa apachikwa jina la 'DOWANS'

Status
Not open for further replies.

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Jamani, amini msiamini: sasa hivi Mheshimiwa Zitto kapachikwa jina la 'DOWANS'. Hivyo ndivyo nimegundua katika pitapita zangu hapa jijini Dar, katika magenge ya kahawa na sehemu nyingine.

"Kashangaza Wananchi kwa kutetea ununuzi wa mitumba ya Dowans, kwa nini basi asiitwe "DOWANS?" nilimsikia jamaa mmoja akiwaambia wenzake katika kijiwe kimoja cha kahawa Kariakoo.

"Barabara, jina hilo ni fiti kabisa kwake," mwenzake akajibu. "Kwani si mshirika wa Rostam?"

Hali kadhalika sokoni Magomeni niwasikia jamaa wakimtaja Zitto kama "Mheshimiwa wa Dowans"

MAMBO HAYO JAMANI!!!
 
Kazi kweli kweli amejizulia yasiyotegemeeka ali kuwa ni miezi michache imebakia kabla ya uchaguzi haaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Hao nao wamekosa kazi!kwani wakimwita Do'ns wanampunguzia nini?any way wanajifurahisha kwenye kahawa na muda unapita
 
Tayari tuna Mzee wa Vijisenti na Mzee wa hata majani tutakula lakini lazima rada inunuliwe
 
Hapa kunamchezo mchafu ambapo mafisadi wanataka kuua ndege wawili kwa jiwe moja.1.Kumaliza Zitto kisiasa 2.Kutumia umaarufu wake kuwashawishi watu kununua mitambo hiyo nimemsikiliza Zitto katika mahojiono yake hapa MAGAZETI YA TANZANIA VIA KENNEDY amezungumzia umuhimu wa kuzikutanisha kamati zote zinazohusika pamoja na Tanesco wizara na serikali kujadili tatizo hili ili kuondoa vaccum iliyopo kwani hapa kuna mazingaombwe.Kama Tanesco inakimbia kutoka katika kamati hadi kamati badala ya kukutanisha pande zinazohusika.Hawa mafisadi walipanga na kizicheza karata zao kwa makini na kusubiri muda mbadala wa kuishinikiza serikali kununua mitambo hiyo kwa vitisho vya kua taifa litabidi kubaki katika giza.Kwa makusudi kabisa hawakuchua hatua zozote za kuziba mapengo yaliyowachwa na baada ya kuvunja mikataba na mikataba mingine kumalizika?kama kuna.watts 140 zimepungu baada ya kuvunja mkataba walisubiri nini kutafuta njia nyingine za kufua umeme?Niwazi kwa makusudi walivuta muda ambao umeme utakua unahitajika na muda wa kununua mitambo utakua finyu au haiwezekani na kuacha alternative ya kununua mitambo hiyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Advocate Jasha, mkuu salamu zako! Zitto hajamalizwa kisasa bali kajimaliza kisiasa. Hakuna mtu aliyemtuma ashikilie bango ishu hili la Dowans. Kama alikuwa ana lolote la kusema angesema tu lakini si kulitetea hivyo na kujibu electronically kama vile yeye anajua vyote.
Mi namheshimu sana Zitto lakini katika ishu hii amekosea stepu na ni vyema akikaa kimya akafanya tafakari na ndiyo aandike au aonge hadharani. Maana sasa hivi amejiaibisha!
 
Unajua uchaguzi mkuu wa Tanzania umekaribia, sasa kuna namna inayofanywa ili kummaliza Zitto Zuberi Kabkwe (ZZK) kisiasa.

Hata akiitwa DOWANS yeye kama yeye hapungukiwi na kitu chochote kile.
 
Unajua uchaguzi mkuu wa Tanzania umekaribia, sasa kuna namna inayofanywa ili kummaliza Zitto Zuberi Kabkwe (ZZK) kisiasa.

Hata akiitwa DOWANS yeye kama yeye hapungukiwi na kitu chochote kile.

Ndio. Ee. Hata Mzee wa Vijisenti hakupungukiwa chochote kile kwa kuitwa hivyo. Au sio? Wahenga walinena hivi: 'Maneno Huumba'. Nadhani pia huumbua.
 
Last edited:
Hao nao wamekosa kazi!kwani wakimwita Do'ns wanampunguzia nini?any way wanajifurahisha kwenye kahawa na muda unapita

First Lady;

I think you are not in Tanzania au huwajui wabongo vizuri... sisi tunadanganywa kwa khanga, mashairi na udaku ...hii ni chachu tosha kwenye campaigns, kuna politicians wamewahi kuharibiwa na kupoteza nafasi na kama unakumbuka hata mramba aliwahi kuanguka, akina cisco, kihiyo, dito, dr. gama n.k. Kumbuka wapiga kura wengi si kama wewe mwenye knowledge ya ziada (i guess).

Just wait and see the impact to Dowans on Zitto, i can bet my nationality for that, there is a huge backslash inakuja unless awe mnafiki na kueleza zaidi au kuangukia baadhi ya watu

Yangu macho na masikio ila ya Zitto ni mazito haswaa
 
Hakuna mchezo mchafu, Rostam atawanunua wote wenye viherehere vya kaziramfuka. Maneno mengi atlast unahalalisha upuuzi.

Subiri mzee mzima wa karatu uone shughuli yake, nae kwisha habari yake. nania anataka kuendelea kuishi maisha ya kifukara.

They are using us!!!
 
Advocate Jasha, heshima mbele. Nakubaliana nawe. Nafikiri Ziitto kaingizwa mjini. Ama kwa kutokujua au labda mengine anayafahamu mwenyewe kama kweli hatagombea tena ubunge. Kwa vyoyote vile wapinzani wake wamefunga mabao mawili kwa mpigo. Kwanza wamemmaliza Zitto kisiasa na pili wamefanikiwa kwa kiasi kuonyesha kuwa upinzani sio lolote na hawaaminiki. Kama Zitto alikuwa na nia njema katika hoja ya Dowans na bado mitego hii akashindwa kuiona, basi kuna haja ya kuwapeleka wapinzani kwenye shule ya siasa.
 
Jamani mbona mnamsakama DOWANS a.k.a ZITO?
Mwacheni dogo wa watu, aliijia siasa ya TZ kwa RIVAS huku kuna NG'OMBE WASIOZEEKA MAINI.....! wametulia tuu!
ama kweli NGOMA IVUMAYO NDIYO IPASUKAYO.....!
 
Binafsi sioni kama kwa hili Zitto eti amejimaliza. Nadhani wengi hawakuelewa na hata hawataki kuelewa point ya Zitto. Halafu timing issue, wakati anatoa mapendekezo yake yale kuna baadhi ya vitu ambavyo havikuwa bayana. So I still find him as a VERY STRONG PERSONALITY ambayo ina THINK BIG. So sioni haja ya kumkatisha tamaa kwa issue hii ambayo iko wazi na logical.
 
Mi nadhani asilimia kubwa ya watu hapa JF tumemheshimu sana Zitto, lakini hata Obama alishakubali "I screwed up".
The sign of a great mind is humility and the willingness to admit fault and learn from mistakes. Siyo kung'ang'ania na kutujibu kama anajua kila kitu. Amesema anaendelea kushikilia msimamo wake wakati the premises of his arguments are false.
Ameleta ubishi ambapo angetakiwa kuonyesha upevu kwa kukiri kutojua na kutafakari. Tena tunaambiwa alikuwa nje ya nchi alipoandika majibu yake. Sasa hii inaonyesha hayuko makini.
 
Hawa jamaa wa KIGOMA wana matatizo ukishawapa pesa kidogo tu wAnasahau. INANIKUMNBUSHA YULE DR. WALID KABOURU hivi aliishia wapi? Wahenga walisema ukiwa mwongo usiwe msahaulivu. Jina alilopewa linamfaa kwani huyo DOWANS hatujamwona yeye anasema tununue mtambo kwa manufaa ya taifa basi yeye ndiye Dowans. Kama anabisha atuambie basi nani mmiliki wa DOWANS.
 
Hivi wakuu hapa JF kuna kidude mtu akitoa post nzuri unayokubaliana nayo unabonyeza "Thanks" Je kama mtu ametoa kitu kika Kubore unabonyeza wapi?

---Sipendi sana Generalisation of People. Eti jamaa wa KIGOMA!
 
Shapu mkuu, jamaa amebipu nini? labda ni mtani wenu?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom