Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Status
Not open for further replies.
Ben sijui kwann sijui sana siasa ila nilikua naona kama ndio uamuzi sahihi kabisa huo....kama anataka kwenda mbali kwa siasa za kitanzania ni lazima abake CDM tumeona wengi kina kaborou,lamwai walipoishia..kusema tu samahani ni shida gani

Mkuu wangu Maishapopote, mwebzetu anajiona ndo kaibeba CHADEMA mpaka jufikia hapo ilipo. Watu walivyokuwa wakimwunga mkono alifikri yeye ndo jiwe kuu la pembeni!!
 
Zitto ni makini na washauri wake ni makini pia, huenda maamuzi magumu anayotaka kufanya ni kuendelea na chama kwa kuomba msamaha. Maana hakuna kitu kigumu kama kuomba msamaha.

Sioni dalili ya huyu jamaa kuja ACT kama alivyotuahidi
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini

Kwa nini nyie chadema msieandae mazingira chanya yatayomshawishi Zitto aombe msamaha badala yake mnafanya maamuzi kwa mihemko ya kisiasa na sifa kwa public.Hii ni mbaya hasa kwa sasa ambako tunaelekea kwenye uchaguzi na tunahitaji nguvu moja iliyoimara,sisi wananchi tunaamini kwama Ukawa inaweza chukua nchi vizuri tu(tathimini:matokea ya serikali za mitaa ambayo ndo msingi wa ushindi wa ccm) ila nashangaa tena Zitto yupo na kiongozi mkubwa wa Ukawa huko kigoma alishawahi kwenda mtwara na Pro Lipumba. Je hii inaashiria nini kwa Uhai wa Ukawa?.Jamani Zitto anahitaji kufanya maamuzi sio magumu bali sahii basi Chadema mlioshika upini fanyeni na nyie kwa nafasi yenu maamuzi yatakayomfanya Zitto aone pia kwamba kuna uhalisia kwa kufanya 1 na 2 kwa maslahi ya chama na wana kigoma,kwani wazee wa chama si wapo,vijana wenzake wa chadema(halima mdee,mnyika,sugu na hata kafulila chini ya ukawa) hamuwezi watumia hawa kwa manufaa ya chadema jaman.Kumpuuza Zito ni kupuuza kura za kigoma kwa na watu wengine makusudi kabisaa,kama tumeweza kuwarudisha wakina Kafulila chini ya mwavuli wa ukawa Zitto ni nani hasa na kwa sababu gani hasa asirudishwe hata sio chamani ila ilimradi kura zisiende ccm wananchi tunataka mapinduzi halisia na visible ila hizi propaganda zinaturudisha nyuma kabisaa.
 
Picha ya Tabora .........angemtaja na Dr.Slaa kuwa aliachana na CCM ........
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini

Mbona wewe hujaomba radhi kutembea na sumu mfukoni kutaka kuua watu?!

Dogo acha hizo weweeee!!!!
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini

haya ndio maamuzi magumu.
 
Uamuzi mgumu ni ule wa kujiunga na kijana mwenzake Nchemba na kujiunga CCM iliyomfanya adhalilike kwa kukubali kutumika na kuanzisha chama akiwa ndani ya chama. Otherwise akumbuke wale wote walioanzisha CCJ wakiwa CCM walirudi kuomba msamaha na hadi leo ni mawaziri na vipaza sauti vya chama chao. Take or leave it ZZK.

Kwa hiyo Zito alijipa zamu ya kuongoza si ndio?


Zamu yake aliyokua ameahidiwa ilikua imetimia na wapambe na wapenzi wake wakawa wanamsafishia mtu wao njia ya kuongoza chama kisomi na kidemokrasia.
Alikua anajipanga kimikakati akiamini anakitumikia chama cha wapenda Demokrasia .
Tatizo liko wapi kidemokrasia.
Hayo mambo ya usaliti yanatoka wapi kwenye wakati huu wa mageuzi .
Huu ni woga tu wa Mbowe na maslahi yake.
Sio kweli kwamba Zito anachukiwa na wanachama ambao ndio waliosababisha chadema iwe na nguvu bali ni vita ya madaraka iliyoanza tangu Zito alipotangaza kugombea uenyekiti.

Ulikua ni upumbavu na kukosa mikakati ya wazee ndani ya chadema kumzuia Zito ili hali wangeweza wakamuacha akagombea na mbowe kwani kwa vyovyote Zito angeshindwa kwani wajumbe wengi walikua ni wachaga na marafiki wa Mbowe wanaomwona kuwa Mbowe bado alikua anafaa kuongoza chama.Hata hivyo wazee walishindwa kuiacha demokrasia ifanye kazi yake.Sasa chama kinaishi kwa vitisho na kutoaminiana.

Pia kwa watu wenye maono ya kushika madaraka hakuna haja ya kufukuzana kwenye chama. Hata chama kimoja wakati wa Nyerere kilitokana na vyama vingi vilivyokua na mawazo ya watu tofauti na Nyerere alijua kuwa kuna tofauti kubwa ya kimtizamo ndani ya chama kimoja lakini lengo ni kujenga taifa kwanza sio uadui.
Chadema kimekosa watu wenye dira kwa kuwatimua wakosoaji.Matokeo yake hata wananchi wanakua na wasiwasi wakuwajua viongozi wanaoweza kushika madaraka ya kiutawala kulingana na katiba iliyopo inayomtaka rais Slaa(mfano tu) kuunda serikali kwenye ngazi mbalimbali kuanzia mawaziri,manaibu,makatibu,wakurugenzi,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,makatibu kata na tarafa.Wote hawa tunategemea wawe ni makada wasafi wa chadema ili kuitokomeza kabisa CCM.Hata hivyo hakina dalili za CDM kuingia madarakani ndio maana wanagombea vyeo vya kitoto kabisa mpaka uanachama wanamnyima mtu.
 
Zitto umewafanyia watanzania kazi kubwa. Umefichua ufisadi mkubwa

Hata wakutukane wakutemee mate ila kazi Umefanya.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania bwana, hata nyoka wa makengeza mama wa mboga alipata zaidi ya hapa!
 
Chama cha mafisi ndo kinajitahidi kumtetea Zitto,mnadhihirisha nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom